BALUKTA.... Kwanini Ilifutwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BALUKTA.... Kwanini Ilifutwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bujibuji, Sep 14, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  Hiki chombo kilichokuwa kinajulikana kama baraza la kuhifadi kuran tanzania, kwanini lilifungwa?
  Sasa ni muda mrefu umepita tangu kuvunjwa kwake na bado jibu sijapata, naomba msaada wenu
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nadhani mada hii ni ya jukwaa la dini...i wonder why its under SIASA!

  Lakini kimsingi nakumbuka BALUKTA iLikuwa na msigano mkubwa sana na BAKWATA, wakiituhUMIANA KUWA kimojawapo ni chombo cha propaganda cha serikali!...Pia BALUKTA waliibuka kuwa na misimamo mkali wa dini (Mujahidina), wakikashifu na kukejeli kila aliyekuwa kinyume nao!
  Nategemea kukosolewa na kusahihishwa!
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu uko sahihi, ila ipelekwe kwenye jukwaa husika.
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  BARAZA LA KUCHAKACHUA TANZANIA...!:mad2:
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  Haha haha haha haha aaaa hiii kali
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Guess who was behind it all......the very SHEIKH YAHAYA HUSSEIN :lol:
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  SIKU ya Jumatatu Aprili mosi, 1991 ilikuwa mbaya sana kwa Sara (jina halisi linahifadhiwa), msichana kutoka Mkoa wa Iringa aliyekuwa anaishi na dada yake eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ilikuwa ni ya pili ya Pasaka, yaani Easter Monday kwa Kiingereza, na Sara (aliyekuwa na umri wa miaka 20 wakati huo) aliamua kufanya matembezi katikati ya jiji.

  Ilikuwa majira ya saa nne usiku alipoingia katika Hoteli ya Kilimanjaro kwenye ukumbi wa burudani, ilipokuwa inatumbuiza bendi maarufu ya The Tanzanite's. Akiwa ukumbini hapo, alijikuta akifahamiana na Wazungu wanne waliomkaribisha kinywaji aina ya Vodka.

  Ilipotimia majira ya saa sita usiku, Wazungu wale walimshawishi Sara afuatane nao kwenda kwenye nyumba ya mmoja wao eneo la Mlalakuwa. Sara alifikiri Wazungu wale walikuwa watu waungwana kwa kuwa walionyesha ukarimu kwake. Walimchukua katika gari lao hadi katika nyumba hiyo na kumkaribisha sebuleni kwa vinywaji zaidi. Kwa vile Sara alikuwa si mwenyeji sana katika Jiji la Dar es Salaam hakujua ramani ya eneo alilokuwa huko Mlalakuwa.

  Baada ya kutosheka na vinywaji, Wazungu wale walimwacha Sara peke yake sebuleni na kwenda zao kulala vyumbani. Usiku wa manane ulipowadia, Wazungu waliamka na kumtoa Sara sebuleni hadi baraza ya kando ya nyumba. Walimshika kwa nguvu, wakamvua nguo zake na kubakia kama alivyozaliwa.

  Baada ya hapo walimchukua mbwa wao na kumgeuza ‘mume' wa Sara! Kitendo hicho kilifanywa kwa nguvu bila Sara kuridhia wala kuweza kujitetea. Mmoja wa Wazungu wale alikuwa anapiga picha kwa kamera yake ndogo wakati mbwa akifanyishwa ngono na Sara.

  Baada ya ya unyama huo, Sara alipakiwa katika gari na kurudishwa katikati ya jiji na kuachwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Hospitali ya Ocean Road. Maskini Sara alikuwa amedhalilishwa kiasi cha kuona hana tena thamani katika dunia, hivyo alitaka kujiua kwa kujitosa baharini.

  Wakati akihangaika hovyo karibu na alfajiri, askari polisi wa ulinzi baharini walimwona na kumwokoa. Baadaye aliwasimulia yaliyomkuta, wakaamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa Muhimbili (wakati huo) kupima afya yake.

