BAKWATA nielimisheni kuhusu ndoa ya Kiislam

BAKWATA nielimisheni kuhusu ndoa ya Kiislam

Majimengi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
499
Reaction score
197
Naomba kuelimishwa, kuhusu kanuni na taratibu, za ndoa ya kiislaam, kuanzia uchumba, maisha ndani ya ndoa, mpaka kufikia kutengana,au kuachana (ikibidi).
 
Kwanza naomba nirekebishe kichwa cha habari hapo juu katika mada tajwa nadhani ingekuwa vema au ukaboresha zaidi kwa kuandika 'NAOMBA NIELIMISHWE JUU YA NDOA ZA KIISLAMU NA WANAZUONI WA KIISLAM' ingekaa poa zaidi kutoa uwanja mpana kwani UISLAM NI ZAIDI YA BAKWATA
Ama baada ya maoni hayo swali lako ni pana kidogo hivyo Bi idhnillaah utajibiwa kipengele kwa kipengele kuanzia
1. Uchumba nkwa mujibu wa uislam
2. Ndoa za kiislam
3. Haki za mume kwa mke kwa mujibu wa uislam
4. Haki za mke kwa mume kwa mujibu wa
uislam
5. Maisha ya namna gani kuishi na mke kwa mujibu wa uislam
6. Migogoro itatuliwe vipi kwa mujibu wa uislam
7. Talaka kwa mujibu wa uislam
8. Kukaa eda kwa mwanamke aliepata talaka 1, 2 na 3
Nitajitahidi na kukujibu kwa nilichojaaliwa lakini hii ni fursa kwa masheikh/wanazuoni/maulamaa kutoa darsa zuri na kufuta fikra potofu zilizojengwa kwa watu kuwa uislam unamkandamiza mwanamke
Hakika MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI
 
1. SOMO: UCHUMBA
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Maana ya uchumba katika Uislamu.

Uchumba katika Uislamu ni pale mwanamme anayetaka kuoa au jamaa zake au mtu yeyote aliyemwakilisha anapokwenda kwa wazazi au walezi wa msichana kuposa na kukubaliwa.

Huo ndio unaitwa uchumba kinyume na hivyo unakuwa ni urafiki baina ya mvulana na msichana. Na hili limekatazwa kishari’ah.
Na hata baada ya mvulana kupeleka posa rasmi kwa wazazi wa msichana, hao wawili hawajaruhusiwa kishari’ah kutembea pamoja, kukutana au hata kuwasiliana bila ya dharura
Ama kuhusu sifa njema na nzuri ambazo kwayo mwanamme anafaa achague mkewe na mwanamke naye achague mumewe ni kama zifuatazo kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu:

Kuchagua kwa msingi wa Dini:

Huu ni msingi wa kwanza na muhimu sana. Ukweli ni kuwa kila mmoja ana sifa ambayo anaona lau atapata mwendani wake basi ashafika kwenye kilele katika maisha yake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye ametuelezea pale aliposema:“Mwanamke huolewa kwa sababu NNE: Kwa mali yake, nasaba yake, uzuri wake na Dini yake, Tafuta mwenye dini uwe salama (yaani usiharibikiwe katika maisha yako)”(al-Bukhaariy na Muslim).
Amesema tena: “Akikujieni ambaye mumeridhika na dini na maadili yake, muozesheni. Msipofanya hivyo kutakuwa na fitna katika ardhi na ufisadi mkubwa” (at-Tirmidhiy).

Allaah SW anajua zaidi

Nadhani kipengele hiki utakuwa umekielewa zaidi. Lakini wanaojua zaidi waweza kuongezea au kupunguza au kunisahihisha
 
2. SOMO: NDOA KATIKA UISLAM
Utangulizi.
Qur’an 30:21
“Na katika lama zake amewaumbieni wake kutokana na nyinyi wenyewe ili muishi kwa utulivu nao, na akawatia upendo na rehema kati ya nyoyo zenu. Kwa hakika katika haya ni ishara kwa wenye kufikiri”

Qur’an 16:72

“ Na Allaah amekuumbieni anaetokana na asili yenu na kwa ajili yenu, kutoka kwao watoto wa kiume na wakike na wajukuu na kuwapeni rizki njema”.

Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) amesema:
“Enyi vijana, aliye na uwezo wa kuoa aoe, kufanya hivyo kutamsaidia kuinamisha macho yake chini na kuwa mtii. Na utii ni sehemu ya imani”. (Bukhari).
Na katika hadithi nyingine pia amesema:

“Ndoa ni katika mienendo yangu na atakayekwenda kinyume na hivyo hatakuwa nami” (Bukhari).

Katika aya zilizotangulia Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wata’ala) anatwambia kuwa ameumba waume na wake ili waishi pamoja kwa mapenzi. Wazae watoto na kuishi kwa amani na utulivu na kwa njia hiyo wataweza kutii amri zake na kufuata mafundisho ya Mtume wake.

Kwa ufupi ndoa katika uislamu ni:

1. Njia mojawapo ya ibada. Mnapokuwa katika ndoa mnakuwa mpo katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa mtume saw wake.

2. Kujenga uhusiano wa familia na makundi (jamii).
3. Ni kitendo cha uchaji Mungu.
4. Njia halali ya kuzaliana.
5. Mojawapo ya suluhisho la kuondoa kuchanganyikiwa.

JE NDOA NI LAZIMA?

Imamu Abu Hanifa, Ahmadbin Hanbal na Malik wanasema ingawa asili yake inaonekana ni jambo lisilokuwa la lazima lakini kwa baadhi ya watu linakuwa ni lazima (wajibu).
Imamu Shaafi anasema ni jambo lenye kupendeza (Mubah).

Imeripotiwa na bukhari na wengineo kwamba watu watatu walienda kwa wake za mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) na kuwauliza vipi mtume afanyavyo ibada zake. Walivyoelezwa wakaona inabidi wao wafanye zaidi ya vile alivyokuwa akifanya mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) kwa kuona kuwa kunatofauti kubwa sana kati yao na mtume kiibada japo yeye ni mtu ambaye amesamehewa madhambi yake yote ya nyuma na ya mbeleni. Mmoja wao akasema ataswali usiku daima. Mwingine akasema hatoshughulika na habari za wanawake na hivyo hatooa. Na wa mwisho akasema atafunga daima. Mtume aliposikia habari zao akasema:

“Mimi ni mcha Mungu zaidi yenu, pamoja na hayo ninafunga na kufungua, nina sali na kulala na nina oa. Yule atakaye kwenda kinyume hatakuwa pamoja nami”.

Wanachuoni wamefikia makubaliano kuwa ndoa ni lazima kwa muislamu mwenye uwezo wa kumuhudumia mke. Allaah sw ameahidi kuwasaidia wale wenye kuoa kwaajili ya kujikinga pale aliposema:

“Waozesheni miongoni mwenu wale walio wajane na wema miongoni mwa wajakazi wenu waume au wake iwapo masikini, Allah atawatajirisha kutokana kmknhazina zake”. (24:32).

Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) amesema:

“Kuna aina tatu za wenye haki ya msaada wa Allah, mwenye kuoa kutaka aishi maisha mema, mtumwa ambae bwana wake amekubali kununua uhuru wake atakapo kuwa tayari kulipa na mwenye kupigana katika njia ya Allah”. (Ahmad, An-Nisai, Attirmidhiy, Ibn Majah na al-Hakim).

WANAWAKE WASIO RUHUSIWA KUWAOA

1- Mke wa baba, awe ameachwa au kafiliwa na baba.
2- Mama, wakiwemo mabibi wa pande zote.
3- Binti, wakiwemo wajukuu wa kike kutokana na watoto wako wa kike au wa kiume.
4- Dada, akiwemo wa baba au mama mmoja.
5- Shangazi kwa baba, au mama mmoja na baba.
6- Binti wa kaka.
7- Binti wa dada.
8- Mama aliyekunyonyesha.
9- Mabinti wa mama aliyekunyonyesha.
10- Mkwe wako wa kike (mama wa mke).
11- Ndugu wawili wa kike kuwaoa wakati mmoja.
12- Mwanamke mshirikina (anayeabudu masanamu).
13- Kahaba
Inaelezwa kuwa Murtaid ibn Murtaid alimuomba Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) amuoe mwanamke aitwae Anaq ambae alikuwa na uhusiano naye kabla ya uislam. Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) hakumjibu mpaka aya ikashuka isemayo:

