Bank M-Connecting the dots...

Kwa uchambuzi wako, Utawala wa sasa una uwezo gani wa kupambana na nguvu ya hao "mafisadi wa kimataifa"?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hauwezi hata kidogo! Kumbuka issues kama hizi ziliibuliwa humu Jf! Hata kashfa ya EPA na RICHMOND chanzo ni humu! Kwahiyo alipotokea rais aliyeuchukia mtandao huu pamoja na uhuru wa habari, nilipatwa man mshangao na kujiuliza nia yake haswa ni kitu gani? Sasa ndiyo nikafunduwa kuwa kumbe ni kwamba hawawezi, na hilo wasiporomoke kisiasa, dawa ni kuminya uhuru wa habari.
 
Ya kuminya uhuru wa habari siyo sahihi kwa kuwa unajua fika nguvu ya neno, hasa habari, (iwe ya ukweli, uongo au uzushi).

Kwa sababu hiyo hakuna uhuru usio na mipaka kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya JMT (1977), Ibara ya 29 na 30, Sheria za nchi, Kanuni na Taratibu husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye demokrasia ni hatua zinachukuliwa dhidi ya wanaofanya hivyo na siyo kuminya uhuru wa habari. Wananchi wanatakiwa wapate taarifa zote, nzuri na mbaya kuhusu viongozi wao! Wasitake kuonekana kama Miungu watu ama kama malaika!
Mfano wamarekani, ilitokea habari za Trump kuzungumza maneno machafu, kwamba anaweza kukamata sehemu za siri za mwanamke hao ambao huwa anakutana nao, muda wowote anaotaka na hakuna wa kumfanya kitu. Maneno yale ambapo alisikika akiongea wazi na kuonekana kwenye video, Kwasababu ya demokrasia, wananchi bado walimchagua! Ingekuwa huku kwanza watu wangepotezwa wengi!

Na siyo hayo tu, bali kufichaficha uhuru wa habari ili kwa kuminya uhuru wa habari, ndiyo matoke ya ufisadi kama huu kwenye thread hii kufichwa! Kule kwenye VODACOM ni mara tatu ya hii EPA! Achilia mbali escrow, bado sijui MEREMETA, Buzwagi, radar, 1.5 trillions, and counting!
 
Alituacha pabaya. Yeye kama mchungaji wa kondoo hukutakiwa kuondoka bila kuwa na uhakika wa nani wataendelea kuchunga kondoo (waTZ) wabaki salama dhidi ya mbwa mwitu ambao walikuwa wanasubiri kila kona kurarua kondoo. Moja ya kazi ya kiongozi ni kuandaa warithi. Wachina wameweza vizuri sana. Sasa wanatikisa dunia. Hakuandaa succession. Total failure! Ni bora angebaki kuandaa viongozi kuliko kususa!

Matokeo tumeendelea kuyumbayumba kwa miaka 30! Hakuna tena kitu kimoja kizima hivi, tunachoweza kukiweka kwenye taswira zetu, kama Taifa la Tanzania, kwa majivuno! Tumekwisha kujidharau kwa sababu ya viongozi wabovu. Tunajiita wabongo!!

Angalia Kagame anachofanya. Wenye mawazo yao watamwona dictator. Lakini si kweli? Anaisimamia nchi yake iende nbele. Wakati sisi tunazunguka zunguka, Rwanda inakwenda mbele na yaliyotokea hapa hayawezi kutokea Rwanda. Tunahitaji kutafakari, kuweka sera zenye mashiko, kuweka mikakati ya kuendeleza sera hizo huku tukijifunza!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepatwa na hasira sana. Inakuwaje sisi tunadhulumiwa kiasi hiki, tunaibiwa kiasi hiki, tunanyanyaswa na wahindi ktk maofisi yao kwa pesa walizopata kwa kutuibia sisi wenyewe wakishirikina na wezi weusi.

I say openly nimefikiria kama ningekuwa kiongozi mkubwa wa kimaamuzi serikalini na jinsi amabvyo ningewafanya hawa wahindi and their stooges.

