MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
BAKWATA kirefu chake ni Baraza kuu la waislam Tanzania, kwakweli mpaka sasa hatujui ni waislam gani wanaowakilishwa na taasisi yetu hii,ni swali lililokosa jibu muda mrefu.Sasa viongozi kazi yake nini?
Kufuatia kuuawa na polisi kwa kijana wa kiislam anayejulikana kwa jina maarufu la "SALUM" huko kurasini jiji Dares salaam kwa madai kua alihisiwa kama gaid/Jambazi,Mpaka sasa taarifa zinazotolewa na jeshi la polisi ni tata zinazochanganya, mpaka sasa Baraza kuu la waislam liko kimya, Sheikh wa mkoa yuko kimya.
Kwa uchunguzi uliofanywa na vyombo mbali mbali vya habari ni kwamba Waumini wa msikiti aliokua akisalisha kurasini wamedai kua Salum alikuwa imamu wa msikiti na ni kijana mwenye adabu, wazazi wake na walezi pamoja na majirani wanadai kuwa kijana wao hana historia ya matukio mabaya na amekulia katika malezi ya unyenyekevu,ndugu zake wa nyubani kwao wanasema Salum ni mpole, Walimu wa chuo kikuu Cha Dar es salaam ambako Salum alikua akisoma wanasema kuwa ni kijana mwenye akili sana darasani na ni mfano wa kuigwa kwa nidhamu yake. Sasa leo anapigwa risasi kwa kuhisiwa kuwa ni gaidi, kwakweli BAKWATA wameusikitisha umma sio siri.
Yaani tunakoelekea ni kwamba kufuga ndevu inaweza kumhatarishia mtu uhai wake kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
Hili jambo la kuuawa kwa kijana huyu lisipotazamwa kwa makini linaweza kuzua hali sio nzuri, Waislam wengi hili suala wanalifuatilia kwa karibu sana na ukimya wa BAKWATA pia unaweza kuleta matatizo.Taasisi ilitakiwa kuwa chombo muhimu cha kuwasemea waislam lakini viongozi wake wako kimya.