jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,264
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesitisha mpango wa kugharamia ujenzi wa barabara ya Dar - Chalinze (itakayokuwa na njia sita yenye urefu kilometa 142) na badala yake imeamua kuwakaribisha wawekezaji kujenga, kuendesha na kukabidhi ( Build, Operate and Transfer (BOT) basis.)
Hapo awali mradi huo ulipangwa kufanyika kwa pesa za serikali lakini kutokana na gharama kubwa za mradi huo wameamua ufanywe na mwekezaji ambapo gharama hizo zitarudi kwa watumiaji wa barabara kwa kulipa tozo kama inavyofanyika kwa daraja la Mwalimu Nyerere(Kigamboni bridge).
Katibu mkuu Mhandisi Joseph Kamhanga amesema kuwa mradi huo haujasitishwa wala kusahauliwa ila kwa sababu ya ukubwa wake serikali Inahitaji muda wa kuweka kila kitu sawa.
Barabara hiyo itaanzia Bandari ya Dar kupitia Mbagala kuelekea Pugu, Kisarawe, Kibaha na kufika Chalinze. Nyamhanga alisema pia mradi huo utakamilika katika kipindi cha miaka minne.
The Guardian 7th January 2017