BAKWATA na muundo wa Katiba

BAKWATA na muundo wa Katiba

Msolopagaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2014
Posts
461
Reaction score
212
Ndugu wadau,kunajambo limenifanya niwe sensitive sana na uoga pia umeniingia. Jambo lenyewe ni hofu ya baadhi ya wananchi(hasa humu jamii forum nkiamini nkama sample inayowakilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi)kuhusu mahakama ya kadhi katika rasimu ya katiba.

Kwa mtazamo wa wengi(hasa wakristo)wanahofu ikiwa mahakama ya kadhi itapitishwa katika katiba hii mpya. Lakini LOGICALLY hofu ni nini?

Hebu tuijue kidogo mahakama ya kadhi. Mahakama ya kadhi ni mahakama ya dini ya kiislam ambayo hukumu zake znapitishwa kulingana na sheria za kiislam (kutoka katka quran na hadith). Sasa wewe ambae sio mfuasi wadini ya kiislamu unadhurikaje na hili? Kwa wewe kutokuwa muislam tayar katiba inakulinda na mahakama ya kadhi haina mamlaka na wewe.

Kwa nchi ambazo ni za kiislam hasa UARABUNI,tunawaita wenye siasa kali kwa vile wao wana observe sheria zote za kiislam ikiwa na mana kwamba kwao ndo katiba yao. Sasa kwenye nchi ambazo sio za kidini KATIBA ndio mwongozo mkuu ambapo sheria za kidini zinafata mwongozo huo katka kutekeleza hukumu zake.

Naomba nitoe mfano:
Tunajua fika Kenya mahakama ya kadhi ipo lakn hatujawah kusikia mtu kakatwa mkono(ingawa hukmu ya muislam aloiba ni kukatwa mko)na hii ni kwavile tayar katba ilishaweka hukmu yake.

Pia hatujaskia mtu akipigwa mawe hadi kufa(ingawa kwa muislam mwenye mume au mke akizni na mwanando mwingine hiyo ndo hukmu). Sasa mimi najiuliza,Ikiwa hukumu ni laini tu na HAZIMGUSI MKRISTO bali MUISLAMU tu,nini hofu? Kwa hapa kwetu mahakama ya kadhi itabezi katka kutoa hukumu ya MIRATHI na NDOA. Na katka hili ili mjue wakrito hawatadhurika kwa chochote ni kwamba MFANO muislam kamuoa mkristo hata wawe namatatizo ambayo yanahtaji suluhsho kupitia mahakama ya kadhi,hii mahakama hatawashughulikia kwavile wamechanganya iman mbili kwahiyo hukumu haitawezekana na hawa mkumbuke hata chet cha ndoa watachukua cha serikali,sasa hofu ya nini?

Na mirathi ni hivo hivo kama wanando ni dini tofaut mmoja kafa kuhusu mirathi wala mwenza asjisumbue kwenda kwa kadhi mana sheria hairuhusu kugawa hiyo mirathi. Umeonewa rudi kwenye katiba ya nchi angalia inasemaje kuhusu mirathi,nenda mahakaman na ustawi wa jamii kwa ajili ya haki yako.

Ndugu zangu, mwenye hofu na mahakama ya kadhi, kama hofu yake ni kuwa itamkandamiza mkrito, aondoe shaka hilo halimhusu. Na kwa muislamu yeyote mwenye kuiogopa mahakama ya kadhi asiiogope hiyo kwanza amuogope yule aloumba nafsi na roho.

JABBAR.
 
hiyo mahakama ya kadhi itagharamiwa na nani?
pili, kenya na uganda waislam ni wachache sana (less than 20%). hapa Tanzania kuna significant population ambayo ni waislam (30%-40%), na hiyo naturally inasababisha tension ambayo tayari hapa tz ipo. ukileta hiyo mahakama utakuwa tu unatibua maji bora tuache mambo kama yalivyo kwa sasa.
 
