Swash Bizo
Senior Member
- Jan 29, 2011
- 141
- 93
Wakazi wa maeneo inapopita hii barabara kila mwaka kipindi cha mvua wanateseka sana na usafiri. Barabara ina mashimo mengi na makubwa yamejaa maji ya mvua yaliyotuama. Tunaamini Halmashauri ya Ilala/TARURA watasikia kilio cha wapiga kura wa jimbo la Ukonga na kuwarekebishia hii barabara katika hadhi ya lami. Nawasilisha.
Updates.....
TAARIFA KWA WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA
Mbunge wa Jimbo la Ukonga na Naibu Waziri OR Tamisemi Mhe *Mwita Waitara* atafanya ziara Jimboni siku ya Jumamosi tar 25/05/2019 kuanzia saa 3 asubuhi kwa ratiba ifuatayo
Saa 3:00 asubuhi atakuwa kata ya Kivule mtaa wa Kelezange eneo la Matembele 2 ambapo atashuhudia makabidhiano ya barabara ya Kitunda - Kivule - Msongola kwa mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami.
Saa 6 mchana atakuwa Kata ya Msongola mtaa wa Yangeyange
Saa 7 mchana atakuwa Kata ya Pugu kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji ya DAWASCO.
Saa 9 jioni atakuwa Kata ya Buyuni mtaa wa Kigezi chini kuzungumza na wakazi wa kata ya Buyuni juu ya mradi wa umeme wa REA na changamoto zinazowakuta wananchi hao.
Saa 10:30 jioni atatembelea Barabara ya Majohe Viwege kujionea Hali halisi ya barabara hiyo ilivyoaribikia na mvua.
Katika ziara hiyo, Mhe. Waitara atafuatana na wakuu wa Idara za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, TARURA, TANESCO pamoja na DAWASCO.
WANANCHI wa maeneo hayo pamoja na ya jirani mnaombwa kujitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ukonga
24/05/2019