This thread is fire in my heart's bush, burning all my veins mpaka nasema why nimeendelea kuisoma tena na leo. Huwa sipendagi kufatilia haya ma skendo koz najua effect yake on me...yaani nchi ina changamoto nyingi halafu wapumbavu fulani nao wanatuibia ibia kila siku

Najua viongozi wa vyama na serikali mnapita hapa please ktk kazi zenu do the needful...waTanzania wanaumia sana sana sana kuyona au kuysoma haya ilhali watu waliowaamini wafanye maamuzi kwa niaba yao wapo na wanawapeleka chaka.

Kwa hili la kukamata huyo Indians naomba Mh. Rais asiishie hapo, unapotaka kuua nyoka aima at its head naomba hiyo chain yote tuibobomoe regardless of political and social affiliations...

The zeal for this country is consuming me badly, yaani nina hasira sana, nina hasira sana sana ndiyo maana sipendagi kuyafatilia haya skandali


Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Wala usiwalaumu wahindi mkuu,kuna kitu kinaitwa ''BEHIND THE SCENE'' ukijua nyuma yao utatamani watu wasiojulikana walitakiwa wawe wameshafanya yao.Kuna miswahili ndiyo iliyokuwa inasuka mipango yote hiyo hawo wahindi walikuwa chambo tu.Kuwavalisha mazezeta T-SHETI na KOFIA nchi nzima na kuwagaia fedha na ubwabwa unafikiri shilingi ngapi??? AMKA
 

Wewe ungependa uandike uchafu gani dhidi ya mtu ili uthibitishe kuwa unayo haki na uhuru wa mawazo zaidi ya yale unayoyaandika?

Wangapi wamepotezwa kwa kuandika au kuwasema vibaya viongozi kwa matusi, mengine ya nguoni na/au kuwazushia tuhuma?

Tusijifanye vipofu au viziwi.

Ukweli unabaki kuwa watu wanapotezana au kijeruhiana kwa sababu za kibinafsi kabisa, ingawa imekuwa desturi ya upinzani kuhamishia hayo kwa Serikali. Sababu kuu ni kukosa hoja ya kisiasa yenye mshiko kitaifa.
 
Si unaona Sasa! Kumbe kuandika ufisadi wa Taifa ndo unasema ni “uchafu dhidi ya mtu”, so what? A nation is bigger than a single person.

Huwezi kusema wanapotezana wenyewe na wakati hata mkuu anavunja katiba kwa kuzuia siasa. Kauli za rais zinachukuliwa kwa uzito wote na vyombo vya usalama! Kuanzia wenye kufanya waziwazi kama inavyoonekana kwenye kesi za kubambikiwa, mpaka wale wa sirini AKA wasiojulikana! Na hata vyombo vya habari ni the same! Mkuu wa mkoa alivamia studio za clouds TV na kaonekana kwenye cctv.

Eti sababu kuu ni kukosa hoja ya kisiasa! Ufisadi nyie, uuwaji nyie, utekaji nyie! Si laana ya nchi ni nini?
 
Buku7 uzi huu wanauchungulia kama mijusi

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣hawatii mguu humu! Wenyewe wanataka propaganda nyepesi nyepesi tu! Wanapigia kelele mishahara ya kina Lissu na Nasari. Na huku wenyewe ndiyo walafi waliyoifukarisha nchii hii. CCM imepoteza legitimacy ya kuliongoza Taifa!
 
🤣🤣🤣hawatii mguu humu! Wenyewe wanataka propaganda nyepesi nyepesi tu! Wanapigia kelele mishahara ya kina Lissu na Nasari. Na huku wenyewe ndiyo walafi waliyoifukarisha nchii hii. CCM imepoteza legitimacy ya kuliongoza Taifa!
Mabilion yamepigwa mpk aibu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa halafu imagine, hasira zote hizo, ndiyo unaambiwa unyamaze lasivyo wewe ni msaliti wa Taifa! ccm ni lazima imewaroga watanzania Labda kuna mitambiko hatari siyo bure! Wengi wanaoisapoti pengine hawajui kwasababu ya kuminywa kwa uhuru wa habari nk.
 
Tujaribu kukumbushia tu tulikotoka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…