Hao bakwata na makadhi ni njaa tuu zinazowasumbua na hasa pale penye kesi ya mtu alicho nacho na asiyekuwa nacho ndo hapo tatizo na shehkh atatoa hukumu kwa mujibu ya yule aliezidi hongo ndo mshindi
 
Hatuhitaji kuingiza masuala ya dini kwenye katiba. Mmepewa uhuru wa kuabudu na kuunda vyombo vyenu kwa imani yenu bila kuingiliwa, fanyeni hivyo bila kuvunja sheria. Kama ulivyosema wengi wanahofu, ni kweli wengi tunahofu kwa sababu mambo ya kuingiza masuala ya dini ya kiislam kwenye katiba za nchi yamepelekea umwagaji damu usiomithirika duniani. Hatutaki. Katiba ya taifa iwe kwa maslahi ya taifa zima. Habari za dini na mahakama za ndoa zenu undeni utaratibu wenu wenyewe lakini sisi hatutaki kuona kwenye katiba ya nchi. Hivi kila dini ama kabila zikaamua kulazimisha katiba isajili mahakama zake, itakuwaje? Msidhani ni dini yenu tu ndiyo ina taratibu za kumaliza migogoro. Kila dini kuna taratibu zake. Kila kabila lina taratibu zake. Lakini kwa uungwana, maadamu serikali haiingilii uhuru wao, wanavyombo vyao na wanamaliza migogoro yao kwa kanuni zao zile bila kulazimisha serikal ishiriki ili lmradi hawavunji sheria. Masuala haya sisi hatutaki. Vinginevyo mtangaze kwamba Tanzania ni nchi ya kiislam tujua la kufanya.

Mkuu kama ishu ni gharama kwa hapo simpingi mkristo yeyote,waislam inabdi wajipange wenyewe. Ila kuhusu wingi wao ambao wewe unaona kwamba unaleta tension,sasa hlo ntatizo lako mwenyewe hyo tension hamhusu muislam
 
Ushahidi wa hilo uko wapi? Nahata kama ikifanyika hivo, inawahusu zaidi waislam. Kuna mabaraza yawazee watawekana sawa
 
Hatuhitaji kuingiza masuala ya dini kwenye katiba. Mmepewa uhuru wa kuabudu na kuunda vyombo vyenu kwa imani yenu bila kuingiliwa, fanyeni hivyo bila kuvunja sheria. Kama ulivyosema wengi wanahofu, ni kweli wengi tunahofu kwa sababu mambo ya kuingiza masuala ya dini ya kiislam kwenye katiba za nchi yamepelekea umwagaji damu usiomithirika duniani. Hatutaki. Katiba ya taifa iwe kwa maslahi ya taifa zima. Habari za dini na mahakama za ndoa zenu undeni utaratibu wenu wenyewe lakini sisi hatutaki kuona kwenye katiba ya nchi. Hivi kila dini ama kabila zikaamua kulazimisha katiba isajili mahakama zake, itakuwaje? Msidhani ni dini yenu tu ndiyo ina taratibu za kumaliza migogoro. Kila dini kuna taratibu zake. Kila kabila lina taratibu zake. Lakini kwa uungwana, maadamu serikali haiingilii uhuru wao, wanavyombo vyao na wanamaliza migogoro yao kwa kanuni zao zile bila kulazimisha serikal ishiriki ili lmradi hawavunji sheria. Masuala haya sisi hatutaki. Vinginevyo mtangaze kwamba Tanzania ni nchi ya kiislam tujua la kufanya.

Mambo ya kuingiza ishu za dini kwenye katiba yamepelekea umwagaji wa damu,ok sikatai,je unaweza kunipa relevant example with reference ili kuthibitisha usemi wako? Na uoneshe muunganiko halisi kati ya umwagaji wa damu na mahusiano yake na kipengele cha ishu za dini katika katiba hiyo. Na lingine ni kwamba, huo umwagaj wa damu unaosema umeshatokeaga ulihusisha wafuasi wa dini moja au dini mbili? Kama ni mbili hapakwetu kwa ishu hii haiwez tokea manake wanaohukumiwa ni wa upande mmoja tu katka sheria hizo.
 
