BAKWATA yawataka Maimamu na Mashehe katika misikiti kuliombea Taifa kuliepusha na baa la njaa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Baraza kuu la waislam Tanzania BAKWATA limewataka Maimamu na Mashehe katika misikiti kuwaongoza waislamu nchini kuliombea dua taifa kupata mvua pamoja na kuondoa ukame na baa la njaa lililolikumba taifa.

Chanzo: ITV

15966230_1092510434193263_4330184903309654484_n.jpg
 
Hao nao watakuwa wamelipwa na wafanyabiashara watangaze njaa !
 
Unaona Viongozi wa Dini Nchi hii? Aliyesema hakuna Njaa hamwambii kitu, aliesema kuna njaa nani?

Mwenyewe kasema hakuna njaa, na kasema kuna Magazeti mawili yanachochea yamenunuliwa na wafanyabiashara yaandike njaa, Dawa yao inachemka, sasa Kama hamuwezi kumwambia je na sisi tukiomba Mungu atuepushie na Njaa na ukame akitushughulikia itakuwaje?

Ombeni wenyewe tumechoka kutukanwa.

Viongozi waoga Kama nini, ndio ubaya wa kushabikia chama huku ukiwa kiongozi wa Dini
 
Naona hao BAKWATA hawajipendi kabisa.
Rais ameshasema Tanzania hakuna njaa, Nchi ni yakijani kabisa(akimaanisha mvua zimenyesha kwa wingi), sasa nani mwingine anajua zaidi ya rais wetu? Hao BAKWATA wamenunuliwa na nani tena?
Rais wetu anajua kila kitu kuhusu Tanzania kuliko mtu yoyote yule.

Mimi nasubiri kuona rais akithitisha ule msaada wa kuwajengea lile jengo kubwa pale Dar hao BAKWATA na ikiwezekana hata mle msikiti mkubwa unatakiwa kujengwa kwa pesa za msaada wa Mfalme wa Morocco usijengwe kabisa.

Rais wetu hapendagi watovu wa nidhamu, BAKWATA wanamjaribu mtukufu mtukufu mtukufu Magufuli.
 
Back
Top Bottom