Barabara ya Mandela,DSM Kiama

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaoitumia barabara ya Mandela (zamani Port Access) mtakubaliana na mimi kuwa kwa miezi miwili barabara ile mekuwa hovyo kupita maelezo.

Mpango umekuwepo kwa muda mrefu wa kuifanyia marekebisho barabara ile iliwemo kuipanua ili ikidhi mahitaji.Hilo limeana kutekelezwa na mamlaka husika.

Hata hivyo, upo udhaifu mkubwa wa mamlaka husika pamoja na mkandarasi aliyepewa kazi ya kuishughulikia barabara husika.Miezi miwli na nusu iliyopita walikwangua sehemu ya juu ya lami kuanzia eneo la SONGAS Ubungo mpaka External mabibo.Lengo ilikuwa ni kuondoa lami iliyochoka na kuweka layer mpya ya lami na kupunguza gharama za kuondoa na kuleta kifusi kingine.Tatizo ni kwamba kwa muda wote huo wa miezi miwili hakuna lolote lililofanyika kwenye barabara hiyo hivyo watumiaji tunapata shida sana kupita kwenye barabara yenye migongomigongo iliyotokana na kukwangua lami.

Haiingii akilini kuona mhandisi wa manispaa, jiji na mhandisi mkuu wa kampuni husika wanasimamia zoezi kama hilo la kukwangua barabara na kuiacha kwa muda wote bila kuikarabati.Je, ilikuwepo haja gani kukwangua wakati hawajawa tayari kuweka lami mpya?Mbaya zaidi kwasasa, wiki iliyopita wamekata na kuchimbua sehemu hiyohiyo ya barabara kwa lengo la kuziba mashimo kwa kifusi kabla ya kuweka lami mpya.

Kwa kweli barabara hiyo sasa imekuwa mashimo marefu na hatari kwa magari na migongomigongo ni mingi.Kwa wanaoendesha inakuwa vigumu kukwepa shimo na migongo kwa kuwa ni vigumu sana.

Staili hii ya ujenzi na ukarabati wa barabara zetu haijaanza leo.Niliwahi kuandika kuhusu Uhuru road eneo la Buguruni.Malalamiko no mengi kuhusu barabara zetu lakini inavyoonekana hatuna watendaji makini.

Ipo haja ya kuwawajibisha na iliwezekana uwekwe mkakati wa kuandaa orodha ya maeneo yanayojidhihirisha yenyewe kuwa nawatendaji wabovu.
 
Back
Top Bottom