“Mzinifu mwanamume hatooa ila mzinifu mwanamke au mshirikina mwanamke na mzinifu mwanamke hatoolewa na yoyote ila na mzinifu mwanamume au mshirikina mwanaume. Na kuwaoa hawa ni haramu kwa muumini.”

Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) akamsomea Murtaid hiyo aya na kumwambia asimuoe (Abu Daaud, an-Nisai na Tirmidhiy).

KUCHUMBIA

- Hairuhusiwi kumposa mwanamke alie katika eda ya kuachwa au kufiwa na mume kwani wakati huu huhesabiwa ni sehemu ya ndoa yake mwanamke.

- Hairuhusiwi kumposa mwanamke ambaye anajulikana kuwa amekwishaposwa na mtu mwingine.

Katika hadithi iliyopokelewa na Muslim, Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) anasema:

“Muumini ni ndugu wa muumini mwingine. Kwa hivyo hairuhusiwi kwake kumpiku ndugu yake katika kununua kitu au kutoa posa kwa mwanamke wakati anapokuwa ndugu yake ameshaposa, ila awe amempa ruhusa”.

KUMUONA MCHUMBA UNAETAKA KUMUOA

Ina ruhusiwa kumuona mchumba kwa sababu wanaosema jicho ni mtumishi wa moyo. Na macho yatakapoonana na kukutana na nyoyo za mume na mke zinaweza zikakutana.

Al-Mughirah ibn Shui’bah amesema:

“Nilitaka kumuoa mwanamke, mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) akaniuliza kama nimemwangalia nikamjibu bado akaniambia nikamwangalie kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta mapenzi kati yetu. Nikaenda kwa wazazi wake na kuwajulisha ushauri wa mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) wakawa wamesita juu ya hilo. Binti yao akasikia maongezi akasema: ‘iwapo mtume amesema uniangalie basi niangalie’. Nikamwangalia na hatimae nikamuoa”.(Ahmad, al-Tilmidh, ibn Majah, ibn Hakim).

NIKAHA

Mambo yatakikanayo kutimia ili ndoa ikamilike kufungwa.

1. Mlezi: Baba au mwakilishi wake wa kutoa idhini.
2. Mahari (Qur’an 4:4):

“Wapeni wanawake mahari yao…”.

3. Muoaji na Muolewaji.
4. Kauli ya kuozesha na kukubali.
5. Mashahidi wawili.

HAKIKA MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI
 
Habari zenu
Kutokana na ndugu yangu hapo juu uzeebusara kaweka vipengele kwenye ndoa ya kiislam , nitajitahidi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kuvifafanua, na yeye mwenyewe akirudi atatuelimisha zaidi.
Mimi sio mwalimu ila nitaelezea kwa Mujibu wa nilivyofundishwa.
1. Uchumba kwa Mujibu wa uislam.
Kwenye uislam mtoto wa kiume kwanza huchaguliwa mke na wazee wake au pia anaweza kuchagua mwenyewe.
Sasa baada ya kuona binti fulani atanifaa, huswali kumuomba Mungu kwanza, hii swala inaitwa swalatul Istighaar, ni rakaa mbili, Kisha hhuwaambia wazee wake wende wakapelekee posa kwA wazee kuhusu Jambo lake Hilo, hapo wazee tena wanawezaa kuwafikiana au msiafikiane kwa sababu Tofauti.
Maana mwanamke huolewa kwa mambo manne
Dini yake, uzuri wake, nasabu yake na cheo chake, lakini lilolo Bora katika yote ni dini yake, (mchague mwenye dini)
Tuchukulie mmeafikiana, sasa ndio wazee huendaa kwa wazee wa mwanamke kwa ajili ya kukuposeaa.
Kuna kuwa kuna muda maalum wazee hupeana, sasa hapo wazee wa kike humpeleleza mwanamme anaetaka kumuoa mtoto wao na familia pia huangaliwa, lkn haswamwanamme mwenyewe muhusika ndio hutizamwa zaidi.
Jee Ana dini, tabia zake nzuri, atamueza mke n.k.
Yakisha kukaa sawa pande zote mbili, sasa wanaume wanakuja kuchukua jibu kuwa wamekubaliwa. Na kupanga kukutana tena kwa ajili ya makati na ya kupanga harusi.
Sasa kwenye kipindi hichi hakuna kutembeleana mwanamme na mwanamme kwa mujibu wa taratibu za dini. Kama kuna jambo ni kuenda kwao kuzungumza mbele ya mahram wake (baba ake, Kaka, ami, mjomba) yoyote katika hao,sio siri wewe na yeye tuu, au kutoka nae hayo hayapo kabisakutokana na sheria za dini.
HUO NDIO UCHUMBA