Hao bakwata na makadhi ni njaa tuu zinazowasumbua na hasa pale penye kesi ya mtu alicho nacho na asiyekuwa nacho ndo hapo tatizo na shehkh atatoa hukumu kwa mujibu ya yule aliezidi hongo ndo mshindi

Ficha UPUMBAVU wako KAFIRI mkubwa wewe,,,una dhani Mahakama ya kadhu kama kisutu?
Huku Duniani mna msemo wenu "Sheria Duniani haki mbiguni" sasa kwa M /Mungu hakuna kitu kama hicho

Sent from my iPad Air using JamiiForums
 
Hiv katiba ya sasa isiyo tamka mahakama hiyo inawazuia waislam kutatua migogoro ya ndoa ma mirathi kidini?
 
Ni mwehu pekee ndiye anaweza kutetea upuzi huu. Wewe huoni yanayotoekea hadi uombe mfano jf? Unaishi dunia gani? Hata hivyo siku zote waislam hata kule walikoharibu tayari, walianza kwa lugha rahisi lakini zenye hila ndani. ISIS walipoanza Syria walionekana wema wenye mambo yao. Walipoingia iraq wakaanza kwa kuonyesha wema kama hawana tatizo na mtu. Leo yko wapi? Ni nani aasiyefwafahamu kwa hila?

Kwanza mnashindwa nini kufanya mambo yenu ya kidini hadi serikali iingilie? Ni kwa sababu ya mapigano misikitini kila siku kiasi kwamba hamwezi kufanya jambo hadi dola iwasimamie? Kama matatizo yenu ya ndoa yamekuwa mengi hadi yaundiwe mahakama, umoja wenu katika famlilia ni shida, hamwezi kumaliza masuala ya mirathi hadi yaundiwe mahakama, bado mahakama hizi hamwezi kuzisimamia hadi serikali, si muache hiyo dini?

Hili halijadiliki. Kama mnataka anzisheni hizo mahakama misikitini. Serikali haiingii kwenye huo msala. Hili halipo. Full stop.

Mambo ya kuingiza ishu za dini kwenye katiba yamepelekea umwagaji wa damu,ok sikatai,je unaweza kunipa relevant example with reference ili kuthibitisha usemi wako? Na uoneshe muunganiko halisi kati ya umwagaji wa damu na mahusiano yake na kipengele cha ishu za dini katika katiba hiyo. Na lingine ni kwamba, huo umwagaj wa damu unaosema umeshatokeaga ulihusisha wafuasi wa dini moja au dini mbili? Kama ni mbili hapakwetu kwa ishu hii haiwez tokea manake wanaohukumiwa ni wa upande mmoja tu katka sheria hizo.
 
Nchi hii haina dini ndio maana mtu anapewa uhuru wa kuabudu atakavyo ila asivunje sheria za nchi
 
Mimi kama Mkristu hoja kwamba ni tatizo kuingiza Mambo ya dini katika katiba ni tatizo haina mashiko. Hata sasa hivi applicable laws Tanzania ni pamoja na Islamic Laws kwenye Muslims personal matters. Someni Katiba iliyopo na Sheria inayoitwa Judicuture and Application of Laws Act. Inasema Islamic Personal Laws zinatumika km sehemu ya sheria zetu.

Pia, ukiangalia jurisdiction ya Primary Court ni pamoja na mambo ambayo sheria za kimila pamoja na za kiislam zinatumika.

Na ni ukweli Mahakimu Waliopo wanazitumia kuamua kesi. Masharti yake ni kwamba Lazima pande zote wawe Waislam.

Changamoto iliyopo ni pale ambapo hakimu mkristu anawahukumu Waislam kwa sheria ya Kiislam.

Majaji wengine wajanja wao huomba opinion toka kwa muslim scholars na kuzitumia km expert opinion although not binding upon them.

Sijui kwa nini Waislam hawaridhiki na hali ilivyo. Ila Rwanda Uganda na Kenya zipo kwenye katiba na hutahisi ukiwa huko mana zinawahusu wao kwa mambo binafsi km ndoa mirathi talaqa kuzika n.k.

Haigusi transactions laws au criminal laws hata km wote ni Waislam.

Kwanini wenzetu wameziweka kwenye katiba na kusimamiwa na serikali?

Nadhani jibu lipo wazi.

Ukiziweka Chini ya setikali na kuzugharamia una Baki na nguvu ya kuzisimamia na kuchukua hatua za haraka km wanatenda kinyume.

