Balozi za Tanzania nje kufikia 50 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi za Tanzania nje kufikia 50

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 21st October 2011

  SERIKALI inatarajia kuongeza Balozi za Tanzania nje ya nchi kutoka 32 hadi 50 ifikapo mwaka 2020 kwa lengo la kuwafikia wawekezaji wengi zaidi ili kuimarisha diplomasia ya uchumi wa nchi na kupunguza utegemezi.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru ya wizara hiyo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  “Hadi sasa Tanzania ina balozi 32 za nje hivyo ni lazima tupanue wigo ili kuimarisha uchumi na hatua ya kwanza tuliyoanza nayo kwa sasa ni kujenga vitega uchumi katika balozi zetu na kuhamasisha mabalozi wetu kuitangaza nchi kwa utalii,” alisema.

  Alisema kuwa katika awamu ya tatu ya uongozi, nchi imejenga diplomasia ya uchumi ambapo wameagiza balozi zote zilizopo nje kuzisaidia wizara ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa zilizopo duniani.

  Aidha alisema kuwa wizara hiyo imeanzisha mpango wa kuwakutanisha Watanzania zaidi ya milioni mbili waliopo nje ya nchi ili kuwashirikisha katika kuchangia maendeleo ya nchi na kujenga uchumi kwa kuwahamasisha kutangaza fursa za utalii na uwekezaji kwa mataifa mengine.

  Akizungumzia suala la amani ya nchi, Membe alisema kuwa inatokana na misingi imara aliyoijenga Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alihamasisha mshikamano, amani na utulivu.

  “Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani ambazo zimemaliza miaka 50 ya Uhuru bila kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, zipo nchi ambazo kila nyumba ina handaki la kujificha vita vinapoanza, pia zipo nchi ambazo wananchi wao wapo tayari kuliwa na simba kuliko kuuawa.

  “Tanzania itaendelea kuwa na amani na utulivu kama miaka 50 iliyopita kwa kuwa tumepokezana awamu nne za uongozi wa demokrasia kitu ambacho nchi nyingi zimeshindwa kufanya uchaguzi wa demokrasia.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Haya Marafiki wa Rais na Watoto wa Wakubwa Chungeni sana hizo balozi Mpya
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,506
  Trophy Points: 280

  "Wachukuaji" sasa basi mpaka hapo tutakapokuwa na watu makini watakaoweza kusaini mikataba ambayo yenye manufaa kwa Tanzania na Watanzania, na siyo kama hii ya sasa ambayo tunaibiwa mchana kweupe huku wageni na shareholders wao wakitajirika kwa rasilimali zetu.
   
Loading...