Balozi tim clarke wa umoja wa ulaya namkubali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi tim clarke wa umoja wa ulaya namkubali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KALABASH, Dec 5, 2011.

 1. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Huyu Balozi Tim Clarke anawakilisha Umoja wa Ulaya hapa Tanzania. Umoja wa Ulaya ni mjumuiko wa watawala wetu wa zamani kabla hatujapata uhuru. Hata hivyo mwenendo wa huyu balozi hauonyeshi chembechembe za ukoloni wa wakati huo ingawa siwezi kuzungungumzia kuhusu ukoloni mambo leo. Nimekuwa nikimwona katika matukio mbali mbali na katika sehemu mbali mbali za nchi na jinsi anavyojichanganya na Watanzania wa kawaida. Leo nimemwona kwenye luninga akitoa salamu zake za miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania/Tanganyika akizungumza kiswahili kwa ufasaha na kwa kujiamini. Ananipa picha ya muwakilishi aliyeweza kuwa sehemu ya jamii anamoishi. "Give credit where it is due." Mpo wana JF?
   
 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nimemwona pia kwa luninga pia. Namfananisha na yule mama Zindonga balozi wa Zimbabwe alivyokuwa anajichanganya na jamii ya watu wa kawaida.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Uliza watu wanaofanya kazi chini yake hasa watanzania utapata picha kamili. Si vyote ving'aavyo ni dhahabu!
   
 4. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Angalizo langu kuhusu Balozi Tim Clarke limeegemea zaidi katika upande wa kisiasa na kijamii kwa ujumla. Swali la uhusiano wake na wafanyakazi wake ni mambo ya ndani. Kwa mfano Reginald Mengi anasifika sana kwa kufanya mambo mengi mazuri ya kijamii lakini ukizungumza na baadhi ya wafanya kazi wake unaweza kukuta wana mtizamo tofauti.
   
 5. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280

  Atakuwa ni mtu wa pronciple na watz walivyo wavivu watakuwa wanamchukia kufa.
   
Loading...