Bange si chakula

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,265
4,729
*Story ya Mabangi..*
```Baba kutoka Mashambani alipata Safari ya kwenda Mombasa kwa Biashara. Baada ya Wiki moja, akampigia Simu Mtoto wake Mabangi kujulia hali ya Nyumbani.```

*Baba:* Alooo! Vipi hali zenu huko?
*Mtoto:* Tuko poa Baba, kila kitu sawa isipokua kidogo tu kulitokea Shida..
*Baba:* Shida gani
*Mtoto:* Waujua ule ufagio wenye gongo refu? Basi lile gongo lake lilivunjika.
*Baba:* Aaaah umenishtua, si neno tutanunua mwengine. Lakini Ni nani alovunja?
*Mtoto:* Ni ngombe wetu aliuangukia.
*Baba:* Ngombe!?
*Mtoto:* Naam alikua anakimbia kwa khofu maana zizi lilikua limeshika moto?
*Baba:* Ah moto! Lakini ngombe yuko salama?
*Mtoto:* hapana baba ngombe alikufa
*Baba:* Lahaulaaaa..... na ilikuaje zizi likashika moto?!
*Mtoto:* Kwa hakika moto ulianza kwa nyumba yetu ukaenea mpaka ukafika zizini.
*Baba:* Nyumba yetu imeshika moto!
*Mtoto:* Naam Baba wajua yote ni huyu ndugu yangu *Ally,* Mungu amrehemu..
*Baba:* Mungu amrehemu?! Kwani Mwanangu Ally, amekufa?
*Mtoto:*ndio Baba, Ally amekufa. Wajua alikua akivuta Sigara Chumbani kwake Sigara ikaanguka kwa Godoro na yeye amelala. Moto ukawaka Nyumba nzima.
*Baba:* Wanambia Ally siku hizi avuta Sigara! Alianza lini mambo hayo?
*Mtoto:* Alianza wiki hii tu kwa sababu ya Stress na huzuni nyingi.
*Baba:* Alikua na huzuni za nini?
*Mtoto:* kutoka Mama afe, Ally amekua na huzuni kubwa sana, hali wa halali.
*Baba:* Mtumeeeee, Mamako pia amekufa!
*Mtoto:* Ndio Baba, lakini usijitie Stress Baba kama ni Ufagio, Wallahi nakuhakikishia tutapata tu mwengine...

*BANGI si Mboga *

Akili Zangu bhana...mniache tu
*©*
 
Back
Top Bottom