Hivi karibuni tumeshuhudia jinsi wananchi wa Rungwe Mbeya wanavyotaabika kuvuka mto kwa kamba, akina mama wakiwa na mizigo yao huvuka mto huo kwa kuning'inia kwenye kamba mithili ya nyani au mwanajeshi anayevuka vikwazo kipindi cha vita, hali ile inahatarisha maisha ya wananchi na wakazi wale, lakini ni hivi karibuni tumeshuhudia rais akiwa anaahidi kujenga barabara ya kwenda kanisani kwa mzee wa upako.
Kati ya daraja lile na barabara ya kwenda kwa mzee wa upako ni kipi kilihitaji pesa ya haraka kwa ajili ya kujengwa?
Kwanini Rais hakuelekeza pesa hizo katika uje wa daraja lile ili kuokoa wale akina mama wanaoning'inia kwenye kamba kama nyani.
Rasimali za taifa zigawanywe sawa Tanzania sio Dar es Salaam tu.