Barabara ya Kilwa vipi ??

siame jg

New Member
Apr 21, 2009
4
0
Jamani Hawa Ma-Engineer wetu vipi ???? Mifereji ya kupitisha maji imejengwa hovyo kwa kiwango ambacho hata mtoto mdogo hakubali, Sio muda mrefu barabara itabomoka kwa mvua.
Jee ni kweli mifereji inatengenezwa na Wa-Tanzania ( Tanroads) na sio KAJIMA ?????
Jee hawa Engineers wetu wanajifanya hawaoni au wamekula kitu kidogo ????
Ubora wa barabara nao Unatia shaka, Hata kama ni Msaada TANROAD wawe makini kufuatilia ubora, baada ya muda mfupi gharama za matengenezo zitarudi kwetu.
MIFEREJI Imebomoka hata miezi 2 bado.
 
Barabara hii itakufa kabisa katika muda wa mwaka mmoja ujao.Sasa hivi barabara hii tayari imevimba kuashiria kuwa misingi yake imeathirika vibaya.
Kwa vyovyote vile kazi iliyofanywa katika barabara hii haiwezi kuwa imetekelezwa katika utaalam unaohitajika .
Hebu linganisha na barabara zilizojengwa na Konoike zaidi ya miaka 10 iliyopita(Morogoro Rd, Ally Hassan Mwinyi n.k.)
Wadau tusiposhituka sasa ndo tumeliwa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom