BAKWATA ni taasisi ya Serikali?

Waisilamu huwa wananishangaza sana. Kuna wakati walikuwa wanataka serikali kuwaanzishia mahakama ya kadhi, lakini wanapinga serikali kuwaanzishia BAKWATA

Nashukuru moto wa mahakama ya kadhi umepoa, na kwa kubana matumizi kwa JPM, itabidi wasubiri atakapokuwa hayupo madarakani!
 
Mzee wangu Mohammed Said

Ni jambo jema sana na yapasa kumshukuru Mungu, kwa namna anavyowaumbua wale wanafiki ambao walikuwa wanakusema na kukutukana wewe kwa nyakati tofauti juu ya minakasha yako ya Serikali ya CCM na BAKWATA. Leo hii jibu limepatikana.

Vile vile kuhusu hila na ghilba za Julius Nyerere, Leo hii kupitia kifo cha Mzee Jumbe, watu wameanza kuziamini.

Sasa nadhani, itakuwa jambo la kiustaarabu sana kama hao watu wakikuomba msamaha hata kwa njia ya PM.
 
Lengo la serikali ni kuhakikisha madai ya waislamu yanaletwa na watu makini
 
Asante kiongozi, hapa tunapata tafsiri ya hilo gorofa na vile 'vitita'
 
Ndugu zangu hili suala la Wanasiasa kuingilia mlango wa Dini kufikia malengo yao Daima binafsi sitolifumbia macho kusema.

CCM kutumia mlango wa dini acheni mara moja,na mkome tabia hiyo msije kuliingiza Taifa katika matatizo au machafuko ya kidini yasiyo ya lazima kwani taifa letu halifungamani na masuala ya dini.

Nanyi viongozi wa dini zote mnayo yafanya hakika hayapo katika imani zetu zote ziwe za Uislam na Ukristo na hata kama na mengineyo,jukumu na lengo la ninyi Viongozi wetu wa dini ni kusimamia,kutoa elimu na kuongoza ibada kwa imani yenu husika TU na siyo huko mnapo jificha na kutaka kupitia au wanasiasa wanapotaka kupitia

Ninyi viongozi wa dini simamieni misingi THABITI ya imani yenu na muache kuyumbishwa na ya duniani kwani mtaulizwa baadaye kwa kupotosha na kupoteza umma huu waWatz.kwa makusudi kisa tu maslahi yebu binafsi.

Hakika hili mtalijibu na kutoa hesabu yake ahera,endapo mtakubali kutuingiza au kuchanganya siasa na imani za watu.Kumbukeni hawa wanasiasa ni watu wenye malengo yao binafsi na yakishatimia mkataba umekwaisha na itakuwa tayari mmekwisha muudhi Allah na kutufarakanisha sisi waumini wenu.

VIONGOZI WA DINI PIGENI MARUFUKU KABISAA WANASIASA KUTIMIZA MALENGO YAO KUPITIA DINI NA NINYI WANASIASA MSIYO MUOGOPA MUNGU ACHENI UPESI KABLA KIAMA HAKIJASHUSHWA KWENU NYOTE.. PERIOD!!!!!
 
BAKWATA ni kibaraka wa serkali na ccm baada ya kuuwa EAMW S ndo iliundwa miaka 1960,serikali ilishirikiana na akina Nassib wa Bukoba ili kuvunja nguvu ya Aghakan aliyekuwa mlezi wa jumuiya ya kiislamu kama ilivyotajwa hapo juu.Hii ndiyo sababu Bakwata haikubaliki kwa waislamu wengi wasomi.
 
Sijamuelewa kabisa Makonda.Anasema serikali ya mkoa wa Dar es salaam inatoa mapesa hayo kweli?...Kwahiyo nchi hii ni ya kidini?
 
Yaani tuseme waislam hawana uwezo wa kuji organize wenyewe hadi wasaidiwe na kafri.
 

Serikali inafidia kwa waislam kwa kuteua zaidi ya 75% wakiristu kwenye uongozi
 
BAKWATA ni tawi la CCM.
 
Daah his hela in at okay kwenye fungu gani? Kuna nini nyuma ya hii misaada. Naomba baada ya kumaliza huo ujenzi wakajenge na makao makuu ya kkkt
 
Wana chuo wa Udom wana kula nyasi huko field kisa hawajapata malipo yao, duh kweli hata kile kidogo tulicho nacho makapuku tunapo konywa!
 
We unaona haya majungu?
BAKWATA kuwa chini ya serikali kwako ni jambo zuri?
Mkuu nikufafanulie tu,hiyo pesa haitoki serikalini,Makonda amehamasisha upatikanaji wa hiyo pesa,inatoka kwa akina Mengi hata TEC wamechangia na mufti kasema bi halali kupokea hela ya mchango wa asiekuwa mkristo akasema hata mtume Muhammad (SaW) aliwahi kupokea,
 
.....hapo dar ukienda temeke na mwananyamala hospital kina mama wanalala chini....huyo makonda anashindwa kuwasaidia...hapo dar huyu huyu makonda anaomba wadau wachangie madawati.....leo anapata wapi bil.5 za kuwajengea bakwata??.....taasisi za dini kila leo wana mikakati ya kusaidiana kujenga taasisi zao..na hili wala si shida....sasa hizi siasa kuingia kwenye taasisi ya dini inakuwaje??pesa wanachimba wapi??...hizi comedy tz haziishi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…