Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,796
- 5,508
Wadau, leo 06 July 2016, Gazeti la Mwananchi limechapisha makala ya Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress isemayo, "Vita dhidi ya Ufisadi isiondoe Demokrasia."
Ktk makala yake, Balozi Childress anaandika, "ninaguswa pale sauti za Watanzania zinapopazwa na kutoa malalamiko kuhusu kuminywa kwa demokrasia, iwe ni kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa au kuzuia matangazo ya televisheni vya vikao vya Bunge."
"Ninaamini kwamba mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa hakika ni muhimu kwa nchi zetu mbili ni lazima yafanyike bila kukwaza majadiliano, hali ya kutofautiana maoni au kuwepo kwa uhuru wa kujieleza ".
Balozi Childress amekumbusha kuwa, Ukweli ni kwamba mkinzano wa kibunifu kati ya mawazo tofauti yanayoshindana ndiyo huifanya demokrasia kuimarika, kustawi na kuwa hasa ya uwakilishi wa watu.
Hiyo ni sehemu tu ya makala ya Balozi Childress ambayo inapatikana kwa ukamilifu ktk Gazeti hilo.
Mawazo ya Balozi Childress hayana tofauti na Watanzania wengi wasiokuwa na mlengo wa kiitikadi wa vyama vya siasa hapa nchini mwetu. Nakumbuka wiki chache nilikuja na thread humu nikieleza kasoro ninazoziona ktk utawala wa JPM ambazo ni mbili tu kama alivyoandika Balozi Childress leo ingawa wapo wengine walionishukia kwa hasira kama mwewe ashukiavyo kifaranga.
Tuendelee kumuunga mkono utawala JPM, lkn kuukosoa mahali penye makosa, pia ni kumuunga mkono Rais wetu JPM ktk kupiga vita Ufisadi wa aina zote nchini mwetu.
Ifahamike kuwa tunaookosoa kuhusu kuminywa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kupata habari, ni kwa nia njema ya kujenga Taifa imara linalozingatia na kuheshimu haki hizo.
Vv