Elections 2010 Ban ki Moon na uchaguzi wa Tanzania

Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATANZANIA WOTE KWA UCHAGUZI MKUU WA AMANI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtumia salamu za pongezi Rais Jakaya Mrisho Kikwete na watanzania wote kwa kukamilisha uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani na utulivu.

Katika pongezi hizo, Ban Ki Moon anasema , “ Mhe Rais, niruhusu nitumie fursa hii kuipongeza serikali yako, wananchi wa Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC),kwa kukamilisha uchaguzi mkuu uliokuwa umeandaliwa vizuri na kufanyika katika mazingira ya amani na uwazi”.

Amesema kwa mara nyingine kwa kupitia uchaguzi mkuu uliomalizika, watanzania , vyama vya siasa na viongozi wa vyama hivyo wameonyesha ukomavu mkubwa na utashi wa kudumisha amani na demokrasia.

Aidha katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemhakikishia Rais Jakaya Kikwete na serikali yake ushirikiano usioyumba kutoka kwake.

Na kwamba UN itaendele kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa malengo na maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

Source: UN-HQ , NY

COMMENT: Mnaotaka kuandamana huko ughaibuni, msisahau kufika pia UN HQ.

You are wasting your time!

Mawazo ya ki-kokoto!
 
Huyo Ban ki moon hajui anachozungumnza, hajui machungu tuliyonayo..
Chonde chonde Migiro, mwambie ukweli tuu, msimchakachue huyo mkorea wa watu..
 
Ban Ki Moon ni wale wale wanaopelekea vijikaratasi wakasoma tu bila kujua au kuhoji uhalali na uhalisia wa hali halisi kama JK.

Hii haina siri kuwa Pembeni ya Ban Ki Moon yupo kada wa juu wa JK na Chama chake cha ufidhuli, yaana mama Migiro, na tunavyomjua, kamwe hawezi kukubali hata siku moja serikali iliyomtuma kule aiseme kama ni feki...si mnajua anapenda aendelee kubakia alipo au hata 2015 aweze kuwekwa angalau ktk list ya warithi wa Rais wa wachakachuaji!!
 
BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATANZANIA WOTE KWA UCHAGUZI MKUU WA AMANI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtumia salamu za pongezi Rais Jakaya Mrisho Kikwete na watanzania wote kwa kukamilisha uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani na utulivu.

Katika pongezi hizo, Ban Ki Moon anasema , “ Mhe Rais, niruhusu nitumie fursa hii kuipongeza serikali yako, wananchi wa Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC),kwa kukamilisha uchaguzi mkuu uliokuwa umeandaliwa vizuri na kufanyika katika mazingira ya amani na uwazi”.

Amesema kwa mara nyingine kwa kupitia uchaguzi mkuu uliomalizika, watanzania , vyama vya siasa na viongozi wa vyama hivyo wameonyesha ukomavu mkubwa na utashi wa kudumisha amani na demokrasia.

Aidha katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemhakikishia Rais Jakaya Kikwete na serikali yake ushirikiano usioyumba kutoka kwake.

Na kwamba UN itaendele kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa malengo na maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

Source: UN-HQ , NY

COMMENT: Mnaotaka kuandamana huko ughaibuni, msisahau kufika pia UN HQ.

You are wasting your time!

Mawazo ya ki-kokoto!

ban k moon siku izi anaandika kiswahili? Tena kiswahili cha kiuni? Au ban k moon wa kiswaili? Ama kweli wabongo majuha,kishongo jifunze kudanganya!
 
BAN KI MOON AMPONGEZA JK NA WATANZANIA WOTE KWA UCHAGUZI MKUU WA AMANI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtumia salamu za pongezi Rais Jakaya Mrisho Kikwete na watanzania wote kwa kukamilisha uchaguzi mkuu katika mazingira ya amani na utulivu.

Katika pongezi hizo, Ban Ki Moon anasema , “ Mhe Rais, niruhusu nitumie fursa hii kuipongeza serikali yako, wananchi wa Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC),kwa kukamilisha uchaguzi mkuu uliokuwa umeandaliwa vizuri na kufanyika katika mazingira ya amani na uwazi”.

Amesema kwa mara nyingine kwa kupitia uchaguzi mkuu uliomalizika, watanzania , vyama vya siasa na viongozi wa vyama hivyo wameonyesha ukomavu mkubwa na utashi wa kudumisha amani na demokrasia.

Aidha katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemhakikishia Rais Jakaya Kikwete na serikali yake ushirikiano usioyumba kutoka kwake.

Na kwamba UN itaendele kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa malengo na maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Tanzania.

Source: UN-HQ , NY

COMMENT: Mnaotaka kuandamana huko ughaibuni, msisahau kufika pia UN HQ.

You are wasting your time!

Mawazo ya ki-kokoto!

ban k moon siku izi anaandika kiswahili? Tena kiswahili cha kiuni? Au ban k moon wa kiswaili? Ama kweli wabongo majuha,kishongo jifunze kudanganya, vizuri au ukae kimya!
 
huyo kachakachuliwa na huyo mingiro mache angee huo ujinga wake cc atumwelewi atakidogo
"people is power"(chadema)
 
Hizi salaam zimeandikwa na asha migiro-b-moon hamjui mkwere!!!!!!!!!!! tusidanganyane -wanaJF HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!!!!!????????????
 
Siasa za UN ziache zilivyo huzifahamu,kifupi wao wanaangalia kama vurugu hazijatokea watukuandamana mabarabarani,watukuumizwa na vyombo vya dola havijamwagika damu Swala la nec wakichakachua wao hawana chukuongeza wala kupunguza wao wana generaliez,pili hawezi akasema kitu kibaya kwa tanzania kwani ndiyo nchi pekee kurayake iliyo mwingiza madarakani UN,tz wasingepiga kura Ban asingekuwa katibu mkuu!shukurani zake ndo huyo migiro!!pili kumbuka wakati yeye ni waziri wa nje korea,Jk ni waziri wa nje tz hivyo hakuna chochote anaweza kusema zaidi yakusifia.
 
Mlitaka aseme kuwa Chadema ndio imeshinda kura?

Mbona hamueleweki?
 
Hapa nadhani suala muhimu ni kujiuliza wale waangalizi wanaotumwa na UN &ts affiliates huwa wanaenda kuripoti nini wakirudi huko kwa wakubwa zao.. Nadhani ingekuwa busara uwekwe utaratibu wawe wanadisclose taarifa nzima kwa vyombo vya habari nchini; taarfa hizo zikiakisi ukweli halisi ndio waruhusiwe kuzipeleka UN &affiliates. Vinginevyo wataendelea kufuga donda pasi kulitibu., matokeo yake....
 
Hutu katibu mkuu sidhani kama ana muda wa kufatilia mambo ya dunia ya tatu wakati nchi yake na majirani wanapigiana ubabe hawezi kuwa na update za bongo, so tunatumia cheo cha migiro kujitengenezea habari za kujiridhisha. They will never understand Africa let alone TZ
Hapa nadhani suala muhimu ni kujiuliza wale waangalizi wanaotumwa na UN &ts affiliates huwa wanaenda kuripoti nini wakirudi huko kwa wakubwa zao.. Nadhani ingekuwa busara uwekwe utaratibu wawe wanadisclose taarifa nzima kwa vyombo vya habari nchini; taarfa hizo zikiakisi ukweli halisi ndio waruhusiwe kuzipeleka UN &affiliates. Vinginevyo wataendelea kufuga donda pasi kulitibu., matokeo yake....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom