comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,939
Mbunge wa siku nyingi na mwanasiasa nguli nchini Mh Mama Getrude Mongela amesema vijana wa miaka hii wamevunja tamaduni na mila kiasi cha kuibuka kwa wimbi la kubaka,
Zamani ungeonekana kituko ukisikika umebaka huwezi kusikia mtu amebaka kwani wanaume wa zamani walikua na maneno matamu ya kuwaeleza wasichana na kupatana kuliko miaka hii' hali ya miaka hii kwa vijana hawajui kutongoza ndio inapelekea kuwabaka wasichana hivyo ameshauri vijana watumie busara na maneno matamu ili wapatane kuliko kubakana na kupunguza ongezeko la magonjwa na kesi nyingi za ubakaji nchini, hivyo amerejea kauli kwamba vijana waingie darasani wakafundwe kutongoza kwa busara