  Madaktari walithibitisha kwamba ni kweli alikuwa ameingiliwa kimwili na mnyama. Uthibitisho huo uliwapa fursa polisi kuanza uchunguzi. Wakati polisi wanafanya uchunguzi, habari hizi zilifika Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) wakati huo na kuandikwa katika gazeti la serikali la Sunday News la Aprili 7, 1991. Siku chache baadaye, polisi walifanikiwa kujua nyumba ambayo Sara alifanyiwa unyama na kuwatia mbaroni Wazungu wale.

  Polisi hawakuchelewa kufungua mashtaka mahakamani (wakati huo Kivukoni). Wazungu walipelekwa kusomewa mashtaka na kunyimwa dhamana. Siku walipofikishwa mahakamani, watu wengi walifika kutaka kuona Wazungu hao walikuwa watu wa aina gani.

  Pale Kivukoni ilipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara hivi sasa, palifurika watu ambao hawajawahi kuonekana tena eneo hilo. Dk. Masumbuko Lamwai ndiye alikuwa wakili wa utetezi na hoja zake za kuomba dhamana kwa washtakiwa zilishindwa, kwani hakimu alisema wakiachiwa wanaweza kudhuriwa vibaya na jamii iliyokuwa imekasirishwa sana na habari za unyama waliofanya.

  Baada ya mwezi mzima wa kesi, serikali ilitoa hati ya kuwafukuza nchini Wazungu wale, kama watu wasiotakiwa kufika tena hapa Tanzania. Ilibainika baadaye kwamba walikuwa ni raia wa Ujerumani na walikuwa nchini kama wataalamu wa kigeni (expatriates) wakati huo maarufu kama ‘TX'.

  Serikali ilichukua hatua hiyo baada ya kuona kesi hiyo inaweza kujenga hisia za kibaguzi katika jamii, kwani tayari watu wengi walianza kuonyesha chuki mbaya kwa Wazungu wote, wakiwamo watalii, wawekezaji na mabalozi. Ulikuwa ni uamuzi wa busara sana wa Serikali ya Awamu ya Pili chini ya Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

  Lakini busara hizo hazikuzingatiwa sana, kwani habari za uchunguzi zinasema Wazungu wawili miongoni mwa wale wanne, walirudi tena nchini kinyemela. Inasadikiwa walirudi chini ya mwavuli wa dhehebu moja la dini. Hadi sasa haifahamiki kama walitumia majina mengine ya bandia na kama bado wapo nchini, lakini habari za kuonekana kwao tena Dar es Salaam zilifahamika tangu 1997.

  Wakati Sara alipodhalilishwa, hakuna kiongozi yeyote wa dini aliyetokeza kukemea au hata kutoa tahadhari yoyote kwa jamii. Viongozi wa dini walikaa kimya hadi kesi ikafunguliwa na dola na hatimaye washtakiwa kutimuliwa.

  Kimya hiki cha viongozi wa dini zote kimeendelea hadi leo. Lakini katika kipindi hicho hicho (1991-95), viongozi kadhaa wa vikundi vya kidini waliendesha mihadhara kadhaa ya kukashifiana kidini.

  Ni katika kipindi hicho ambapo kikundi fulani cha waumini wa dini waliandamana kuitaka serikali ifute leseni za maduka ya nyama za nguruwe yaliyo katika makazi ya watu wengi.

  Maandamano hayo yalihitimishwa kwa waandamanaji kuvunja maduka kadhaa ya nyama za nguruwe na kuharibu mali za wafanyabiashara hiyo maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Dhima ya maandamano ilikuwa ‘vita dhidi ya makafiri na biashara zao'.

  Hatua iliyofuata ni kwa rais kuhutubia taifa na kukemea udini. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Rais mstaafu Mwinyi kuitwa ‘Mzee Ruksa', kwani katika hotuba yake hiyo alisema kila raia wa taifa hili ana haki sawa na mwingine, anaweza kuishi popote, kufanya biashara yoyote na kula chochote apendacho akizingatia sheria.

  Hotuba hii ndio iliyochochea chuki kati ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Baraza la Kuendeleza Kuran Tanzania (BALUKTA) lililokuja kufutwa rasmi na serikali. Uhasama ulitokana na BAKWATA kuunga mkono hotuba ya Rais Mwinyi wakati BALUKTA ilipinga ‘ruksa' iliyotangazwa.

  Hotuba ya rais iliwapa jeuri wafanyabiashara wa nyama ya nguruwe ambao waliendelea kufungua maduka kwa wingi na kuuza hadharani ‘kitimoto' kwenye baa mbalimbali. Mfumo wa vyama vingi vya siasa ulioanzishwa tena rasmi 1992 uligongana na mgogoro huu. Wanasiasa waliokuwa wanatafuta umaarufu kwa gharama nafuu, walijitosa kuchochea pande zilizokuwa zinagongana (BAKWATA na BALUKTA).

  BALUKTA walianza kufadhili mihadhara ya kashfa dhidi ya dini nyingine zilizoitwa za makafri, hasa Kanisa Katoliki. Baadhi viongozi wa dini nyingine walidai serikali ilikuwa inafurahia hali hiyo, ndiyo maana ilikuwa haichukui hatua dhidi ya mihadhara hiyo.

  Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo alikuwa, Augustine Mrema. Serikali ilimwagiza kutatua tatizo hilo. Haraka haraka, Mrema aliwaita ofisini viongozi wa BALUKTA chini ya Shekh Yahya Hussein na kuwaasa waache kufadhili mihadhara ya uchochezi dhidi ya BAKWATA, Rais Mwinyi, serikali na dini nyingine.

  Bila woga, viongozi wa BALUKTA walikataa agizo hilo waziwazi. Hatimaye Mrema akaagizwa na rais wake kuwakamata na kuwafungulia mashtaka ya uchochezi viongozi wote wa BALUKTA. Hatua hiyo ilikwenda sambamba na kufutwa rasmi usajili wake.

  Mrema alitekeleza maagizo hayo, lakini akitumia kauli zilizofanya BALUKTA wadhani huo ulikuwa uamuzi wake binafsi. Hatimaye kesi dhidi ya viongozi hao ilifutwa na serikali na wakaachiwa huru baada ya kukiri kwamba hawatajihusisha tena na uchochezi.

  Lakini uchochezi haukuisha kabisa, kwani wanasiasa ndani ya serikali kama hayati Profesa Kighoma Malima, aliyekuwa Waziri wa Fedha walikuwa wanapinga kisirisiri hatua za serikali kufuta BALUKTA.

  Wakati alipohama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), baada ya kuondolewa kwenye Baraza la Mawaziri, hayati Malima alilishutumu Kanisa Katoliki kwamba alipokuwa waziri lilikuwa linamhujumu na kuipotosha serikali.

  Kwa kuzingatia elimu yake na nafasi za juu alizowahi kupewa serikalini, hayati Malima alipata wafuasi wengi kabla ya kifo chake kilichotokea ghafla akiwa Ulaya kama mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama chake kipya, alichokuwa amekibadilisha na kuitwa NAREA.

  Viongozi wa NRA akiwemo hayati Abubakar Ulotu waliishutumu CCM na serikali kwa kifo cha Profesa Malima wakidai kilipangwa. Hizi zilikuwa ni shutuma mbaya sana dhidi ya serikali, lakini busara za mzee Mwinyi zilitumika kufuta hisia hizo kwa kushiriki kwake kikamilifu katika mazishi ya Profesa Malima.

  Hata hivyo, wanasiasa kadhaa walitaka sana kujaribu kumtumia mwana wa Profesa Malima kuendeleza chuki za kidini na kisiasa. Adam Kighoma Malima alipewa nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya NRA na hatimaye CUF, lakini akashindwa kwa kura nyingi. Hatimaye alijirudisha CCM na kushinda ubunge wa Mkuranga 2005.

  Historia hii inaonyesha uhusiano wa dini na siasa unavyoweza kuleta madhara kutokana na wanasiasa dhaifu kupenda umaarufu wa kirahisi kwa kuhubiri chuki na uchochezi.

  Hivi sasa jamii ya Tanzania inakomaa katika siasa za ushindani wa vyama na kuanza kubainisha wanasiasa wa aina hiyo. Lakini wanasiasa wapenda umaarufu nafuu wanabuni mbinu mpya. Mbinu mojawapo hivi sasa ni ya kutumia migogoro ya mbali kama ya huko Mashariki ya Kati.

