Bandari ya Chato kukamilika mwezi Agosti mwaka huu

Area 56

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,555
Reaction score
4,085
BANDARI ya Nyamirembe, Wilaya ya Chato mkoani Geita, inatarajiwa kukamilika Agosti 23, mwaka huu.

Mradi wa ujenzi huo uliogharimu Sh bilioni 4.1 ambazo ni fedha za serikali, unajengwa na Mkandarasi wa ndani ambaye ni Kampuni ya VJ Mistry, kutoka Bukoba mkoani Kagera.

Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina, akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo jana, alisema mradi huo unaendelea na uko katika hatua ya asilimia 40 utekelezaji.

Alisema sehemu ya kazi iliyobakia ni kumalizia ujenzi wa gati, jingo la abiria, jingo la mizigo, chumba cha mashine ya umeme, vyoo na chumba cha walinzi.

“Katika gati hili, meli ziliacha kuja miaka minane iliyopita kwa sababu kampuni iliyokuwa inaleta meli hizo kusitisha kwa sababu zao wenyewe lakini Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wameurudisha mradi huu,” alisema.

Msina alisema bandari hiyo itakapoanza kazi itachochea biashara kati ya nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na nchi jirani. Naye mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo, Injinia Anderson Mbogowe alisema hadi jana mradi huo umefikia asilimia 47.

Hakika maendeleo hayana vyama.
20190610_144806.jpeg
 
Kuna msitu wa Chato nao upo kwenye mchakato wa kutangazwa kuwa National Park, tunaangalia tu namna ya kuongeza idadi ya wanyama waliopo. Chato itakuwa kitovu cha biashara na utalii very soon
 
Imekuwaje hiyo bandari ya Chato imetangazwa? Maana sasa hivi inaonekana kama miradi ya huko haitakiwi kutangazwa kwani huenda inajengwa bila sifa stahiki na iwapo itafahamika viashiria vya upendeleo wa wazi vitafahamika.
 
Hivi kipau mbele cha ujenzi wa hiyo bandari ni kipi maana hapo tayari kuna bandari ya mwanza na ya bukoba
BANDARI ya Nyamirembe, Wilaya ya Chato mkoani Geita, inatarajiwa kukamilika Agosti 23, mwaka huu.

Mradi wa ujenzi huo uliogharimu Sh bilioni 4.1 ambazo ni fedha za serikali, unajengwa na Mkandarasi wa ndani ambaye ni Kampuni ya VJ Mistry, kutoka Bukoba mkoani Kagera.

Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina, akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo jana, alisema mradi huo unaendelea na uko katika hatua ya asilimia 40 utekelezaji.
Alisema sehemu ya kazi iliyobakia ni kumalizia ujenzi wa gati, jingo la abiria, jingo la mizigo, chumba cha mashine ya umeme, vyoo na chumba cha walinzi.

“Katika gati hili, meli ziliacha kuja miaka minane iliyopita kwa sababu kampuni iliyokuwa inaleta meli hizo kusitisha kwa sababu zao wenyewe lakini Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wameurudisha mradi huu,” alisema.

Msina alisema bandari hiyo itakapoanza kazi itachochea biashara kati ya nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na nchi jirani. Naye mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo, Injinia Anderson Mbogowe alisema hadi jana mradi huo umefikia asilimia 47.

Hakika maendeleo hayana vyama.View attachment 1123728
 
Back
Top Bottom