Barabara ya Kilwa bomu!

Barabara haijamalizika kujengwa wala haijakabidhiwa rasmi kwa wahusika mshaanza kuiponda, hebu kuweni na subra kidogo, akaa.

Na mimi naunga mkono hawa jamaa bado hawajakabidhi rasmi hii barabara, wanachofanya sasa ni kuwa wanaangalia mapungufu na kuyarekebisha kuweza kupata barabara iliyo bora lakini wananchi kwa vile wameruhusiwa kuitumia barabara ile wanafikiri tayari imemalizika. Kuweni na Subira.
 
tatizo lililopo ni siasa za ujingaujinga tu, kila mtu alimkubali John Pombe Magufuli alivyofanya kazi kwenye sector ya barabara, lakini kwa kuogopa asiwe rais kwa sababu ajaandaliwa au hayupo kwenye ukoo huo wa kiraisi, JK akaamua kumtupatupa tu, ili asionekane umuhimu wake, ukweli ni kwamba hata kama ni msaada, uwezi kukubali msaada wa ujinga ujinga tu, hakuna kiongozi ambaye yuko commited kwenye mambo ya barabara kama alivyokuwa JP Magufuli, na alikataa kufungua miradi mingi tu ambayo ilikuwa substandard,
NCHI HII SASA HAINA MWENYEWE NA UTASHANGAA RAISI WA NCHI ANAENDA KUIFUNGUA HII BARABARA AKIWA PAMOJA NA WAZIRI WA MIUNDO MBINU NA WASHAURI WENGINE WA RAISI, NI AIBU

Support Mkuu!!
 
Barabara haijamalizika kujengwa wala haijakabidhiwa rasmi kwa wahusika mshaanza kuiponda, hebu kuweni na subra kidogo, akaa.

Mkuu heshma...ila kibovu ni kibovu tu hata kama hakijakabidhiwa. Hivi ukiona jengo linalojengwa huku likikaribia kubomoka utakaa kimya hadi likabidhiwe? Ukiona kitu sio kizuri sema uwezapo (ila kwa kuzingatia ukweli uuonavyo wewe)......ni kweli ujenzi wa Kilwa road unatia mashaka sana. Ile lami imeanza kufeli mapema mno (angalia kwenye makutano na speed humps).

Hatupaswi kupuuzia mashaka walionayo watumiaji wa barabara kwa sababu tu eti sio wataalamu. Ni kweli wataalamu wanaweza kutupa tathmini nzuri zaidi, lakini hili halina maana tusio na utaalamu huo hatuwezi kujua kitu kizuri!

Well put.
 
Waswahili wana msemo, ''Hadia japo ya kokwa la tende ni hadia'', sasa nyinyi mnapiga kelele kwa kibara-bara cha hadia? si mtowe pesa zenu za madafu halafu mjenge yenu, muisimamie mnavyopenda? Khaa, nawashangaa, mnasaidiwa halafu mnajitia wajanja, si mngejenga yenu? mnachonga kwa cha kuomba? mngekuwa mnataka class A road mngeijenga wenyewe. Tembeeni duniani muone, hata hapo Japan waliotusaidia haka ka barabara wana classes kwenye bara bara zao, tusitegemee barabara iliyo bora kwa kuomba-omba. Tumeomba, tunachopewa turidhike, kama hatukitaki tusiombe tena. Kuchonga tuwache.

......duuuhh.........sijui hata kama wee jamaa unaelewa unachoandika......hii hapo juu ni argument ya mwaka 2009...........naanza kukubali kauli ya Nyani...........NDIVYO TULIVYO!!!
 
Utaelewa tu, kwani ukweli unauma!
 
Waswahili wana msemo, ''Hadia japo ya kokwa la tende ni hadia'', sasa nyinyi mnapiga kelele kwa kibara-bara cha hadia? si mtowe pesa zenu za madafu halafu mjenge yenu, muisimamie mnavyopenda? Khaa, nawashangaa, mnasaidiwa halafu mnajitia wajanja, si mngejenga yenu? mnachonga kwa cha kuomba? mngekuwa mnataka class A road mngeijenga wenyewe. Tembeeni duniani muone, hata hapo Japan waliotusaidia haka ka barabara wana classes kwenye bara bara zao, tusitegemee barabara iliyo bora kwa kuomba-omba. Tumeomba, tunachopewa turidhike, kama hatukitaki tusiombe tena. Kuchonga tuwache.

Kwa hiyo unataka kusema hii barabara ni sadaka na kama ni sadaka basi haipaswi kuwa bora? Mbona huwa tunasikia kuwa sadaka unatoa kilicho bora? Kama tutaendelea kusaidiwa kwa mabomu ili tusiseme kama kitu ni bora au la ni afadhali tusisaidiwe kabisa!
 
