Paragumu
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 326
- 142
Nikiwa kama mdau wa maendeleo ninaezunguka maeneo mbali mbali nchini naomba mamlaka zinazohusika zifanyie kazi hiyo Barabara inayounganisha Kijiji cha Usinge kilichopo Wilayani Kaliua na Barabara kuu inayotoka Tabora kuelekea Kigoma katika center inayoitwa Kibaoni maarufu kama njia panda ya Ugansa.
Kwakweli imeoza wenyeji wanasema kipande hicho chenye urefu usiozidi kilomita 5 haijafanyiwa marekebisho yapata miaka 2,mbaya zaidi katika kipindi hiki cha mvua ndio imekuwa balaa zaidi madaraja hakuna,mashimo kibao wananchi wanaumia.
Mbaya zaidi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaliua pamoja na Mkuu wa Wilaya wanafika katika kijiji hicho kila wakati kuhimiza shughuli za maendeleo na ulipaji wa mapato ya Serikali sasa swali langu kwenu viongozi wa Wilaya hiyo barabara hamjaiona au kiburi mnataka siku moja mje mchambwe kama alivyochambwa mwenzenu Waziri Kamwele pale Kiyegeya na mjomba Magu sio! Mbunge ndio hovyo kabisa hata haonekani kutetea hilo.
Hao TARURA sijui ndio wameacha kazi maana nadhani hicho kipande kinawahusu lakini hata pua zao hazionekani Usinge.
Baba Magu pita na Meneja wa TARURA wa Kaliua maana ulishatoa maelekezo lakini hawakuelewi. Kwa taarifa yake meneja wa TARURA hicho kipande kitakatika muda sio mrefu na huenda mawasiliano na kijiji hicho cha Usinge kutokea kibaoni yasiwepo.
Ni hayo tu, nikiripoti kutoka Masankuroni ni mimi msangatonge PARAGUMU wa wananchi.
Sent using Jamii Forums mobile app