Balozi Dkt. Slaa atoa somo

Balozi Dkt. Slaa atoa somo

Dr kasoma ulaya, kaishi ulaya muda mrefu nadhani kuliko kiongozi yeyote pale Chadema; nina hakika hiki anacho kisema sasa hivi sio kwamba kajifunza kwasababu ya kazi yake ya ubalozi aliyonayo sasa, mfano ni huo wa Gwantanamo alioutolea, Gwantanamo ilishika kasi Zaidi kipindi akiwa active nationalist in this country kuliko sasa, Gwantanamo ya sasa sio ile ya Enzi za Bush Jr na Obama, GWantanamo ya sasa iko poa kidogo kuliko ile so aliijua vizuri sana those days wakati anatuhutubia aliokua akihutubia. Anyway, labda swali tu kwake; Hivi Gwantanamo ilikua inatesa Wamarekani eti eeh? Jibu ni No, ilikua inatesa raia wa nchi zingine na sio MArekani kutesa raia wake mwenyewe so mfano wake haufanani, alete mwingine.
 
Jana nimeona video za Dkt Slaa kwenye social media ambazo alihojiwa na wanahabari baada ya mkutano wa viongozi wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam Tanzania. Dkt Slaa kwenye video hizo amezungumza mambo mbalimbali hususani mambo ya kiuchumi na mambo ya kisiasa ambayo msingi wake mkubwa ni UZALENDO.

Sijajua wewe mwenzangu umejifunza nini juu ya maneno yale ya Balozi. Funzo kubwa ambalo mimi nimejifunza ni kuwa Watanzania wengi wanaamini Wazungu ni wazalendo kwetu kitu ambacho si sahihi. Ukisikiliza kwa umakini Dkt anasema yanayofanyika huku Afrika huko Ulaya yanafanyika mara dufu. Na amesisitiza pamoja na kwamba wao nchi zao zipo katika Dunia ya kwanza bado kuna takataka nyingi za uvunjifu wa haki za kibinadamu huku akitolea mfano Gwantanamo.


Dkt amejaribu kutoa elimu kuwa kunapokuwa na mambo ya ndani ya nchi basi yazungumzwe ndani ya nchi. Kama ni kuchapana fimbo tuchapane humu humu na kamwe tusitoe mambo yetu nje. Amesema kutoa mambo yenu nje ni kuruhusu mianya ya kuwapenyeza watu wanaozitamani rasilimali zetu kwa ajili ya nchi zao.

Kubwa kuliko yote pamoja na kuwa msingi wa Dkt Slaa alijikita kuwaambia Watanzania kuwa wawe wazalendo, lakini alikuwa anafikisha ujumbe kuwa vita ya uchumi kwa dunia ya leo ndiyo ngumu kuliko vita yoyote.

Tunatambua kuwa ili nchi zilizoendelea ziendelee kuwa na viwanda imara, masoko ya bidhaa zao, malighafi kwa ajili ya viwanda vyao na miundo mbinu bora katika nchi zao waitegemea zaidi afrika. Bidhaa nyingi tunazoenda kununua ulaya na kuziingiza kwenye masoko yetu ni wazi kuwa mali ghafi zimetoka huku huku afrika. Hivyo wanapojitokeza viongozi ambao wanataka malighafi hizi zichakatwe hapa hapa na kutolewa nje zikiwa zimeongezwa thamani basi ujue unajitengenezea maadui ambao walikuwa wakitegemea malighafi hizi.

Mh Rais tangu hotuba yake ya kufungua Bunge alishaonyesha dhamira yake ya dhati katika kulinda uchumi wa Tanzania na kufufua viwanda. Matokeo ya kukusanya mapato na kubana matumizi tunaona matokeo yake. Mambo makubwa yanafanyika hapa nchini katika kipindi chake na bado ameendelea kusisitiza kuwekeza kwenye viwanda na kulinda rasilimali zetu hasa madini, misitu, Wanyama n.k. Kufanya hivyo tayari amejitengenezea maadui wa ndani na nje waliokuwa wanatumia mianya hiyo kujinufaisha.

Wanasiasa na wanaharakati wanaodhani wazazi wao ni wazungu, wanaodhani kunapotokea matatizo hapa nchini basi baba na mama zao ni wazungu wa kwenda kusemelea watambue kuwa wanawatengenezea maisha magumu watoto wao na wajukuu zao. Hawa wazungu ambao waligawana bara letu tangu 1884 baada ya mkutano wa Bern ndio waliotufikisha hapa. Hawana nia njema na sisi. Hawa ndio waliwaua ndugu zetu kwa kuwachinja, kuwachapa, kuwafunga minyororo, kuwatosa baharini na kuwafanyisha kazi ngumu(manamba). Ni matatizo ya akili kama tunaona watu waliotusababishia wimbi hili la umasikini kuwa leo wanaweza kutusaidia.

Wanachofanya kama ilivyokuwa zamani akikupa 2 ujue amechukua 100. Historia inatukumbusha kuwa walikuwa wanachukua madini yetu na kuwaletea babu zetu nguo, sigara, bangili au saa. Hivyo hata leo wanafanya hivyo ijapo si rahisi kwa kuwa ukoloni wa sasa umeboreshwa na Waafrika wenye akili nao wameungana nao kama ilivyokuwa kwa akina Karl Peters, Livingston na akina Henury Morton.

Mwandishi Okot P'Bitek kwenye kitabu cha Song of Lawino and Song of Ocol anaandika "Dont uproot pumpkins in the old homestead". Waafrika wengi tunadharau vya kwetu na kuamini vya Wazungu. JPM amekuja muda mwafaka, tumuunge mkono. Kama ni kumkosoa basi tutumie lugha zetu na utamaduni wetu wa ndani kukosoa kwani hata yeye si malaika. Ulaya hawatawasaidia zaidi mnawatafutia njia ya kutunyonya zaidi.

Mambo mengine ya Diplomasia ya kimataifa tuwaachie Ambassadors na Consular agent(Wanadiplomasia ya uchumi) waendelee nayo huko.

Nakumbuka ule usemi wake akiwa Chadema,kwamba "nchi haita tawalika",madaraka raha sana.
 
hakuna cha kujifunza kutoka kwa wanafiki.

Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi inazuiliwa na wazungu??
Mlipewa fursa ya kupata katiba mpya mkaichezea,mlibishana hata kuweka nukta tu kwenye vifungu vya katiba
Sasa ajenda ni viwanda labda aje rais mwingine
 
Kuendelea kutegemea Wazee tukizani kwamba wanaweza kulisogeza taifa mbele ni weu
 
Mlipewa fursa ya kupata katiba mpya mkaichezea,mlibishana hata kuweka nukta tu kwenye vifungu vya katiba
Sasa ajenda ni viwanda labda aje rais mwingine
Yes viwanda vya akina Azory Gwanda, Ben Saanane, Mawazo nk.
 
Uzuri Dr slaa anayo majibu kuwa wengi wa upinzani tatizo ni upeo.sina uhakika mnaona waafrika wanavyouliwa marekani na.haki haitendeki.kwa darasa la bure nazo hizo ni haki za binadamu zinatakiwa zichukuliwe sawa na zinavyivunjwa huku kwetu kwa homework yako nenda kagoogle kama kifurushi hakijakata jinsi ukaya inavyoratibu issue ya wahamiaji ambao ndo wanachama wa EU zote ziko kwenye misingi ya haki za binadamu sawa sawa na ushoga ukiridhika njoo na essaey usijali format we jikunje ilimradi inasoneka.
Unachoongea ni kweli kabisa..Marikali watu weusi wanavunjiwa HAKI ZAO za KIBINADAMU kama hapa Tanzania kwetu ..ila kwa kiasi kikubwa wanaofanya hivyo wanakamatwa hata kama ni watumishi wa Vyombo vya Usalama na kushtakiwa na hatua kuchukuliwa. Labda katofauti kadogo kwetu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa yakitokea kama ya Marekani..tunauwana na kutekana bila kuhojiana kabisa. Nauhakika hilo tutarekebisha hasa kwa wapinzani wetu..
 
Slaa hana kitu ni mnafiki mkubwa. Ni mtu wa kupuuzwa tu. Tangu lini ameona ccm inafaa. He is very bogus.
 
Slaa hana kitu ni mnafiki mkubwa. Ni mtu wa kupuuzwa tu. Tangu lini ameona ccm inafaa. He is very bogus.

Mkuu umeandika utadhani umekasirishwa. Vipi Dkt Slaa anaweza kuwa sababu ya kuwakosesha safari ya matumaini 2015?
 
Huyu mzee tumunee huruma mpaka ananunuliwa na ccm Nyumba yake ya bweni ilikuwa imeshauzwa na bank Sasa asipofanya kazi ya kusema uongo nyuma na kula atapata wapi?
 
Hivi hili lijamaa si lilienda Marekani kisa tu alinyimwa kugombea urais. Msikilizeni mie nishapunguza volume
 
Huyu mzee tumunee huruma mpaka ananunuliwa na ccm Nyumba yake ya bweni ilikuwa imeshauzwa na bank Sasa asipofanya kazi ya kusema uongo nyuma na kula atapata wapi?


Jaribu kupata utulivu, ili uweze kuandika vizuri.
 
Back
Top Bottom