Balozi wa US alikuwa anafanya nini Dodoma?

Balozi wa US alikuwa anafanya nini Dodoma?

KRS

Member
Joined
Sep 9, 2014
Posts
32
Reaction score
5
Asubuhi ya leo Dodoma,magari kuelekea njia ya uwanja wa ndege yalikuwa yamesimamishwa kwa kipindi kirefu kidogo!! wengi tulijua ni viongozi wetu wa kitaifa!! na hali hii kwa dodoma mi kawaida kabisa!!! msafara ulipopita tuligundua ni balozi wa US!!!kwa walio na taarifa alikuwa anafanya nn hapa dodoma tukizingatia issue ya escrow iko moto tujuzane!!!nawasilisha wakuu!!
 
Mkuu leo ni siku muhimu sana kwa nchi hii, tutajua mbivu na mbichi.
 
Alikuwa anaulizwa watu wakipigwa chini itatosha Us kufund bajeti ama mpaka wapelekwe keko? ...loading
 
Asubuhi ya leo Dodoma,magari kuelekea njia ya uwanja wa ndege yalikuwa yamesimamishwa kwa kipindi kirefu kidogo!!
hapo ndio unapom miss Julius Nyerere.

Ulikuwa huwezi siku zile kusimamishwa njiani eti balozi wa Marekani anapita na msafara, hata siku moja!

Sasa siku hizi haka kanchi kamepata mjomba huko nje, kama alivyokuwa akisema mwenyewe, inabidi tuwalambe viatu.

Huwezi kusimamisha watu barabarani Washington DC eti balozi Mula Mula wa Tanzania anapita, watamlenga shabaha!
 
Asubuhi ya leo Dodoma,magari kuelekea njia ya uwanja wa ndege yalikuwa yamesimamishwa kwa kipindi kirefu kidogo!! wengi tulijua ni viongozi wetu wa kitaifa!! na hali hii kwa dodoma mi kawaida kabisa!!! msafara ulipopita tuligundua ni balozi wa US!!!kwa walio na taarifa alikuwa anafanya nn hapa dodoma tukizingatia issue ya escrow iko moto tujuzane!!!nawasilisha wakuu!!
.........anataka aone ukomo wa upeo wetu wa kufikiri hasa ktk suala la ESCROW na jinsi tusivyokuwa na aibu katika mambo ya msingi yahusuyo taifa letu;
 
Wao ndo wenye kutoa hela za millenium challenge. Wanaangalia kama hela zinapigwa kijinga, kwa mini aaendelee kutoa
 
Back
Top Bottom