Balozi Mpungwe: Tusijidanganye, Zanzibar kuna tatizo

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Ami Mpungwe ametahadharisha kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar, akisema “tusijidanganye kuwa hakuna matatizo” kwenye visiwa hivyo na kutaka ufumbuzi utafutwe kabla haujasababisha madhara.

Balozi Mpungwe, ambaye amefanya kazi za kidiplomasia kwa takribani miaka 25, anaungana na wanasiasa na wachambuzi ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakitoa wito wa kutaka ufumbuzi wa matatizo ya Zanzibar upatikane kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi wa marudio.

Zanzibar ipo kwenye hali tete kisiasa baada ya Tume ya Uchaguzi (ZEC) kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, ikisema sheria, kanuni na taratibu zilikiukwa na kutangaza tarehe mpya ya kupiga kura kuwa Machi 20.

Hata hivyo, vyama vingi vya upinzani vimesusia uchaguzi huo vikisema ZEC haina mamlaka ya kufuta matokeo wala kuitisha uchaguzi mwingine, na kuitaka Tume hiyo kutangaza mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25. ZEC ilifuta uchaguzi huo Oktoba 28, siku ambayo ilitakiwa kutangaza mshindi wa mbio za urais wa Zanzibar.

Ilifuta uchaguzi wakati tayari matokeo ya majimbo 31 yakiwa yameshatangazwa, huku matokeo ya majimbo tisa yakiwa yameshahakikiwa na kusubiri kutangazwa rasmi. Pia wakati huo, tayari washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani walikuwa wameshatangazwa.

Hali hiyo ilikifanya chama kikuu cha upinzani, CUF kupinga hatua hiyo ya ZEC kikisema hakikuwa na mamlaka ya kufuta matokeo kwa mujibu wa katiba na hivyo kutangaza kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio.

“Tunaweza kupretend (kujifanya) kuwa Zanzibar kuna matatizo ya kisiasa ambayo yanahitaji suluhu ya kisiasa, lakini ukweli ni kwamba pale kuna tatizo,” alisema Mpungwe ambaye ni balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini aliyepelekwa mwaka 1994 mara baada ya nchi hiyo kutangaza kuachana na siasa za kibaguzi.

“Tunaweza tukajiridhisha kuwa tunakwenda kwenye uchaguzi, lakini lazima tukubali lipo tatizo ambalo linahitaji suluhu.” Alisema tatizo lililopo visiwani humo ni la kihistoria na kuwa haliwezi kumalizwa kwa vyama vikuu vya kisiasa vya CCM na CUF pekee kuzungumza. Alisema badala yake yafaa atafutwe mtu wa tatu asiyeegemea upande wowote, akisema hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro.

Tangu kutokee machafuko ya kisiasa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, CCM na CUF ndivyo vimekuwa vikikutana kutafuta suluhisho ambalo lilipatikana baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 wakati vyama hivyo vilipokubaliana kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iliyofanya kazi kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 kulipotokea kutokubaliana. “Ukiwaachia CCM na CUF pekee, hawawezi kufikia muafaka.

Wanapaswa kutafuta mtu wa tatu ambaye atakuwa huru na atasimama katika kuleta suluhu,” alisema Mpungwe ambaye sasa anaingia kwenye bodi za taasisi mbalimbali akiwa mkurugenzi huru.

“Naamini hakuna ukomo wa mazungumzo na naamini mgogoro utatatuliwa kwa mazungumzo na amani ya Zanzibar itapatikana kwa njia hii tu. “Mimi ni muumini wa kutatua matatizo kwenye meza maana ukiondoka kwenye meza sasa uende wapi? Bado tunayo nafasi, tuwashirikishe wazee wastaafu na watu wa kada mbalimbali weledi wa masuala ya usuluhishi wakae na kutafuta suluhu katika tatizo lililopo.”

Alisema ni vibaya kufumbia macho suala la Zanzibar kana kwamba hakuna tatizo na kwamba kusema kuendelea kuamini hivyo hakutasaidia zaidi ya kuchelewesha utatuzi wa tatizo.

Alisema uamuzi wa kuunda serikali ya mseto ulikuwa wa busara ambao ulipunguza migogoro kwa kiasi kikubwa.

Chanzo: Mwananchi
 
makame silima 16/03/2016 kwa 9:05 mu · Log in to Reply
Mimi ninao mtazamo tafauti na mtoa mada juu.
Nawezakusema tatizo la Zanzibar si mgawanyiko wa wananchi wa Zanzibar kutokana na historia ya nyuma kama tunavyo fanywa na Tanganyika tuamini hivyo na wao kupata kichaka chakutugawa ili watutawale.

Tatizo hili nilakutengenezewa na hao hao Viongozi watanganyika kwa misingi ya kutumia hila za kufufua maiti wa historia ya vyama vyanyuma ,uarabu na uafrica ,upemba na unguja.

Haya yote nawezakusema yameshapitwa na wakati na ndio ukaona ccm imepigwa vibaya sana Zanzibar na kama sikutumia nguvu kubwa na mizengwe basi wasingaliambukia kitu.

Sasa leo tukisema matatizo ya Zanzibar sio ya kisiasa ni ya historia zao za wenyewe kwa wenyewe za nyuma ? Mimi sikubaliani nayo hii na wazanzibar tusikubali kugaiwa kwa misingi hii ya kufanywa mbubumbu wakuta kujua ujanja wao watanganyika wakitugawa .

Hii mbinu hii ndio silaha yao kubwa watanganyika yakitaka kitugonganisha vichwa wenyewe kwa wenyewe ili kupata mwanya wakuendelea kutugawa na kututawala na ndio weapon yao kubwa bada yakuona hivi sasa wznz wamepuza hilo na kungana ndio wamekoko moto hivi sasa kutaka kuturudisha tena kule tuliko toka kuvunja umoja wetu.

Mimi nasema wazanzibari tusikubali tusikubali tusikubali kuibomoa nyumba yetu kwa mikono yetu wenyewe huku wa Tanganyika na viongozi wao wakitumia ulahai wakusema haya ni yawazanzibar wenyewe kutokana na historia zao za nyuma huuni ujanja tu wakutugawa na kutugonganisha vicwa ili tubaguwane waendeleze ukoloni wao.

Tusisahau kua wenzetu wanaipenda nchi yao na watu wao huku sisi tukitiwa kasumba zakubomoana wenyewe kwa wenyewe.

Nanialokua hajui kua Luwassa alikuwa na umma wa watu na wafuasi walomungo mkono na uwezo wakuiondosha madarakani ccm alikua nao.

Lakini lakini waliangalia mbali kuwa Tafauti yetu na sisi ni kubwa ,wao nchi yao wanayo wenyewe na mipango yao wanapanga wenye na hata nafasi za viongozi wa upinzani chama kikuu chadema zote wamezipata na kuzidi ispokua uraisi tu lakini nafasi zote walipewa na ccm kwakuinusuru Tanganyika yao na kuwapenda watu wao wasingie vitani.

Chadema wao hawapiganii nchi yao kama sisi Zanzibar tulio tawaliwa kijeshi , wao chadema wanapo sema wanataka chenging ni madaraka tu ya uraisi kuongoza lakini hata hilo halikuwatia pressure sana ndio ukaona hawakuleta Fyoko Fyoko yakuwangiza umma barabarani na uwezo walikua nao.

Sasa vipi leo sisi tuambiwe matatizo ya ya Zanzibar ni yao wenyewe kwa historia yao ya nyuma .

Hii nikupotezwa ili tusijitambuwe na kujijia au tuwe wavivu wakufikiri? Haliyakua matatizo ya Zanzibar 99% ni yakutengenezewa na Tanganyika na watu wao ili waendelee kututawala na kuona Zanzibar ni bande lao la Ardhi lililoko beani ya Tanganyika.

Hii usultan,upemba ,unguja ni matapishi tu tunaliswa tukubali kuwa kuwa mgogo wa Zanzibar unatokana na mwenyewe?.

Wazanzibar wenye kuamini hivyo kwa sasa ni asilimia 0 niwale naweza kusema wazazibara wenye kulishwa chuku ili kwa kuona wao na systeam hii inawapatia uongozi wa kuwa vibaraka wa Tanganyika kwakuendeleza ukoloni waki Tanganyika.

Kwani nani alokua hajuwi kuwa Tatizo limekuja baada ya Kikwete kutuma Jeshi la JWTZ kuvamia kituo cha matangazo ya uchaguzi hotel ya Bwawani na kuwabeba mwenye kiti wa tume ZEC na makamo wao.

Na badae na mpaka leo kumimina jeshi Zanzibar na vifaa visito visito na kuwatesa wazanzibar na kuwaweka wananchi wa Zanzibar roha juu.

Jee hii ndio kulinda Amani au jee huu ndio Muungano? Wazanzibar tunasema unaweza kumburaza Punda mpaka mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji .

Kwa style hii hakuna Mzanzibar mwenye kuikubali ccm au Muungano munajidanganya tu Wabara kua nguvu rabda ndio zitswafanya wazanzibar wasalimu amri yagujuu.

Kwa hapa tulipofika hakuna mzanzibar mjinga munae zani anaipenda hali hii yakuteswa ndugu zao hata wawe ccm maslahi basi ni unafiki tu wa tonge lakini si wakuwamini .
 
Ninakubaliana na Ami Mpungwe,watawala wasiwe kama Mbuni.Itatugharimu siku zijazo/Wakati tunachekelea na kushehereka ati CHOTARA auawe au apigwe tu,chuki ndani mwetu zinaene.WaPemba hawako Pemba tu,hawa wanandugu kila mahali huku bara.Leo kwao kesho hatuijui.
 
Ninakubaliana na Ami Mpungwe,watawala wasiwe kama Mbuni.Itatugharimu siku zijazo/Wakati tunachekelea na kushehereka ati CHOTARA auawe au apigwe tu,chuki ndani mwetu zinaene.WaPemba hawako Pemba tu,hawa wanandugu kila mahali huku bara.Leo kwao kesho hatuijui.
Sijui Uchochezi utakusaidia nini wewe mbibi!!??? Kutwa kukicha ni Uchochezi tuuu....
 
Matatizo ya zanzibar yalitoka tanganyika .,yanatoka tanganyika na yataendelea kutoka tanganyika .hizi siasa za kudai ni za kihistoria baada ya miaka 50 kupita .utawaeleza nini vijana wanaodai usawa wa wa muungano?

Rejea ripoti ya warioba wakati wa kukusanya maoni ya katiba

Vijana wengi wa zanzibar walitaka muungano wa serekali tatu

Mada ya napinduzi kwa vihana wa zanzibar ilishahama na kuhamia kwenye muungano wa kinyonyaji .

Tatizo kubwa sana kuliko lote kwa wakati huu ni dharau kwa zanzibar (under the umbrela of what so called amiri jeshi mkuu
 
Muafaka umepatikana siku nyingi Zanzibar. Wanzazibari wamoja, we are a people. Kinachoendela Zanzibar ni fyoko fyoko za kutugawa zinazoendelezwa na Watanganyika wachache wanaomiliki dola kwa masilahi yao wenyewe. Maendeleo ya Zanzibar chini ya mwavuli wa Serikali mbili ni ndoto ya mchana. Nothing grows under the shadow of a big tree. Huo ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom