Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 18,633
- 20,975
Kama si lowassa // RAIS angelikuwa membe as for their planed,tungedumaa kwa miaka 10 tena huku R1,akiendelea kukuimu urais.
hebu wataalam wa uchumi wanifahamishe
uchumi wa nchi je unakuzwa kwa kubana matumizi ama kwa kufungua mianya mingi ya kuingiza pato ikiwemo pato la kigeni?
kwa mfano:
nyumbani wazazi huwa wanatumia hela kwa uangalifu huku wakiwa wanatafuta mbinu mbadala za kukuza kipato manake with time matumizi na gharama za maisha huwa zinapanda.
je katika uchumi wa taifa hili limekaaje?
LAzima uanzie apo pa kubana matumizi na nidhamu...then ayo mengine yatakuja yenyewe...btw pole yako
Mimi na Lowassa picha hazipandi. Sijawahi na wala sitawahi kumuunga mkono Lowassa katika harakati zake za kisiasa. Lakini, kwakuwa mimi ni muumini wa ukweli daima, namsifu Lowassa kwa kumchora Rais wa Tanzania ambaye kiukweli sasa tumempata. Tumempata Rais aliyesemwa na kuchorwa na Lowassa. Ni Dr. John Pombe Magufuli. Wa awamu ya tano hapa Tanzania.
Ndugu Edward Ngoyai Lowassa, alipokuwa CCM, alikuwa ni mwanachama wa kwanza kutangaza nia ya kuwania Urais kupitia CCM. Alitangaza nia tarehe 30/5/2015 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Lowassa, wakati akitangaza nia, alimchora Rais atakiwaye Tanzania kama ni Rais mwenye uthubutu, imara, mwenye kutoa jambo likatekelezwa na kadhalika. Rais kweli kweli.
Lowassa, hata kwenye kampeni zake akiwa CHADEMA, kuanzia mwanzo hadi mwisho, alikuwa akihubiri mabadiliko ya kimfumo na kisera. Nasema kwa kujiamini kuwa ni Lowassa ndiye mwanzilishi wa Rais tuliyempata na 'mhubiri' wa sera ya mabadiliko ya kimfumo na kisera. Ilifikia mahali, CCM kupitia kwa Dr. Magufuli wetu, tukakubali kuendana na hali halisi. 'Tukaiba' sera za CHADEMA na sisi kuanza kuhubiri mabadiliko. Tukaongeza kuwa mabadiliko ya 'kweli'. Ikalipa.
Mambo anayoyafanya Rais Magufuli ni mambo mazito. Yanabadili mfumo na sera. Mambo ya kukataza, kufuta, kubadili na kuanzisha mengine ni mambo yanayogusa moja kwa moja sera na mfumo uliokuwepo. Si mchoro wa Lowassa huu? Namsifu Rais Magufuli kwa 'kukopi na kupesti' mambo na kusonga mbele. Anakopi na kupesti kile wananchi walikuwa wakikisubiri na kutamani kwa muda mrefu.
Tumsifu mkimbiaji lakini tusisahau anayemkimbiza. Sifa tumpe Rais wetu kwa kufanya mambo mazuri na makubwa. Lakini, Lowassa ndiye aliyetuonesha kuwa yawezekana!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Naona CCM kwa CCM mmeanza kuparuana, teh teh tehe!Wewe mnafiki si ulisema mabadiliko hayawezi kutokea ndani ya CCM? Leo unarudi kinyumenyume....inaonekana kile kidawati chako cha pale ufipa kimeanza kukuchosha
Una majanga gani mkuu naona unapewa pole!pole yangu kwa nini??
Mabadiliko ya kweli yanaletwa na CCM. Uroho na tamaa ya madaraka vimemponza Lowasa. Aende zake. Magufuli anasifika kwa utendaji wake kila alipokuwa. Huyo Lowasa ni bla blaa tu. CCM haikukosea kumsimamisha Magufuli
Naona CCM kwa CCM mmeanza kuparuana, teh teh tehe!
MZEE TUPATUPA wa Lumumba ni mwana CCM kindakindaki, wewe maamuna wa juzi tu huwezi kumkaribia hata robo kiukada, ila mara nyingi huwa anaponzwa na tabia yake ya kusema ukweli.