BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATANZANIA WOTE KWA UCHAGUZI MKUU WA AMANI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtumia salamu za pongezi Rais Jakaya Mrisho Kikwete na watanzania wote kwa kukamilisha uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani na utulivu.
Katika pongezi hizo, Ban Ki Moon anasema , Mhe Rais, niruhusu nitumie fursa hii kuipongeza serikali yako, wananchi wa Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC),kwa kukamilisha uchaguzi mkuu uliokuwa umeandaliwa vizuri na kufanyika katika mazingira ya amani na uwazi.
Amesema kwa mara nyingine kwa kupitia uchaguzi mkuu uliomalizika, watanzania , vyama vya siasa na viongozi wa vyama hivyo wameonyesha ukomavu mkubwa na utashi wa kudumisha amani na demokrasia.
Aidha katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemhakikishia Rais Jakaya Kikwete na serikali yake ushirikiano usioyumba kutoka kwake.
Na kwamba UN itaendele kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa malengo na maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Source: UN-HQ , NY
COMMENT: Mnaotaka kuandamana huko ughaibuni, msisahau kufika pia UN HQ.
You are wasting your time!
Mawazo ya ki-kokoto!

Hapa nadhani suala muhimu ni kujiuliza wale waangalizi wanaotumwa na UN &ts affiliates huwa wanaenda kuripoti nini wakirudi huko kwa wakubwa zao.. Nadhani ingekuwa busara uwekwe utaratibu wawe wanadisclose taarifa nzima kwa vyombo vya habari nchini; taarfa hizo zikiakisi ukweli halisi ndio waruhusiwe kuzipeleka UN &affiliates. Vinginevyo wataendelea kufuga donda pasi kulitibu., matokeo yake....
Mlitaka aseme kuwa Chadema ndio imeshinda kura?
Mbona hamueleweki?