Banyani mbaya, kiatu chake dawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Banyani mbaya, kiatu chake dawa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lilombe, May 13, 2011.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF nimepitia katika kumbukumbu zangu nikagundua Wakili alitukuka Bw. Mabere Marando ni mmoja wa wapambanaji dhidi ya UFISADI na matumizi mabaya ya raslimali za nchi, sote twaelewa hivyo tangu akiwa NCCR Mageuzi hadi leo hii CDM. Hatahivyo yeye ni mmoja wa mawakili wanaomtetea Jeatu Patel katika kesi ya kukwapua pesa za watz kupitia akaunti ya EPA. Hapa ni CDM wapo mtegoni isije baadaye wakageuziwa kibao kuwa chama chao pia kimefaidika na mapesa ya ufisadi wa EPA.
  Kama tujuavyo 1 + 1 = 2 hivyo Jeatu Patel + Marando = Pesa za Ufisadi hivyo basi CDM hawatakwepa mtego huu wa kutumia mapesa ya UFISADI.

  Sasa ni wakati muafaka wa CDM kufikiri kwa kina nafasi ya Marando, sikuwashangaa kipindi cha karibu na uchaguzi kumkaribisha Marando kwa vile wakati ule mawazo yalikuwa ni kukusanya nguvu raslimali ili kuelekea IKULU.

  Kama CDM ni washabiki wa BANYANI MBAYA, KIATU CHAKE DAWA! Kaeni kimya vinginevyo CHUKUENI HATUA!
  :A S 103:
   
Loading...