2.NDOA ZAKIISLAM
kwa mujibu wa taratibu za dini, ndoa ya kiislam Ina sharti zake ili kukamilika

Idhini ya Walii.

b) Kuridhika kwa bibi harusi mtarajiwa.

c) Kutimia kwa tamko la ndoa yaani Ijaab na Qabuul (yaani iijab na qubuul iliyounganishwa kwa tamko la ndoa au yenye kufidisha maana hiyo).

d) Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu.

e) Kubalighi na kuwa na utambuzi baina ya wanandoa, hivyo haifai kuwepo kwa ndoa ikiwa mmoja wapo ni mwendawazimu au mdogo kwa umri na bado hajabaleghe.

Yakishakamilika hayo masharti basi ndoa imeshakamilika.
Hayo mengine ya kuwaalika watu kwenye harusi na walima ni sunnah, maana tumeambiwa tutangaze harusi na tufiche uchumba.

Haki Za Mume Na Mke
haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللّهُ عَزِيزٌ حَكُيمٌ

Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shariy’ah). Na kwa wanaume juu ya hao wanawake wana daraja. (Al-Baqara 2: 228)

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema katika Hijjah ya kuaga aliposimama kuwahutubia Maswahaaba:

((يآ أيُّهَا النَّاسُ إِنَّ لِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقاً وَلَكُمْ عَلَيْهِنَّ حَقّ)) أبو داود

((Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu)) Abu Daawuud

Zifuatazo ni haki zinazowahusu wote wawili; mke na mume katika kuamiliana:

1-Ukweli

Mke na mume wawe ni wakweli baina yao kwa kauli na vitendo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ

Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. (At-Tawbah: 11)

2-Mapenzi, huruma na utulivu.

Kila mmoja amdhihirishie mwenziwe mapenzi, na wawe na huruma baina yao katika shida na matatizo mpaka iwe kila mmoja awe ni kutulizo cha mwenziwe wakati wa dhiki. Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) Anasema:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَة ًإِنَّ فِي ذَلِكَ لَآ يَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

“Na katika Aayaat Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaotafakari.” (Ar-Ruwm 30: 21)

3-Amana, Uaminifu na kutumiza ahadi:

Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amewasifu na kuwaahidi Jannah wanaotimiza amana na ahadi zao:

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ

Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (wanazitimiza). [Al-Muuminuwn 8] (Al-Ma’aarij: 32)

Kuweko uaminifu kutazuia dhana mbaya au kutiliana shaka:

فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ

Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah Mola wake (Al-Baqarah: 283)

4-Tabia njema

Wawe na tabia njema katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

Na kaeni nao kwa wema ((An-Nisaa 4: 19))

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akausia:

((Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake)) Al-Bukhaariy na Muslim

5-Kuhifadhiana siri

Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao nje:

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwenda kwa mume wake kisha (mmojawao) akapita kutoa siri yake)) Muslim

Haki hizo zitakapotimizwa kwa mume na mke, itakuwa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

وَلاَ تَنسَوُاْ الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). (Al-Baqarah 2: 237)

Haki za mke kutoka kwa mume:

1-Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe kumvisha na kumtimizia mahitaji yake.

