Barabara mkoa wa Katavi katika hali mbaya

Barabara mkoa wa Katavi katika hali mbaya

Leo Asubuhi

Member
Joined
Apr 5, 2017
Posts
64
Reaction score
43
Mpaka mwaka huu 2018 mkoa pekee usiounganishwa kwa Lami ni Katavi, kwa kumbukumbu za haraka haraka nafikiri Mkoa huu ndiyo wa Mwisho katika nyanja za miundombinu.

Mawasiliano ya barabara kutoka Mpanda/Katavi kwenda Tabora ambapo ni takribani Km 360 inakubidi usafiri siku mbili ulale njiani, barabara ni chafu zimekatika na hakuna kipande chochote cha Lami kwa barabara hiyo.

Halikadhalika kutoka Mpanda/Katavi kwenda Kigoma ni Vumbi/tope japokuwa njia hiyo ina nafuu kidogo.

Ndani ya Mkoa/Wilaya zake ni vumbi lami katikati ya mji haizidi km 25 ni ile ya kutoa vumbi.

Niombeeni nimalize mishe nirudi salama mjini.
 
Si tuliona yule wa Ujenzi akizindua ujenzi wa barabara ya Katavi - Tabora; je ile ya Rukwa - Katavi haijakamilika?
Viwanda 100 kila mkoa vitatimia kweli!
 
Si tuliona yule wa Ujenzi akizindua ujenzi wa barabara ya Katavi - Tabora; je ile ya Rukwa - Katavi haijakamilika?
Viwanda 100 kila mkoa vitatimia kweli!
Nimepita juzi barabara ya Tabora-Katavi ni tope , naona ndo hii hii iliyozinduliwa
 
Mh. Mizengo Pinda baada ya kustaafu aliweka wapi makazi yake ya kudumu?

IMG_7919.JPG


Nimeambiwa hapa ndipo nyumbani kwake hapa mitaa ya Makanyagio
IMG_7919.JPG
 
Back
Top Bottom