Balozi wa Marekani atuasa kuhusu Demokrasia

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,737
5,438
Wadau, leo 06 July 2016, Gazeti la Mwananchi limechapisha makala ya Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress isemayo, "Vita dhidi ya Ufisadi isiondoe Demokrasia."

Ktk makala yake, Balozi Childress anaandika, "ninaguswa pale sauti za Watanzania zinapopazwa na kutoa malalamiko kuhusu kuminywa kwa demokrasia, iwe ni kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa au kuzuia matangazo ya televisheni vya vikao vya Bunge."

"Ninaamini kwamba mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa hakika ni muhimu kwa nchi zetu mbili ni lazima yafanyike bila kukwaza majadiliano, hali ya kutofautiana maoni au kuwepo kwa uhuru wa kujieleza ".

Balozi Childress amekumbusha kuwa, Ukweli ni kwamba mkinzano wa kibunifu kati ya mawazo tofauti yanayoshindana ndiyo huifanya demokrasia kuimarika, kustawi na kuwa hasa ya uwakilishi wa watu.

Hiyo ni sehemu tu ya makala ya Balozi Childress ambayo inapatikana kwa ukamilifu ktk Gazeti hilo.

Mawazo ya Balozi Childress hayana tofauti na Watanzania wengi wasiokuwa na mlengo wa kiitikadi wa vyama vya siasa hapa nchini mwetu. Nakumbuka wiki chache nilikuja na thread humu nikieleza kasoro ninazoziona ktk utawala wa JPM ambazo ni mbili tu kama alivyoandika Balozi Childress leo ingawa wapo wengine walionishukia kwa hasira kama mwewe ashukiavyo kifaranga.

Tuendelee kumuunga mkono utawala JPM, lkn kuukosoa mahali penye makosa, pia ni kumuunga mkono Rais wetu JPM ktk kupiga vita Ufisadi wa aina zote nchini mwetu.

Ifahamike kuwa tunaookosoa kuhusu kuminywa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kupata habari, ni kwa nia njema ya kujenga Taifa imara linalozingatia na kuheshimu haki hizo.

Vv
 
Huyo barozi aanze yeye kuimarisha demokrasia ubalozini kwake. Visa kupata ni longo longo. Hata uwe na sababu genuine unanyimwa tu.
 
Huyo barozi aanze yeye kuimarisha demokrasia ubalozini kwake. Visa kupata ni longo longo. Hata uwe na sababu genuine unanyimwa tu.
Siyo hapo tu kamalize matatizo ya kuwaua weusi kwa kutumia askari Polisi. Si bora hapa wanapigwa virungu tu USA river wana wa ISIS kabisa
 
Huyo barozi aanze yeye kuimarisha demokrasia ubalozini kwake. Visa kupata ni longo longo. Hata uwe na sababu genuine unanyimwa tu.
Mbona wengine wanapata tu kilaini? Wewe una shida kwenye supporting docs zako! Ukweli utasemwa daima demokrasia inabakwa kisingizio cha kupamban ufisadi au maendeleo!
 
Huyo barozi aanze yeye kuimarisha demokrasia ubalozini kwake. Visa kupata ni longo longo. Hata uwe na sababu genuine unanyimwa tu.
Balozi amezungumzia Demokrasia wewe unaleta mambo ya viza. UK hawaitaji Wageni wasio na tija ndiomana wanakunyima.
 
Marekani siku zote huonekana kama mtu anayejali demokrasia,ila ukweli ni kwamba marekani ndo nchi inayongoza kwa kuvunja/kuingilia demokrasia ya nchi nyingi Dunia.
 
Kwa upande wangu sitathubutu kuamini maneno yanayotolewa na viongozi wa marekani kamwe!!!,Labda nchi hiyo iongozwe na Malaika!!
 
kwa masuala ya africa wazungu ni wanafiki wala tusiwategemee. lile lililotokea zanzibar walipaswa hata kuondoa ubalozi wao hapa bongo lakini wapi...hakuna mzungu anayelipenda taifa letu kamwe bali rasilimali zetu....
 
Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.

Bila demokrasia hakuna maendeleo. Nimesema ukweli.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom