Mario Balloteli jana alifunga bao moja na kuisaidia AC Milan kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Siena.Bao lingine la Milan liliwekwa kimiani na Mexes aliyeunganisha krosi ya Montolivo. Mabao ya Milan yalipatikana katika dakika za lala salama za 84 na 86. Hadi dakika ya 83,Milan ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 huku ikihitajika kushinda mechi hiyo ya mwisho ya Serie A.Kwa ushindi huo,Milan imetinga UEFA Champions League ikianzia kwenye mzunguko. Pamoja na Fiorentina kushinda kwa 5-1,bado imezidiwa pointi 2 na Milan. Hongera sana AC Milan,najivunia kuwa shabiki wa timu hiyo. Nakala apewe: Gang Chomba
gang Bang Gang Chomba ameipokea nakala hiyo kwa furaha sana.
Alikuwa anaiangalia mechi hiyo huku akiwa na wasiwasi mkubwa haswa muda ulivyokuwa unayoyoma na AC Milan wakawa nyuma.
gang Bang Gang Chomba ameipokea nakala hiyo kwa furaha sana.
Alikuwa anaiangalia mechi hiyo huku akiwa na wasiwasi mkubwa haswa muda ulivyokuwa unayoyoma na AC Milan wakawa nyuma.
Mkuu Gang Chomba,hunizidi mimi. Mwenzako ilipofika dakika ya 83,nikazima ka-TV kangu na kujilalia. Nililala moyo ukiuma.Lakini,nikaamka tena dakika ya 89 na kuyakuta maajabu ya AC Milan. Hadi sasa siamini