Lakini ukiwaachia wenyewe watazipeleka watakavyo na mwisho wa siku utakuja kushtuka washazifanya kuwa na nguvu kuliko ilivyotakikana. Si ajabu zikawa sababu ya kudai au ku assume jurisdiction zaidi.

Pia kuzirasimisha na kuziweka Chini ya mfumo rasmi ktk serikali kunatoa fursa ya rufaa kwenda mahakama za juu. Check and balance inapatikana pale wanapotoa hukumu inayokinzana na haki.

Vile vile utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama ya Kadhi km iko rasimishwa yatafabywa
 
Sory nimalizie. Utekelezaji wa maamuzi utafanywa na normal courts kwa hiyo km kuna injustice itaondolewa. Hili linawezekana ikiwa ktk mfumo rasmi.

Sometimes if you want to control someone so that he doesn't hurt you bring him in your home and recruit a guard well armed. It has costs of feeding and guard but you will be safer than letting him at large.
 
Mufti Sheikh Mkuu Shaban tayari alikwisha teua makadhi wa mikoa na wilaya! Hivyo tayari mahakama hizo zipo na zinafanya kazi kama kawaida!

Wanachohitaji waislam hapa ni serikali izigharimie mahakama hizo! Kama sheria itatungwa kuilazimisha serikali kugharimia mahakama hizo suala ya kuweka mahakama za kadhi katika katiba halipo kabisa!
 
Hatuna dini nchi hii full stop ukitaka hukumu ya kikadhi zifuate kwenye nchi zinazo tekeleza hilo
 
Mkuu kama ishu ni gharama kwa hapo simpingi mkristo yeyote,waislam inabdi wajipange wenyewe. Ila kuhusu wingi wao ambao wewe unaona kwamba unaleta tension,sasa hlo ntatizo lako mwenyewe hyo tension hamhusu muislam

Mkuu nadhani issue sio gharama tu, kuna zaidi. Suala kuu kuliko yote kwenye suala la Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba, nionavyo mimi, ni madai ya UDINI ndani ya Katiba ya nchi isiyokuwa na dini; hili ndio suala la msingi, na ndipo hofu ya wenye hofu ilipo; mengine kama gharama, n.k. ni ziada tu.

Kwa mfano, hivi ikitokea mataifa au matajiri wa ndani au waislamu kwa umoja wao wakaamua kuchangia gharama zote za uendeshaji wa mahakama husika kwa sharti kwamba itambuliwe ndani ya Katiba bado sidhani kama "wenye hofu" watakuwa wameondokewa na hofu yao kwa sababu bado kiini cha hofu, yaani udini ndani ya Katiba ya Jamhuri, bado kingalipo.

Labda niulize swali rahisi tu, Mahakama ya Kadhi ni suala la kidini au sio suala la kidini? Tukipata jibu sahihi la swali hili, tutapata msingi imara wa kujenga hoja zenye mashiko kuhusiana na suala la Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba ya Jamhuri.
 
Mambo ya kuingiza ishu za dini kwenye katiba yamepelekea umwagaji wa damu,ok sikatai,je unaweza kunipa relevant example with reference ili kuthibitisha usemi wako? Na uoneshe muunganiko halisi kati ya umwagaji wa damu na mahusiano yake na kipengele cha ishu za dini katika katiba hiyo. Na lingine ni kwamba, huo umwagaj wa damu unaosema umeshatokeaga ulihusisha wafuasi wa dini moja au dini mbili? Kama ni mbili hapakwetu kwa ishu hii haiwez tokea manake wanaohukumiwa ni wa upande mmoja tu katka sheria hizo.
Mbona unachagua vya kujibu? Umeambiwa kuna dini nyingi sana hapa TZ na kabila nyingi sana kama kila kabila au dini ikiingiza ishu za dini yake hii itakuwa katiba? Msukumo wa kutoa ufafanuzi umeutoa wapi? Kuchukua nafasi ya Mungu umeanza lini, eti hii haiwezi tokea, utazani unaongelea scientific issues labda kuzama na kuchomoza kwa jua, kwa habari ya social issues utasemaje haiwezkani?. Hivi kuvua viatu msikitini mmetumia mahakama gani, mbona waumini wanatii tu? habali ya dini haihitaji mahakama kwa sababu hakimu ni Mungu tu!
 
Back
Top Bottom