Banza Stone: Mwalimu wa walimu

Banza Stone: Mwalimu wa walimu

makaveli10

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
37,429
Reaction score
108,441
Nasikiliza ngoma zake kadhaa hapa, nimekumbuka miaka kadhaa nyuma, huyu jamaa alikuwa fundi mnoo, tungo zake bora kabisa, anaimba, anapiga vifaa(ngoma) na ku-rap juu.

Kwangu mimi alikuwa ni mwanamziki bora katika aina ya muziki aliokuwa anafanya kwangu mimi alikuwa bora zaidi ya wale wenzie mafahari wawili (Muumin na Ali Choki)

Kazi aliyoifanya akiwa Twanga Pepeta kisha kule kwa marehemu captain komba ni kubwa mnoo, tungo zake zilikuwa matata saana, rap zake zilikuwa murua mnoo.

Duniani wanadamu tunakosea na kufanya mazuri pia, Mola ndio anajua wapi tunastahili, mimi siwezi kumuhukumu, namuombea Mola amsamehe pale alipokosea amfanyie tahfifu huko.

Amuweke mahala pema.
 
Mwana masanja nilipoanzaa Ee Mwana masanja nilipoanza watu wote matumbo joto, teacher wa maticha nilipoanza Ee ticha wa maticha nilipoanza watu wote matumbo joto. Banza Stone nilipoanza ee.. Banza Stone nilipoanza watu wote matumbo jotoo...
 
Mwana masanja, sinza kwa wajanja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom