Balozi Ibrahim Kaduma amrushia Kombora JK, CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Ibrahim Kaduma amrushia Kombora JK, CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by msafi, May 23, 2011.

 1. m

  msafi Senior Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Balozi Ibrahim Kaduma, ambaye alikuwa waziri katika serikali ya awamu ya kwanza ya mwalimu J.K Nyerere ametilia shaka utekelezaji wa mkakati wa kujivua gamba kwa madai kuwa CCM na mwenyekiti wake, raisi Jakaya Kikwete hawako makini kwa sababu wameshindwa kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kukivuruga chama. Alisema mkakati wa CCM wa kujivua gamba utafanikiwa endapo kikwete na chama chake watakwa na dhamira ya kweli. "kujivua gamaba kwa ccm kutawezekana kama wakiwa `serious`(makini). kwa sababu wakati wetu hakuna mtu aliyeshutumiwa akabaki kwenye kamati kuu ya chama" alisema kaduma na kuongeza, "kama raisi ana msimamo huo awatoe kwenye chama wanaotuhumiwa. kwa nini awaseme tu au anataka wajiondoe wenyewe? anasema mawaziri wana harufu ya wizi lakini wamo kwenye baraza, kwa nini asiwatoe?"
  Huku akitaja sifa za kiongozi bora, kaduma alisisitiza kuwa kutokana na kukosekana kwa maadili kwa sasa, taifa limekosa mwelekeo. "mpaka sasa hatuko kwenye `right truck`, kwa sababu tumeshapoteza maadili.
  Akizungumzia kuanguka kwa azimio la arusha na kuingia azimio la zanzbar, alisema hali hiyo ilisababishwa na ubinafsi wa viongozi wenye tamaa ya mali.
  "Ufisadi ni zao la ubinafsi, waloshindwa azimio la arusha walikuwa wabinafsi. mtu kama huwezi kufanya kazi uondoke serikalini, kwani hatukulipi mshahara hata ukishindwa kututumikia(wananchi)?" alihoji.
  Akikumbuka uongozi wa mwalimu nyerere, balozi kaduma alisema, raisi huyo wa kwanza Tanzania, alifanya viongozi waaminike katika jamii kwa sababu alikuwa mkali. "Mwalimu alikuwa strict. aliwahi kutoa mfano wa mke wa kaisari (Cesar) ambaye alipewa talaka kwa kututhumiwa tu. mke wa kaisari hakupaswa kutuhumiwa, alisema kaduma.
  "Wakati ule ukifanya kosa unajondoa mwenyewe, maana ukingoja (Nyerere) atakufukuza tu. Ndiyo maana enzi za Mwinyi wafungwa walipokufa shinyanga, alijiuzuru. Jenerali Natepe pia aljiuzuru kwa matatizo yaliyotokea gereza la ukonga"


  Source: Mwananchi Jumapili Mei 22 2011
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Haya wazee wanajirudia tu kiyasema haya sie tulisha sema zamani sasa huyu nae watamshukia sijui watamwita nani magamba au ngozi
   
Loading...