BAKWATA yakerwa na lugha za matusi

BAKWATA yakerwa na lugha za matusi

Arusha Leo

Senior Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
120
Reaction score
72
BARAZA la waislamu {Bakwata}wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wamewaonya wanasiasa kuacha kutumika kutoa matamkoa anayoweza kuleta machafuko nchini.

Kiongozi wa Bakwata wilayani humo,Sheikh Haruna Husen alitoa Tamko hilo mbele ya viongozi wa dini hiyo katika msikiti wa mji Mwema ,Usa River wilayani humo.

Maneno yaliyotamkwa na viongozi hao wa dini yalionyesha wazi kumlenga aliyekuwa katibu mkuu wa chadema Taifa dkt. Willbroad Slaa,ambaye hivi karibuni alitikisa kwenye vyombo vya habari kwa kumsakama waziri mkuu aliyejihudhulu ,Edward Lowasa.
Viongozi hao wa dini ya kiislamu wamechukizwa na kauli ya maaskofu kudaiwa kuhongwa ili wamuunge mkoano mgombea wa urais kupitia Ukawa Edward Lowasa.

Pia baraza hilo lilitaka wanasiasa hao wasiwagawe wananchi kwa kauli zao ,bali watamke watawafanyia nini kuwaondoa kwenye umasikini.


==================================
Bakwata-5Aug2015.jpg

Viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, wamekemea wagombea wa vyama vya siasa wanaotumia lugha za kashfa katika kampeni hali inayoweza kutishia uvunjifu wa amani.

Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Arumeru, Ustadhi Haruna Hussein alisema, wanasiasa hao wanachopaswa kufanya ni kunadi sera na sio kutukanana kwenye majukwaa hali ambayo inaashiria kuwapo kwa uvunjifu wa amani kutokana na mienendo yao.

Aidha aliwataka wanasiasa hao kunadi sera zao kwa wananchi kuwa watawafanyia mambo gani pindi watakapochaguliwa badala ya kusimama kwenye majukwaa na kuanza kutoa lugha za kashfa na matusi kitendo kinachochagia wananchi kukosa imani nao.

Alisema viongozi hao ni kioo kwa jamii hivyo wanapaswa kuonyesha dira ya uongozi na sio kuwa na matusi na kashfa.

Naye mjumbe wa Bakwata Wilaya ya Arumeru, na Kaimu Sheikh wa Msikiti wa Patandi, Ally Ramadhani Haji, alisema madhara ya kutaja mambo ya aibu za watu majukwaani ni kutengeneza chuki zisizokuwa na maana, kwa sababu dunia inapita kwenye kipindi kigumu na moja ya mambo yanayosababisha chuki na vurugu ni siasa za chuki baina ya viongozi ambapo mwisho wa siku watu wanaingia kwenye matatizo.

Kwa upande wake, Sheikh wa Wilaya ya Arumeru, Ally Isa Ibrahimu alisema, viongozi hawatakiwi kufarakana na kutukanana pamoja na kuchafuana kwenye kampeni bali wawe wamoja katika mambo yao huku wakizungumzia suala zima la amani ya nchi ili kufanyika kwa kampeni za kistaarabu.

Alisema katika kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi vyama vya siasa pamoja na viongozi wa siasa wanapaswa kutangaza amani ya nchi, kwani jamii haipo tayari kuona viongozi hao wa kisiasa wakifanya kampeni chafu zinazochangia viasharia vya amani.

Sheikh wa Msikiti wa Patandi, Abdalah Said Omar alisema, kwa ujumla baraza hilo wilayani Arumeru halifurahishwi na siasa chafu zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa ikiwamo kutoleana lugha za matusi hatua ambayo inaipeleka nchi pabaya hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanazungumza maneno mazuri yenye kuiletea nchi amani.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom