gambosh1972
Senior Member
- Oct 30, 2013
- 119
- 22
Jamani ni aibu sana hata sijui niseme nini kuiona taifa la kesho likiangamia na madawa ya kulevya aina ya bangi na hata kile kifaa cha bakhresa(sembe) masaa 24 na wala hawabugudhiwi na chombo chochote cha usalama kwa raia.Nashindwa kuelewa mfano polisi wanashindwa vipi kuyatawanya haya makundi ktk eneo nzima la msamvu na hata Itigi nyuma ya Lupira?bangi zinasokotwa hadharani na watu wako hoi kwa kupinda udenda nje nje na ukabaji uliyokithiri nyakati za usiku.Jamani polisi wetu waokoeni hawa vijana na hata raia wanaokabwa na kuporwa vitu na hata kuumizwa.