Bandari na kituko cha taifa

Nimesikiliza Clip ya Waziri Mkuu inayo trend, naye amejikita kutetea Mwekezaji, lakini anasahau Watu wanahoji aina ya Mkataba.
 
Reactions: Ame
Duh! Mi kila siku nafikiria walivyotuaga kwamba wanaenda kwenye maonyesho ya biashara na walivyorudi hawakutwambia kwamba tayari wameshauza bandari zote.

Mara paaaa.. Nikaona jengo refu Dubai lina picha ya mama nikajua tayari Dubai wameshangilia goli hata kama hatujaona mechi yenyewe.
 
UVIVU. Sawa kabisa!
 
Binafsi nataka Rais ajiuzulu au aondolewe kwa kura, hafai

 
Mi nitawaelewa tu siku mkiunganisha kelele hizi na yale yanayotokea migodini kwa wawekezaji wazungu........wanaenda kutua huko na ndege zao (hatujui katu zinabeba nini zinapokuja ikizingatiwa kuwa wao huko makwao wana makampuni kabisa ya kutengeneza silaha (biashara yenye faida kuliko zote navyosikia)) na ndege zao zinaondokea hukohuko baada ya kubeba mzigo (km ni madini pekee au kuna vingine, ni wao na wapinga mkataba wa bandari kina tibaijuka na Dr slaa ndo wanajua).

Kama hiyo haitoshi, mchanga wenye madini unabebwa na kupelekwa huko kwa wazungu kuchambuliwa kisha ndo wanatuambia kuwa katika mchanga uliojaa katika contena fulani, tumepata grams 2. Najua, taarifa hiyo hupokelewa na maneno, 'Praise the Lord!' na kina Dr slaa na kadinali Pengo huku kina prof Tibaijuka na takataka zingine humu huitikia kwa shangwe, ''Aamin!" na makofi juu.

Kama vp tuanze upya kwa kila kitu, lkn biasness kwa misingi ya kiitikadi tu haki ya nani tutakwama. Yakiisha maandamano yenu ya kupinga uwekezaji wa bandari, yatafuata maandamano mengine ya kupinga mikataba ya hovyo ya madini na gesi.....we subiri tu utaona!
 
Uongozi wa awamu hii na ule wa awamu ya 4 ni mapacha
Nakazia.
Hata staili ya uongozi wa Mama nadhani itakuwa ni ushauri 100% kutoka kwa JK mfano sasa hv kaja na ile ya kuweka pamba masikioni asisikie kelele za wananchi...JK yeye alikuwa anajisemea ni upepo tu utapita!
Serikali imewekwa mfukoni na kikundi cha watu fulani, we umewahi kusikia wapi duniani eti safari ya Rais inafadhiliwa na watu binafsi, rejea Royal Tour kule Marekani...badae akasema eti tutaambiwa majina ya wafadhili wa safari hadi leo anaona aibu kuwataja!.
 
Nilimsikiliza mwanasheria Mama mmoja wa Kenya akidadavua jinsi ambavyo Nchi yetu inaingizwa chaka ktk mkataba huu, lakini nikajisemea moyoni kwamba Kenya wana hofu na mafanikio ya Bandari yetu endapo biashara hii itakuwa postive, kwa maana port ya Mombasa na Lamu ni competitor wetu, japo hakuna aliyewahi kutoboa bila ku take risk lakini naanza kuona umuhimu wa kuwasikiliza wanaNchi kabla ya kulipeleka jambo hili haraka haraka.
jambo hili la bandari na kujengwa kwa bandari ya Bagamoyo ambayo JPM aliikataa ni pacha, na maelezo ya PM siamini kwamba suala la DP world linaanzia kwenye DUBAI TRADE FAIR, Hi inaanzia awamu ya Nne na inawezekana kuna ahadi inayosubiliwa kutimizwa na ninaanza kuona azima ya ulazima wa kubadilisha ikologia ya majabu ya dunia ya wanyama kuishi na wanadamu kwa kusudi linaloonekana jema la kuwahamishia Msomera ili Ngorongoro ibakie huru, tusisahau ile kelele ya awamu ya Nne ya kusafirisha wanyama hai kupelekwa nje. kIla kiongozi ana historia yake, iwe njema au mbaya, vizazi vijavyo vitatoa hukumu.
niseme Mama Samia imalize hiyo ahadi tusije kukaa tunaogopa ogopa kumbe huko mbele kuna mambo mema, kama mabaya itakuwa agenda ya historia yako, vilio vya Watanzania huko mbele yakitokea machafuko machozi yatakuwa yetu wote ikitokea neema itakuwa yetu wote hivyo Samia fuata dhamira ya sauti ya Mungu inayonong'oneza moyo wako. ya kuambiwa weka pembeni yasitengeneze hukumu yako.
 
Unaijua GDP ya tz kabla na baada ya jk!?..GDP huja tu bila uongozi thabiti!?..au umekula sakrament ukashushia divai,unajamba chuki tu now!?
 
Hivi Tulia spika wa Bunge haoni aibu kwa yanayoendelea? Ilitakiwa pale serikali iagizwe kurekebisha baadhi ya mambo ndipo waendelee kupitisha azimio, pale hata kama sio mwanasheria lakini bado utaona mapungufu ya wazi kabisa yaliopo
Hata mimi najuliza hilo swali
 
Nakubaliana na wewe...Hata hayo madini yaunganishwe humo humo mikataba yake kuidai iwe reveiwed, tuanze upya...Hapa kama taifa tumekwama, tunahitaji utashi wa dhati kulikwamua taifa bila kujali dini, itikadi ama kabila...At the end we are all Tanzanians
 
Nimesikiliza Clip ya Waziri Mkuu inayo trend, naye amejikita kutetea Mwekezaji, lakini anasahau Watu wanahoji aina ya Mkataba.
Hana la kufanya kwakua huwezi kutetea kitu ambacho ni obviously hakina substance
 
Hapa kwakweli hawa hitoria itawakumbuka kama akina Mangungo...What a shame!
Shida ya wabunge wetu ni kutokutana na wananchi, wao muda wote wako kwenye biashara zao, wakitoka huko hawana jipya, ni wakati sasa bunge lipunguzwe ukubwa wake liwe controlled na wananchi na ikitokea mbunge hana ufanisi basi aondolewe bila kujali kama muda wake umekwisha au la
 
 

Attachments

  • 6FAA82CE-F3F5-49E4-92EF-D6657E342487.jpeg
    26.4 KB · Views: 2
  • 2C37D26F-428D-4F25-A22B-5A9EE53ABF5B.jpeg
    48.5 KB · Views: 2
Kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…