Bans

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,091
Reaction score
136,650
Hivi ni mimi tu au? Siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la bans. Watu wanalimwa ban shoto kulia.

Na nyinyi mmeliona hilo?

Halafu kuna mods wawili ambao ni wachemkaji sana ila mmoja wao naona kidogo siku hizi amekuwa na afadhali kidogo lakini bado ni mchemfu.

Jambo jingine nimegundua kuna mods hawawezi kabisa kutetea maamuzi yao ya ama kutoa ban au kufuta mabandiko ya watu. Ukiwabana wanaishia kukufungia au kufutilia mbali kila uandikacho. Mnakera sana na hiyo tabia yenu.

Sasa huu uzi usipofungwa nitashangaa sana. Tusubiri tuone.....
 
NN wewe mchokozi sana, unataka uzi ufungwe tena?
 
Hao watakuwa washawahi kuwa waalimu au maafande maana ukiwa mwalimu au afande automatically utakuwa mnoko konomaaaaaa....
 
NN wewe mchokozi sana, unataka uzi ufungwe tena?

Mimi wala sio mchokozi kihivyo. Mara nyingi huwa nachokozwa. Na nikichokozwa it's on. We'll go rounds.

Sitaki uzi ufungwe ila nitashangaa usipofungwa maana hawa watawala na viranja wa JF huwa hawapendi kukosolewa (ingawa wao nahisi watakuwa na mtazamo tofauti).

Ila kwa vile nimeshasema kuwa nitashangaa kama uzi hautafungwa, sitashangaa pia wakiuacha uendelee ili kuonyesha tu nilikuwa na makosa katika kusadiki kwangu kuwa utafungwa.

Tusubiri tuone.
 
Ila kweli hata mimi nimegundua kuwa NN sio mchokozi kama nilivyokuwa nafikiria hapo zamani,.. Nnachojua ni kuwa ukichokozwa kesi yako huwa haimaliziki mapema...


Hilo la ban mie sina cha kuchangia manake nimewahi kulimwa mara 1 na ile kweli niliistahili so sikuona tatizo na ingenishangaza kama mods wasingenilima ile ban...

Uzi wako uko vizuri sioni kama una tatizo manake umesema kile kinachokukera, wakiuondoa ntaandamana kwaajili hiyo..
 
Hilo la ban mie sina cha kuchangia manake nimewahi kulimwa mara 1 na ile kweli niliistahili so sikuona tatizo na ingenishangaza kama mods wasingenilima ile ban...

Na wewe umewahi kuwekwa lupango? Lini ilikuwa? No way bana....it can't be. Yaani wewe na ban hata hamuendani kabisa.
 
Na wewe umewahi kuwekwa lupango? Lini ilikuwa? No way bana....it can't be. Yaani wewe na ban hata hamuendani kabisa.
Nimewahi asee, mwaka jana , miezi ya mwisho mwisho! Nilijichanganya jukwaa la siasa nkajifanya nimekunywa maji ya bendera... Nilikuwa mstari wa mbele natetea chama kwa zaidi ya masaa ma3, mwisho wa siku nikaambulia ban...
 
Mmmh, kama hatakuja mkaanga sumu muda si mrefu, sijui.

Naskia israel wa ban au unyakuo wa sredi akizunguka zunguka hapa.

Nawapa pole in advance.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…