Na mimi naunga mkono hawa jamaa bado hawajakabidhi rasmi hii barabara, wanachofanya sasa ni kuwa wanaangalia mapungufu na kuyarekebisha kuweza kupata barabara iliyo bora lakini wananchi kwa vile wameruhusiwa kuitumia barabara ile wanafikiri tayari imemalizika. Kuweni na Subira.

Mkuu Elusive barabara ambayo tayari imetiwa lami na ina mabonde yanayokatisha tamaa, unangoja ukabidhiwe ndo ujue kuwa ni mbovu?
Huko ni kutoutendea ukweli haki , kitu kibovu kunaonekana mapema , barabara ya Kilwa bomu!
 
Mimi siyo kama nawatetea hawa KAJIMA, lakini nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa kampuni ya mwanzo ya KiJapan kutujengea barabara, kama mnakumbuka walijenga kipande cha barabara pamoja na daraja la Selander na kipande cha barabara iliyokuwa korofi enzi zile za MECCO cha Jangwani na walifanya kazi nzuri sasa sielewi kama KAJIMA ya sasa ndiyo ile ya zamani au vipi.
 
This is a very good contribution,barabara yenye unene wa lami ya 50mm,wasimamizi wako wapi? Watanzania tusiliwe wakati tunaona wenyewe.Drainage hii mimi sijawahi kuona pengine kwa barabara za nje ya mji.
....Au ndio yale mambo yetu yaleee 10%%%%??!!
 
Kwa hiyo unataka kusema hii barabara ni sadaka na kama ni sadaka basi haipaswi kuwa bora? Mbona huwa tunasikia kuwa sadaka unatoa kilicho bora? Kama tutaendelea kusaidiwa kwa mabomu ili tusiseme kama kitu ni bora au la ni afadhali tusisaidiwe kabisa!

Yes, tukatae misaada ndio jibu, tuanze kujifanyia vitu wenyewe, thats the point.
 
Mimi siyo kama nawatetea hawa KAJIMA, lakini nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa kampuni ya mwanzo ya KiJapan kutujengea barabara, kama mnakumbuka walijenga kipande cha barabara pamoja na daraja la Selander na kipande cha barabara iliyokuwa korofi enzi zile za MECCO cha Jangwani na walifanya kazi nzuri sasa sielewi kama KAJIMA ya sasa ndiyo ile ya zamani au vipi.

Mkuu Elusive,Kajima ilikuwa zamani sio sasa.Walifanya kazi nzuri sana pale Salender Bridge na Jangwani.Sasa hivi they are a shadow of themseves.
Angalia vifaa vilivyopo pale Kilwa vingi ni vibovu na vya siku nyingi sana.Kazi inayofanyika pale si nzuri kabisa kama inavoonekana.
Argument yangu ni, kama barabara haijakabidhiwa tayari msingi wake una bonyea na lami inafuatilia kubonyea huko.
Ninavyofahamu marekebisho ya sehemu hizo utakuwa mgumu na kazi haitapendeza.
 
Hii nchi inabidi tuwekeze kwenye uongozi hasa tukiwaleta wachina waje kusimamia utendaji serikalini, baada ya kufungwa upande mmoja baadhi ya sehemu ya barabara ya Kilwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo ili kupisha marekebisho .

Hatimaye hizo sehemu zilikamilishwa na wajenzi lakini cha ajabu ndani ya wiki mbili tumeshuhudia contractor yule akiweka viraka katika sehemu zilezile alokamilisha ujenzi uliodumu karibu miezi 10, kaweka viraka kuanzia maeneo ya sabasaba hadi Mtoni Mtongani, mambo ya ajabu sana.

Sijui ni dharau au uwezo mdogo? hivi watu hawa si huko China tunasikia wanapigwa risasi?

Hii barabara itakua inakarabatiwa miaka yote?mbali na usumbufu tunaopata kwa ile style ya kufunga upande wa kutokea Mbagala na kuruhusu watokao Mjini.

Huyu Mkandalasi ni tatizo kubwa tunasubiri tuone reaction ya serikali kwa hili.
 
kuna siku alihojiwa akadai hajalipwa.
 
sasa cheki barabara inalalamikiwa toka 2009 hadi leo 2015,mvua ikinyesha pale mataa ya ilala karume huwa hapafai
 
Mimi siyo kama nawatetea hawa KAJIMA, lakini nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa kampuni ya mwanzo ya KiJapan kutujengea barabara, kama mnakumbuka walijenga kipande cha barabara pamoja na daraja la Selander na kipande cha barabara iliyokuwa korofi enzi zile za MECCO cha Jangwani na walifanya kazi nzuri sasa sielewi kama KAJIMA ya sasa ndiyo ile ya zamani au vipi.

kipande cha Mbagala vibaka wengi. waliiba sana vitu kama mifuko ya cement iliokuwa inasaidia ujenzi na hata kuzorotesha kiwango
 
Back
Top Bottom