2-Mume ana haki kumfunza adabu mke anapohisi mke anamuasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa). (An-Nisaa 4: 34)

Aayah hiyo inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo kuhusu: ((wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni)).

Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) na wengineo wamesema: “Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali” (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al-Baswriy kasema: “Ina maana mpigo usio wa nguvu”.

Wanavyuoni wamefafanua kuhusu kauli hiyo ifautavyo:

i) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Mke atakapomtii mumewe, itosheleze kuwa matatizo yamekwisha.

ii) Atakapoendelea mke kutokumtii mume wake, basi mume ajitenge naye kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya na atambue kuwa mumewe amamekasirikia. Pindi mke akikubali makosa yake, yaishe matatizo na warudiane katika hali yao ya kawaida.

iii) Ikiwa bado mke hana utiifu, hapo mume anaweza kufuata amri hiyo ya kipigo. Lakini sio kumpiga kwa nguvu bali kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:

عن جابر (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم: أنه قال في حجةالوداع: ((واتَّقُوا اللهَ في النِّساءِ، فإنهن عندكم عَوَانٌ، ولكم عليهن ألا يُوطِئْنَ فُرُشكم أحدا تكرهونه، فإن فَعَلْن فاضربوهن ضَرْبا غير مُبَرِّح، ولهن رزْقُهنَّ وكِسْوتهن بالمعروف))

Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: ((Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha)) Muslim

3-Ni wajib wa mume kumpatia mafunzo ya Dini mke wake ikiwa mke hakujaaliwa kupata elimu ya Dini yake. Mume amfundishe mwenyewe, na pindi asipoweza, amruhusu mke kuhudhuria darasa kwa sababu ni muhimu kwake apate kujifunza yanayopasa kama ‘Aqiydah na Tawhiyd na ajiepushe na shirki. Pia ajifunze Fiqhi na yote yanayohusiana na Dini yake, aweze kutekeleza ibaada zake sawasawa na pia apate kuitakasa nafsi yake na aweze kujiepusha na maasi na aweze kulea watoto wake. Kwa ujumla aihami familia yake na Moto wa Jahannam. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaamrisha hivyo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾

Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto (ambao) mafuta (kuni) yake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa. (At Tahriym 66: 6)

4-Ni wajibu wa mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata Shariy’ah za Dini; mfano mke asipotimiza hijaab. Vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa ambao kaharimishwa nao kuolewa.

5-Ni wajibu wa mume kumhifadhi mke kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi na msimamizi wa mambo yake na ndiye mwenye majukumu ya kumhudumia:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao. (An-Nisaa 4: 34)

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake)) Al-Bukhaariy na Muslim

6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anakataza kutokufanya uadillifu:

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ

Na wala hamtaweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msielemee muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mke mwengine (msiyempenda) kama kining’inio (aliyetundikwa). (An-Nisaa 4: 129)

Na Anasema:

فَإِنْ خِف ْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ذَلِكَ أَدْنَى أَلاَّ تَعُولُواْ

Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki (masuriya). Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea (kudhulumu). (An-Nisaa 4: 3)

Juu ya hivyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameusia wanawake watendewe mema:

((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu)) At-Twabaraaniy

Haki za Mume kutoka kwa Mke:

1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:

((لَوْ كُنْتُ آمِراً أَحَداً أَنْ يَسْجُدَ لأِحَدٍ لأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقَّهِ عَلَيْهاَ))

((Ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake)) Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr

2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:

((إذا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلىَ فِرَاشِهِ فَأَبَتْ عَلَيْه لَعَنَتْهَا الْمَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ))

((Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi)) Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy

3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

((لاَ تُنْفِقُ الْمَرْأَةُ شَيْئًا مِنْ بَيْتِهَا إِلا بِإِذْنِ زَوْجِهَا)) قالوا: "يا رسول الله! وَلا الطَّعَامَ؟ قال: ((ذَاكَ أَفْضَلُ أَمْوَالِنَا)) صحيح ابن ماجه - حديث حسن الألباني

((Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe)). Wakasema: “Hata chakula ee Mtume wa Allaah”? Akasema: ((Hicho ni mali bora yetu)). Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.

Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe.

Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:

عن همام (رضي الله عنه) قال: سمعت أبا هريرة (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا أَنْفَقَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ كَسْبِ زَوْجِهَا عَنْ غَيْرِ أَمْرِهِ فَلَهُ نِصْفُ أَجْرِهِ)) - البخاري

Kutoka kwa Hamaam (Radhiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake)) Al-Bukhaariy

4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).

5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Peponi:

عن عبد الرحمن ابن عوف (رضي الله عنه) قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا صَلَّتْ الْمَرْأَةُ خَمْسَهَا، وَصَامَتْ شَهْرَهَا، وَحَفِظَتْ فَرْجَهَا، وَأَطَاعَتْ زَوْجَهَا, قِيلَ لَهَا: ادْخُلِي مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ شِئْتِ)) صحيح الترغيب

Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao)) Swahiyh at-Targhiyb

Hizo ni baadhi ya haki tulizojaaliwa kuzinukuu, tukitaraji kwamba pindi zikitimzwa, basi ndoa itaendelea kudumua katika usalama na amani.

MUULIZAJI ZINGATIA MPAKA HAPO KWANZA
 
Mash aalha, uislamu hauna kificho wachangiaji mmejitahidi kwa kadri M/MUNGU alivyowawezesha. aliyeuliza swali basi na azingatie hiyo elimu ndogo iliyotolewa, na asisite kuwaona waalimu ama masheikh waliojirani naye kwa ufafanuzi mwingi zaidi.TOFAUTI na dini nyingine mafundisho haya ya kiislamu hayatofautiani maana kitabu ni kimoja na mwalimu ni mmoja, maana yangu hapo ni kuwa yeyote yule utakayemuuliza msingi wa maelezo utabaki ni uleule.........INSHAAALHA.
 
Mashaa Allaah hakika naona almost wachangiaji wote wamechangia vema kabisa kadiri Allaah sw alivyotujaalia. Sasa hadi hatua hii mleta mada sijui una swali la kuuliza au tuendelee mbele zaidi. Au yatosha ndugu SELISELINA alivyotoa maelezo kwa muhtasari katik vipengele vyote kavigusa. Kama utahitaji maelezo zaidi kwa kina nitaendelea
 
Pendekezo
Ndugu zangu katika imani kuna haja ya kuanzisha uzi endelevu 'sepatare' utakaokuwa wazungumzia mada na kujibu maswali mbali mbali juu ya uislam. Kila mwenye mada au maswali na majibu na mengineyo yoyote kwa manufaa ya watu wote anakuwa analeta. Hakika tunatakiwa kufikisha japo aya moja tu katika ummah huu kuulingania na kukumbushana
Allaahu Yaalaam
 
Duu ! Nimekubali Jf. Inawatu wenye uelewa. Nitakosa shukurani, na utu, nikishindwa kuwashukuru wote waliochangia kwa kunisahihisha,na kuiweka Mada vizuri, kunielimisha kwa kina. Mungu, awaongezee uwezo,na nguvu. Hata aliyesema niende madrasa,ushauri wake umepokelewa.
 
Ndugu zangu katika imani naanzisha uzi mpya wa UJUE UISLAM KATIKA JUKWAA LA DINI tuweze kuelimisha. Hivyo hata kama una lolote linalohusiana na dini tambua nawe ni wajibu wako kufikisha ukichojaaliwa. Tambua ya kuwa Yaummul Qiyyamah miongoni mwa maswali utaulizwa ni pamoja na ulitumiaje umri wako na elimu yako uliyojaaliwa japo aya moja uliitumiaje
Wabillah Tawfiq
 
Hongera sana kwa kutuelimisha. Ninachokifurahia katika mafundisho ya uislamu ni kuwa "bado dini yenu haijachakachuliwa na wenye tamaa ya fedha"
 
2. SOMO: NDOA KATIKA UISLAM
Utangulizi.
Qur’an 30:21
“Na katika lama zake amewaumbieni wake kutokana na nyinyi wenyewe ili muishi kwa utulivu nao, na akawatia upendo na rehema kati ya nyoyo zenu. Kwa hakika katika haya ni ishara kwa wenye kufikiri”

Qur’an 16:72

“ Na Allaah amekuumbieni anaetokana na asili yenu na kwa ajili yenu, kutoka kwao watoto wa kiume na wakike na wajukuu na kuwapeni rizki njema”.

Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) amesema:
“Enyi vijana, aliye na uwezo wa kuoa aoe, kufanya hivyo kutamsaidia kuinamisha macho yake chini na kuwa mtii. Na utii ni sehemu ya imani”. (Bukhari).
Na katika hadithi nyingine pia amesema:

“Ndoa ni katika mienendo yangu na atakayekwenda kinyume na hivyo hatakuwa nami” (Bukhari).

Katika aya zilizotangulia Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wata’ala) anatwambia kuwa ameumba waume na wake ili waishi pamoja kwa mapenzi. Wazae watoto na kuishi kwa amani na utulivu na kwa njia hiyo wataweza kutii amri zake na kufuata mafundisho ya Mtume wake.

Kwa ufupi ndoa katika uislamu ni:

1. Njia mojawapo ya ibada. Mnapokuwa katika ndoa mnakuwa mpo katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa mtume saw wake.

2. Kujenga uhusiano wa familia na makundi (jamii).
3. Ni kitendo cha uchaji Mungu.
4. Njia halali ya kuzaliana.
5. Mojawapo ya suluhisho la kuondoa kuchanganyikiwa.

JE NDOA NI LAZIMA?

Imamu Abu Hanifa, Ahmadbin Hanbal na Malik wanasema ingawa asili yake inaonekana ni jambo lisilokuwa la lazima lakini kwa baadhi ya watu linakuwa ni lazima (wajibu).
Imamu Shaafi anasema ni jambo lenye kupendeza (Mubah).

Imeripotiwa na bukhari na wengineo kwamba watu watatu walienda kwa wake za mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) na kuwauliza vipi mtume afanyavyo ibada zake. Walivyoelezwa wakaona inabidi wao wafanye zaidi ya vile alivyokuwa akifanya mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) kwa kuona kuwa kunatofauti kubwa sana kati yao na mtume kiibada japo yeye ni mtu ambaye amesamehewa madhambi yake yote ya nyuma na ya mbeleni. Mmoja wao akasema ataswali usiku daima. Mwingine akasema hatoshughulika na habari za wanawake na hivyo hatooa. Na wa mwisho akasema atafunga daima. Mtume aliposikia habari zao akasema:

“Mimi ni mcha Mungu zaidi yenu, pamoja na hayo ninafunga na kufungua, nina sali na kulala na nina oa. Yule atakaye kwenda kinyume hatakuwa pamoja nami”.

Wanachuoni wamefikia makubaliano kuwa ndoa ni lazima kwa muislamu mwenye uwezo wa kumuhudumia mke. Allaah sw ameahidi kuwasaidia wale wenye kuoa kwaajili ya kujikinga pale aliposema:

“Waozesheni miongoni mwenu wale walio wajane na wema miongoni mwa wajakazi wenu waume au wake iwapo masikini, Allah atawatajirisha kutokana kmknhazina zake”. (24:32).

Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) amesema:

“Kuna aina tatu za wenye haki ya msaada wa Allah, mwenye kuoa kutaka aishi maisha mema, mtumwa ambae bwana wake amekubali kununua uhuru wake atakapo kuwa tayari kulipa na mwenye kupigana katika njia ya Allah”. (Ahmad, An-Nisai, Attirmidhiy, Ibn Majah na al-Hakim).

WANAWAKE WASIO RUHUSIWA KUWAOA

1- Mke wa baba, awe ameachwa au kafiliwa na baba.
2- Mama, wakiwemo mabibi wa pande zote.
3- Binti, wakiwemo wajukuu wa kike kutokana na watoto wako wa kike au wa kiume.
4- Dada, akiwemo wa baba au mama mmoja.
5- Shangazi kwa baba, au mama mmoja na baba.
6- Binti wa kaka.
7- Binti wa dada.
8- Mama aliyekunyonyesha.
9- Mabinti wa mama aliyekunyonyesha.
10- Mkwe wako wa kike (mama wa mke).
11- Ndugu wawili wa kike kuwaoa wakati mmoja.
12- Mwanamke mshirikina (anayeabudu masanamu).
13- Kahaba
Inaelezwa kuwa Murtaid ibn Murtaid alimuomba Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) amuoe mwanamke aitwae Anaq ambae alikuwa na uhusiano naye kabla ya uislam. Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) hakumjibu mpaka aya ikashuka isemayo:

“Mzinifu mwanamume hatooa ila mzinifu mwanamke au mshirikina mwanamke na mzinifu mwanamke hatoolewa na yoyote ila na mzinifu mwanamume au mshirikina mwanaume. Na kuwaoa hawa ni haramu kwa muumini.”

Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) akamsomea Murtaid hiyo aya na kumwambia asimuoe (Abu Daaud, an-Nisai na Tirmidhiy).

KUCHUMBIA

- Hairuhusiwi kumposa mwanamke alie katika eda ya kuachwa au kufiwa na mume kwani wakati huu huhesabiwa ni sehemu ya ndoa yake mwanamke.

- Hairuhusiwi kumposa mwanamke ambaye anajulikana kuwa amekwishaposwa na mtu mwingine.

Katika hadithi iliyopokelewa na Muslim, Mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) anasema:

“Muumini ni ndugu wa muumini mwingine. Kwa hivyo hairuhusiwi kwake kumpiku ndugu yake katika kununua kitu au kutoa posa kwa mwanamke wakati anapokuwa ndugu yake ameshaposa, ila awe amempa ruhusa”.

KUMUONA MCHUMBA UNAETAKA KUMUOA

Ina ruhusiwa kumuona mchumba kwa sababu wanaosema jicho ni mtumishi wa moyo. Na macho yatakapoonana na kukutana na nyoyo za mume na mke zinaweza zikakutana.

Al-Mughirah ibn Shui’bah amesema:

“Nilitaka kumuoa mwanamke, mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) akaniuliza kama nimemwangalia nikamjibu bado akaniambia nikamwangalie kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta mapenzi kati yetu. Nikaenda kwa wazazi wake na kuwajulisha ushauri wa mtume (Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam) wakawa wamesita juu ya hilo. Binti yao akasikia maongezi akasema: ‘iwapo mtume amesema uniangalie basi niangalie’. Nikamwangalia na hatimae nikamuoa”.(Ahmad, al-Tilmidh, ibn Majah, ibn Hakim).

NIKAHA

Mambo yatakikanayo kutimia ili ndoa ikamilike kufungwa.

1. Mlezi: Baba au mwakilishi wake wa kutoa idhini.
2. Mahari (Qur’an 4:4):

“Wapeni wanawake mahari yao…”.

3. Muoaji na Muolewaji.
4. Kauli ya kuozesha na kukubali.
5. Mashahidi wawili.

HAKIKA MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI
Hiyo namba 5 kwamba inazuia kuchanganyikiwa cjaelewa?
Halafu kwa mfano mm ni mwanamke wa kiislam nataka kuolewa je naweza kumtolea mahali mwanaume kidin inaruhusiwa?
 
Mashaa Allaah hakika naona almost wachangiaji wote wamechangia vema kabisa kadiri Allaah sw alivyotujaalia. Sasa hadi hatua hii mleta mada sijui una swali la kuuliza au tuendelee mbele zaidi. Au yatosha ndugu SELISELINA alivyotoa maelezo kwa muhtasari katik vipengele vyote kavigusa. Kama utahitaji maelezo zaidi kwa kina nitaendelea
Kwanza nahifadhi haya, ni mambo mazito, yenye elimu, niliyoitaka hata huko Bakwata,nisingeipata!_- Wako wapi?
 
Back
Top Bottom