Bank teller alivyotapeliwa

Teller yeyote akikupa hela ukaishika mkononi ukimrudishia kumwambia akupatie chenchi kama ilivyo lazima ahesabu upya. Huyo mzembe kama ni kweli
 
Nilisha tapeliwa namimi hivi hivi pale Isibania mpakani mwa tanzania na kenye wakati tunaingia Kenya. Badaa ya kumaliza taratibu zote za checkup pale boder upande wa tanzania kisha upande wa kenya.

Kwavile ilikua jpili sikufanikiwa ku change pesa mwaza, nikasema nitabadirishia mpakani. Wakati naingia upande wa Kenya nikadakwa na jamaa anadai ako na Mpesa na wana change pesa, nikaona ngoja ni change.

Nikamawambia anipe 6,800Ksh ambayo sawa na 150,000Tsh kwa rate tulio kubaliana. Akanihesabia akanipa nami nikampa za Tz. Nikaanza kuzihesabu nikakuta inapelea shilingi 100 nikamwambia akaniambia nihesabu tena nami nikahesabu tena kweli zikawa inapelea 100 akaziomba zile pesa nikampa kumbe ndo ikawa kosa.

Akazihesabu nayeye akakuta 100 inapelea akatoa pochi akatoa mia akaiongezea kwenye zile zingine akanipatia, mimi bila kuzihakiki tena nikaziweka mfukoni nikasepa. Nilipo fika kwenye office ya basi tunalo safiri amabapo tunasubiria muda ufike tuendelee na safari upande wa Kenya nakasema ngoja nihesabu zile pesa.

Sikuamini macho yangu, nikaji serch kila mfuko nakuta 3,000Ksh zinapelea kwenye zile pesa. Nikawashilikisha abiria wenzangu wakaniambia umesha ibiwa na ndo mchezo wao pale boder,nikajiona bonge la mjinga.

Kumbe nilipo mrudishia zile pesa akachomoa 3,000 kiaina, either alizidondosha chini au aliziminya mkono wa kushoto akaongeza 100 iliyo pelea akanirudishia.
 
anyway ni vizr kutupa matukio tofauti ili tuwe na experience na kudhibiti pale yanapo jitokeza
Wacha nikupe hii iliyotokea Tabora, benki sihitaji. Mdada naye teller kashapata mchongo wa shule ughaibuni alafu hela hakuna. Akajipanga akapata visa na tiketi kila kitu tayari. Karudi job kachungulia akaunti ya ghabachori moja kavuta mkwanja wa maana hiyo Jumamosi na safari J3. Hawa matajiri wengi walikuwa wanachukua statement zao kila mwisho wa mwezi, kwa sasa nadhani teknolojia imekua. Jumatatu binti haonekani kazini bila taarifa, simu haipatikani. Wanakuja kujua ukweli mwenzao ashaondoka. Sijui mwisho wake ilikuwaje.
 
Ila kwa Bank ni ngumu sana hili kutokea. Wale jamaa wanaweza hesabu hela hata mara 100 maana hasara inakuwaga upande wao
 
duh! Binti alijiongeza sema zitatumika fresh TU maana pesa haichagui mwenye dhambi Ina mtii kila mtu
 
duh! Binti alijiongeza sema zitatumika fresh TU maana pesa haichagui mwenye dhambi Ina mtii kila mtu
Madogo wameajiriwa branch ya Mtwara halafu wakakbidhiwa kuoperate ATM, Branch controller naye kawaamini asubuhi anaacha kubalance akaunti ya ATM. Madogo pesa zinazobaki jana yake wanaweka pembeni wanabalance akaunti alafu wanaweka hela zingine kwa siku husika. Baada ya miezi michache washanunua magari na mishahara miaka ile ilikuwa midogo lazima uchukue mkopo ndo ununue gari. Madogo gheto limesheheni mazaga kibao. Ikabidi tuitwe wazee wa fraud investigation miaka hiyo. Wangekuwa wajanja walikuwa hawana kesi na msala ungebaki kwa controller. Madogo tumewaweka sawa na ahadi kemkem wakaingia line. Msala ukawa wao na kazi ikaisha. Sijui wako wapi siku hizi.
 
Danga langu alipigwa kama ivyo kwenye mpesa yake na biashara yenyewe ikafia hapo
 
Iliwezekanaje wakati kuna mashine ya kuhesabia hela
 
Yani teller apewe pesa tena asithibitishe kama amount ipo sahihi? HAIWEZEKANI. Teller atasahau vyote lakini si kuhesabu pesa..Hiyo ni kanuni namba moja ya bank teller.

Story nzuri anyway
 
Labda kwa [emoji542] bank za enzi hizo sio za Sasa wanna mashine kabisa za kuhesab
 
Imeshamtokea mfanyakazi wa Mpesa, sema jamaa alizihesabu tena na kukuta zile Pesa zimepungua..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…