Barabara ya Bagamoyo kutoka Morocco - Mwenge yaanza kutumika, foleni sasa kupungua

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,771
7,138
Ni siku ya pili sasa wasafiri wa sehemu mbalimbali jino jeupe baada ya kuondokana na hasira za foleni ya Mwenge - Morocco ambapo awali sehemu ya kutumia dakika tatu tulikuwa tunatumia masaa mawili.

Kwa ubunifu wa Rais Magufuli wa kuchukua maamuzi sahihi ya kuondoa ushangiliaji siku ya Uhuru na fedha zikatumika kurekebisha uchumi, kwa hili hongera sana wabeja.

Tulikuwa tunatumia lita tatu ambazo kwa wakati ule wa Kikwete kabla ya kupunguza mafuta sawa na tshs 7500kwa kipande kidogo .

Sasa hivi hata ukiamua kutembelea Bagamoyo hakuna haja ya kufunga barabara upite.

View attachment 330672

Leo mnamo saa tano hivi nimepita barabara hii inayoendelea kujengwa , Barabara ya Bagamoyo kati ya Mwenge na Morroco.

Hali ilikuwa shwari sana kama picha invoonyesha.

Nlikuwa naikwepa barabara hii mida yote maana wakati wowote ilikuwa msongamano wa magari.

Zoezi hili likienda barabara zote kubwa za jiji, kweli foleni Dar itakuwa historia.
Hongera John Pombe Magufuli, kazi nzuri!!
 
Imeanza na mkosi au sijui tuseme ni kafara...jana kafa dereva wa boda na abiria wake kwenye hiyo bara bara mpya...
 
Ni siku ya pili sasa wasafiri wa sehemu mbalimbali jino jeupe baada ya kuondokana na hasira za foleni ya Mwenge - Morocco ambapo awali sehemu ya kutumia dakika tatu tulikuwa tunatumia masaa mawili.

Kwa ubunifu wa Rais Magufuli wa kuchukua maamuzi sahihi ya kuondoa ushangiliaji siku ya Uhuru na fedha zikatumika kurekebisha uchumi, kwa hili hongera sana wabeja.

Tulikuwa tunatumia lita tatu ambazo kwa wakati ule wa Kikwete kabla ya kupunguza mafuta sawa na tshs 7500kwa kipande kidogo .

Sasa hivi hata ukiamua kutembelea Bagamoyo hakuna haja ya kufunga barabara upite

Ukiwa njiani kwa mara nyingine turushie ka-image mkuu tuone
 
Kweli foleni imepungua sana ,nafikiri wakiimaliza yote mambo yatakuwa poa zaidi
 
Nomepita jana ila kwa daladala, naona kama haina kiwango hiyo barabara, kuna maeneo washaanza kuweka patches kwenye barabara!
 
asubuhi bado kuna foleni sasa sijui ni trafiki ama vipi mbona yale matofali yao kuna sehemu bado yapo hivi ishaanza kutumika rasmi ... mh ngoja leo nikiwa natoka jion niiangalie maana..... foleni inakera sana
 
Nikitaka kuona barabara za juu na maghorofa sina haja ya kuja Dar; Naingia mtandaoni naangalia clips za New York, Dubai nk
Ndo kwenu huko? usiwe mtumwa wewe! penda cha kwako. ndio nyie mnaokuwa na wapenzi then unatamani wa mwenzio. pendezesha chako ili ikipende zaidi. tunaitengeneza Tz mpya ili tuzidi kuipenda sawa sawa?
 
Ndo kwenu huko? usiwe mtumwa wewe! penda cha kwako. ndio nyie mnaokuwa na wapenzi then unatamani wa mwenzio. pendezesha chako ili ikipende zaidi. tunaitengeneza Tz mpya ili tuzidi kuipenda sawa sawa?
Ikipatikana hiyo Tanzania mpya, nijulishe nianze kuipenda.
 
Back
Top Bottom