  Ili kujenga uchumi kwa kuvutia vitega uchumi, serikali imekuwa ikijitahidi sana kujenga uhusiano mwema na jumuiya ya kimataifa. Kwa kuzingatia hilo, imekuwa ikisita sana kutoa kauli za kupinga au kuunga mkono pande zozote za migogoro nje ya nchi.

  Lakini viongozi dhaifu ndani ya vyama vya siasa na dini kadhaa wamekuwa wakiishinikiza serikali ijiingize katika migogoro ya nje. Hawafanyi hivyo bila malengo, kwani hapa nchini zipo ofisi za kibalozi ambazo zinafadhili viongozi wa kidini na siasa wanaosambaza propaganda za kulinda maslahi fulani ya kigeni.

  Inashangaza, kwa mfano jinsi viongozi wengi wa kidini walivyokaa kimya kuhusu migogoro ya nchi za jirani kama Burundi, Rwanda, Uganda, Somalia, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini wanaguswa zaidi na migogoro ya Mashariki ya Kati. Wasomali wanaouana kwa miaka 16 hadi sasa, Sudan pia, Kongo na Burundi hakujatulia lakini viongozi wa dini hapa wako kimya!

  Wakati huo huo, vita ya Israel na Hezbollah iliyokuwa idumu wiki tatu tu, ilivuta na kuzua maandamano ya kulaani mauaji ya watu wasio na hatia. Je, wale Waafrika wenzetu mafukara wa Somalia wanaokufa kwa njaa kutokana na vita ya kikabila hawana roho bora kama za Walebanon?

  Mbona mauaji ya watu weusi wa Darfur yanayofanywa na Janjaweed hayalaaniwi kwa maandamano? Kwa nini mauaji ya kinyama ya watoto yanayofanywa huko kaskazini mwa Uganda na kikundi cha Lord's Resistance Army (LRA) hayajatolewa kauli yoyote na viongozi wa dini zetu hapa Tanzania? Ukimya ulikuwa ni hivyo hivyo kwa miaka kadhaa ya vita ya ndani huko Angola, Msumbiji, Chad, Sierra Leone, Liberia, Ivory Coast, Djibouti, Madagascar, Rwanda na Burundi.

  Viongozi wote wa dini wana wajibu wa kutetea roho zisizokuwa na hatia zisiteketezwe hovyo, lakini cha ajabu Mashariki ya Kati kunaonekana kwa na roho bora zaidi. Kiongozi wa Msikiti wa Idrisa uliopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, Sheikh Ally Basaleh alisema Agosti 9, mwaka huu kwamba vita ya Israel na Hezbollah iliyosimamishwa hivi karibuni ilikuwa ni vita ya Ukristo dhidi ya Uislamu.

  Kiongozi huyo alisema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na Radio Times 100.5 FM katika kipindi cha Dira. Kauli ya kiongozi huyo inaonyesha wazi dhamira yake kuhamisha mgogoro wa kijadi wa huko Mashariki ya Kati na kuuleta Tanzania kwa kuchonganisha Wakristo na Waislamu wa hapa.

  Juu ya yote, inawezekana pengine kiongozi huyo hafahamu vizuri historia ya migogoro ya Mashariki ya Kati, lakini pengine anafahamu, anapotosha makusudi ili kutimiza kazi ya propaganda aliyotumwa kama wakala wa nchi au jamii fulani. Lakini kwa bahati mbaya, kauli potofu ya kiongozi huyo ilichapishwa tena katika gazeti la Dar Leo la Agosti 11, 2006 na kuzidi kusambaa.

  Mtu makini anajua fika kwamba vita ya Israel na Hezbollah si kweli kwamba ni ya Ukristo na Uislamu. Kwanza Israel si dola ya kidini kama ilivyo Iran, na pia Wayahudi wengi wanaamini dini ambayo inapingana kabisa na Ukristo. Huko Lebanon nako kuna Wakristo asilimia 17 na hao pia waliathirika kwa mabomu ya Israel.

  Mgogoro mpya ulioibuka karibuni huko Mashariki ya Kati, chimbuko lake ni kauli ya Rais Mahmud Ahmedinejad aliyesema taifa la Israel linastahili kufutwa katika ramani ya dunia. Iran inafadhili Hezbollah ili kuishambulia Israel, lakini wakati huo huo haijamfadhili Osama bin Laden ambaye pia anataka Israel itokomezwe.

