Bakwata waunga mkono katiba ya wananchi

Bakwata waunga mkono katiba ya wananchi

crabat

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
4,323
Reaction score
2,210
Baraza kuu la waislam limesema lina unga mkono katiba ya wananchi iliyo tokana na maoni ya wananchi ikiwa pamoja na mabadiliko katika mfumo wa muungano ili kuleta umoja na kuumarisha uchumi wa pande zote za jamhuri.
Source:startv tbc habari
 
Baraza kuu lipi hilo? wakati leo hii pale MWEMBE YANGA alikuwepo Shehk Mkuu wa Mkoa wa
Dar Es Salaam akiungana na CCM juu ya hoja yao ya Serikali 2 na inawezekana kabisa alikuwa anaiwakilisha BAKWATA.
 
Safi Sana bado wakiristu watoe tamko kwa sababu ccm wanataka kutuletea katiba yao wanayo itaka wao
 
Safi sana waislamu! CCM inatkiwa kujua katiba inayohitajika siyo ya ccm bali ni ya Watanzania.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kama ni kweli wamefanya jambo jema! Maana maamuzi yote yanatoka kwa umma!
 
Baraza kuu la waislam limesema lina unga mkono katiba ya wananchi iliyo tokana na maoni ya wananchi ikiwa pamoja na mabadiliko katika mfumo wa muungano ili kuleta umoja na kuumarisha uchumi wa pande zote za jamhuri.
Source:startv tbc habari
Acha upotoshaji, BAKWATA wameunga mkono hotuba ya Rais, sasa usije ukaleta mambo ya serikali ngapi hapa.
Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Bakwata hawana jeuri wala uwezo wa kwenda kinyume na serikali ya ccm wewe HAMKA
 
Ile ndege ya malaysia iliyobeba watu 239..wasio na hatia wakapotea.Bora ingewabeba wajumbe(wabunge) wa katiba ikapotea nao kuliko vitu wanavyofanya Bungeni.
 
Nimeangalia taarifa ya TBC, wamesema Bakwata wanaunga mkono hotuba ya JK ambayo kimsingi inasisitiza serikali 2
 
Ile ndege ya malaysia iliyobeba watu 239..wasio na hatia wakapotea.Bora ingewabeba wajumbe(wabunge) wa katiba ikapotea nao kuliko vitu wanavyofanya Bungeni.

Kwa hiyo ulitaka mbowe. zitto. lema. tundu. mdee. mnyika. kingunge. sitta. magufuli wafe na tufanye uchaguzi mwingine?
 
Ile ndege ya malaysia iliyobeba watu 239..wasio na hatia wakapotea.Bora ingewabeba wajumbe(wabunge) wa katiba ikapotea nao kuliko vitu wanavyofanya Bungeni.

Ha ha ha ha nimecheka sana!punguza hasira mkuu japo yanayofanyika huko ni maigizo!kuna kundi la watu fulani wanacheza na muda kauli yangu siku zote wakati wa kupata katiba mpya ukifika hakuna mwenye nguvu ya kuzuia hii ya sasa ni ya watu fulani siyo yenyewe!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ile ndege ya malaysia iliyobeba watu 239..wasio na hatia wakapotea.Bora ingewabeba wajumbe(wabunge) wa katiba ikapotea nao kuliko vitu wanavyofanya Bungeni.

NI KWELI MKUUUUUUU.
 
Baraza kuu la waislam limesema lina unga mkono katiba ya wananchi iliyo tokana na maoni ya wananchi ikiwa pamoja na mabadiliko katika mfumo wa muungano ili kuleta umoja na kuumarisha uchumi wa pande zote za jamhuri.
Source:startv tbc habari

Acha uzushi, Bakwata Hawana ujinga huo
 
Acha upotoshaji, BAKWATA wameunga mkono hotuba ya Rais, sasa usije ukaleta mambo ya serikali ngapi hapa.
Akili za kuambiwa changanya na zako.

walio unga mkono maoni ya ccm ni bakwaccm na sio bakwata.
 
Acha uzushi, Bakwata Hawana ujinga huo

hujaeleweka me kima ujinga ni bakwata kuunga mkono wananchi au???fafanua basi maana naona akili yako inashindwa kufikiri vizuri.
 
Back
Top Bottom