BAKWATA ni taasisi ya Serikali?


Why now?
what is the motive?
 
kabla ya kuja na hizi Ngojela zako ungejilidhisha kwanza huyu Makonda anajenga msikiti kama nani?
 
Nakumbuka kuna miaka ya nyuma ulikuwaga moderator.
Kwa utumbo uliotema hapa inaonesha dhahiri kuna watu uliwapa ban kwa kuwaonea tu na wengine hukuwapa kwa sababu hukutambua makosa kutokana udhaifu kwenye kuchanganua mambo.

Huyu anajivua nguo tu humu
 
Muda mwingine unaweza kuhisi serikali inamtumia Makonda kufikisha mambo yaliyomengi yenye UKAKASI...kufukaza ombaomba,kufukaza vijana wote wasio na kazi DSM
 
Makonda kama mwanamchi wa kawaida atasaidia kupatikana kwa kiasi husika kujenga hilo jengo...!

Ninge shangaa kama Bawacha na roho za husda lingewapita hili..
 
Nimeiona hii habari nimeshangaa!
Let's hope hizo bilioni tano ni zake makonda personally. Isije ikawa ni hela za jiji!

Atahamasisha wafadhili lkn hatoi mfukoni kwake au kwa serikali
 
Na ona upande wa pili mnaona wivu tu.. Lini bakwata ilikua huru.. Acha watujengee makao makuu..
 
The Boss iko hivi,

Bwana mkubwa ni mkatoliki na alionesha hilo dhahiri siku ya ijumaa kuu kwa kwenda kubusu msalaba pale saint Peters,

Hii nini maana yake? Kwa Wakatoliki hawana tatizo lolote na utawala huu, kondoo wao ndio yuko kwenye usukani.

Bwana mtukufu akatoka hapo akaibukia Lutheran kwenye ibada ilikuwa ni timing agongane na Laigwani pale lakini timing ilikuwa mbovu.

Hakuishia hapo akaibukia kwa Mzee wa upako ukiangalia vizuri ziara hizi kwa upande wa makafiri deal done.

Akawageukiwa wenye deen ya haki with cash money ndani ya briefcase na kuwaahidi kuzirudisha mali za wakfu za waislamu.....

Leo Makondeko kijana wa nyumbani Kawekamo anakaa na Bakwata kuwawezesha ujenzi wa ofisi.

Mmekwisha, ukimya wa kina Deus Kibamba na taasisi zote zenye kelele ukitaka kupata jibu sahihi Google Mussolini halafu angalia utawala wake Italy ulifanikiwaje na wakati alikuwa Fashisti?

Jibu ni rahisi tu aliliweka mfukoni kanisa katoliki na kanisa kwa neema ilizomwagiwa na huyu fashisti Papa na makadinali wake wakavaa miwani ya mbao kama vile hawaoni nchi ilivyokuwa inaendeshwa, mapadre walilipwa mishahara na serikali ya Italy na kama haitoshi kanisa likapewa nchi yake ndani ya Rome, nchi hiyo inaitwa Vaticano.

Hili ndilo linakuja kutokea huku tusipokuwa makini, wanaanza taratibu tu hivihivi ila ikifika wanataka waungwe mkono hadi na maradical kama Mohamedi Said basi Waislamu watapewa mahakama ya kadhi na makadhi wataingizwa kwenye payroll ya serikali, hapo unakuwa umeshawatia mfukoni waislamu na kuwaziba mdomo.

Huwa sipati jibu mpaka leo chuo cha Tanesco kidato kilichokuwa kinazalisha wataalam wa umeme kupewa waislamu kana kwamba hii nchi wapagani hawana haki.

Tuendelee tu kupiga makofi muda utaongea.
 
Wabunge wa upinzani mliwaponda sana kuwa walikuwa wanakula posho za bure wakati wakitoka nje ya bunge kipind cha budget.

Mi binfsi nimeanza kuelewa kuwa nia yao ilikuwa nzur sana kwa maendeleo yanch yetu.

Walielewa kuwa kuendelea kukaa bungeni et wanapanga budget ambayo mkuu wa nchi hta ifuata ni kupoteza muda na pesa za umma.

Sasa hapa waliokula bosho za bure ni wakina nani kama sio wabunge wa CCM waliopitisha budget hewa.
 
Hata NGOs zitaenda kwa mwendo huohuo, yaan kama mrema na parole, baada ya hapo kusifia mwendo mdundo, sasa sidhan kama watakumbuka mahakama ya kadh
 
Toka kuumbwa kwa dunia hakuna mashirikiano kati ya serikali na watu wa dini ila kuna uadui kati yao.
kwani asili ya serikali zote ni dhulma na dini huwa inatetea wanyonge na kutoa haki kwa kila mmoja hivyo basi haki na batili hazikai pamoja Ukiona dini na serikali zimekaa pamoja na kuelewana ujue hapo watu wa dini wanamatatizo Ndio maana watu kama sheikh ponda,mselemu ally,faridi wanatetea haki za wanyonge ona wanavyopata tabu
 
We mwanasheria wa wapi unauliza swali hili?
Bunge na mahakama zipo chini ya serikali?
TFF iko chini ya serikali?
Catholic Church iko chini ya serikali?
We mwanasheria wa wapi unauliza swali hili?
Bunge na mahakama zipo chini ya serikali?
TFF iko chini ya serikali?
Catholic Church iko chini ya serikali?
Kinadharia hizo taasisi ulizozitaja haziko chin ya gov. lakin practically hizo taasis zinafanya kaz zao kwa matwaka ya gov
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…