KERO Barabara ya Mbalizi - Iwiji inayounganisha Mbeya Vijijini na Ileje no mbovu sana

KERO Barabara ya Mbalizi - Iwiji inayounganisha Mbeya Vijijini na Ileje no mbovu sana

  • Thread starter Thread starter Anonymous (a103)
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
WhatsApp Image 2026-02-05 at 18.53.36.jpeg
Mimi ni Mwananchi wa Wilaya ya Mbeya Vijijini nina kero ambayo inatutesa sana wakazi wa huku.

Kero kubwa iliyopo ni ubovu wa barabara ya kutokea Mbalizi, hadi Iwiji ambapo inapita Isangati, Santilya, Ilembo, Shigamba hadi Iwiji na hii inaunganisha Mbeya Vijijini na Ileje.

Tangu uhuru hii barabara haijawahi kuwekwa kwenye mkakati wa kuweka lami japo kila kipindi cha uchaguzi Wanasiasa wanainadi kwamba watahakikisha inakuwa kwenye kiwango cha lami lakini haijawahi kujengwa kwenye kiwango hicho.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kupitia CCM alitoa hoja bungeni Tarehe 03/02/2026 kwamba ujenzi unaohitajika ni Kilometa 10, wakati ni zaidi ya Kilometa 30, tunaamini kupitia JamiiForums labda Serikali itatukumbuka kwa njia hiyona kutengeneza Barabara ili kutuepusha na kero.
 
Back
Top Bottom