  Hii ni kwa sababu Hezbollah na Iran ni waumini wa Shia wakati Osama na Saudi Arabia ni waumini wa Suni. Hii inaonyesha wazi kwamba, lengo la Hezbollah na Iran limejifunga katika imani ya kidini (Shia) zaidi ya kuipinga Israel.

  Eneo ilipo Israel na Palestina ndio mahali penye kumbukumbu za dini kuu za dunia hii na kumbukumbu hizo ni hazina kubwa kwa biashara ya utalii.

  Kumbukumbu hizo zinatakiwa kuhifadhiwa, lakini hofu ya mataifa makubwa yanayounga mkono Israel ni kwamba, dola zenye imani kali za kidini kama Iran zikiachiwa mamlaka kutawala eneo hilo, zitatokomeza baadhi ya kumbukumbu hizo na kupotosha historia.

  Kuna taarifa kwamba wakati Umoja wa Mataifa uliosaidia katika kuunda taifa la Israel 1948 na kulipa ardhi hiyo, ulitoa sharti la kulindwa kwa sehemu zote muhimu za kihistoria katika miji ya Jerusalemu na kando yake. Hayo ndiyo maslahi ambayo Marekani na dola za Ulaya zinayalinda wala si Ukristo.

  Viongozi wa awali wa Israel walifanya juhudi kubwa kuyaridhisha mataifa tajiri ya Ulaya na Marekani kwamba watalinda hifadhi hizo, japokuwa Wayahudi wengi hawana imani na Ukristo wala Uislamu.

  Wayahudi wanafaidika tu kwa mapato ya utalii. Wakati Wayahudi walifanikiwa kuyashawishi mataifa makubwa kuwaunga mkono, Wapalestina walishawishi mataifa ya Kiarabu na nchi zinazoendelea kuwaunga mkono. Kila upande umepata mafanikio, kwani Palestina wameunda taifa lao na kurudishiwa sehemu ya ardhi yao. Israel nayo imepata nguvu nyingi za kiuchumu na silaha bora za kujihami toka Marekani na Ulaya.

  Sasa linapokuja suala la vita, ni wazi kwamba mwenye nguvu ndiye anaponda mnyonge. Israel haijatumia sana fedha wala muda kusambaza propaganda katika nchi maskini, ndiyo maana hata hapa Tanzania hatusikii sana mambo yao.

  Wayahudi wanajua sana propaganda, lakini wanajali zaidi maslahi ya kiuchumi, hivyo nguvu kubwa za ushawishi zimeelekezwa kwa nchi tajiri. Palestina kwa upande wao, wanaona hawawezi kuishinda Israel kwa propaganda katika nchi tajiri, hivyo wanaelekeza zaidi nguvu zao katika mataifa ya Kiarabu na Afrika. Kwa bahati mbaya, eneo ambalo Wapalestina na Waarabu wanasambaza propaganda, hakuna teknolojia za kisasa za kivita wala uchumi imara.

  Juu ya yote, Wapalestina wanashindwa kushawishi watu katika nchi tajiri kwa sababu jamii za huko zimeelimika na zinatafakari mambo kwa kina kabla ya kupokea propaganda. Israel imefanikiwa huko kwa kuwa ina matajiri na wasomi wengi wahamiaji katika nchi zilizoendelea.
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwenye red: Naikumbuka hii. Kesi ilifutwa kwa sababu wakati ule sheria inayoweza kumtia hatiani mtu 'anayelazimisha mwanamke kufanya ngono na mnyama' kulikuwa hakuna -- under Penal Code au sheria nyingine yeyote ile. Ilikuwapo ile tu inayomkataza binadamu, kwa utashi wake, kufanya ngono na mnyama.
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
 10. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ndo kwanza nalisikia leo hilo baraza
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Jamani mbona tunachanganya dini na siasa!?
   
 12. E

  Eddie JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwandishi hapo kwenye nyekundu kapatwa na magengeza, nia yake kushambulia uislamu na waislamu tu UDINI kwa kwenda mbele!
   
Loading...