Balozi Ombeni Sefue hafai, lakini Kila Mtu analisifia Daraja la Kigamboni

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Watu hapa walikuwa wanasema Kwamba Balozi Ombeni Sefue ndo alipigia chapuo/alishauri Kampuni iliyojenga Daraja la Kigamboni ipewe Tenda. Nikajua wanampinga kwa sababu Kampuni haifai kumbe alituchagulia kilichobora.

China Major Bridges Engineering Company (BCEC) kwa kushirikiana na Kampuni ya China Railway Construction (CRCEG), Wamejenga Daraja la Mfano Afrika Mashariki hadi kila Mtu anasifia. Lakini Ombeni Sefue Ambaye alishauri vizuri, ameambulia Matusi na kejeli.

Mtu Mzima dawa, Ombeni atapakwa matope lakini kazi yake mtaikubali. Sasa hivi kila mtu anaenda kwenye Daraja la Kigamboni Kupiga Selfie. Basi Msifieni na Ombeni pia.
 
Mambo mengine bana si ya kuyaamini hata, tender ya daraja ilikuwa chini ya manunuzi na uwekezaji wa nssf kwa ushauri elekezi wa wizara. KMK anaingiaje kwenye maamuzi ya tender za kimataifa.
 
Mara ombeni sefue Mara Dr dau which is which .

Muwasifie sasa wanachama Wa nssf kwa maana michango yao ndo iliyotumika
 
sifa kwa JK
Ukimsifia baba yako ana mbio msifie anayemkimbiza-Jamhuri Kihwelo Julio Tantalela
 
Watu hapa walikuwa wanasema Kwamba Balozi Ombeni Sefue ndo alipigia chapuo/alishauri Kampuni iliyojenga Daraja la Kigamboni ipewe Tenda. Nikajua wanampinga kwa sababu Kampuni haifai kumbe alituchagulia kilichobora.

China Major Bridges Engineering Company (BCEC) kwa kushirikiana na Kampuni ya China Railway Construction (CRCEG), Wamejenga Daraja la Mfano Afrika Mashariki hadi kila Mtu anasifia. Lakini Ombeni Sefue Ambaye alishauri vizuri, ameambulia Matusi na kejeli.

Mtu Mzima dawa, Ombeni atapakwa matope lakini kazi yake mtaikubali. Sasa hivi kila mtu anaenda kwenye Daraja la Kigamboni Kupiga Selfie. Basi Msifieni na Ombeni pia.
Mtu anajenga daraja kwa Billioni 256 wakati gaharama halisi ni Billioni 150 halafu tumsifie??

Kwani katoa hela yake mfukoni au alitukamua vichenchi vyetu??

Huko ikulu alienda kwa kazi gani kama si kujenga mambo kama hayo??
 
Back
Top Bottom