BAKWATA: Hatujapokea taarifa yoyote kuhusu kwenda ibada ya Hijja ukiwa na chanjo ya Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema hakuna taarifa yoyote iliyoifi kia baraza hilo na taasisi zingine zinazohusika na masuala ya ibada ya Hijja kwa mwaka huu iliyotolewa na wizara inayohusika na jukumu hilo kutoka Saudi Arabia.

Aidha imesema taarifa zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ikiinukuu mamlaka za nchi hiyo juu ya utaratibu unaowataka mahujaji wanaokusudia kwenda nchini humo kuwa wawe wamefanyiwa chanjo ya Covid-19 haina ukweli wowote na kama ingekuwa sahihi basi taarifa hizo zingeifikia Bakwata kwa utaratibu uliozoeleka wa utoaji wa taarifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma alisema hadi sasa siyo Bakwata wala taasisi zingine zinazohusika na Hijja zimepokea maelekezo hayo, hivyo Waislamu wanapaswa kuwa watulivu na kuendelea na majukumu yao wakati wakisubiri taarifa rasmi kutoka mamlaka husika.

“Ni vizuri Waislamu wakaendelea kuwa na subira kwa sababu kila mwaka taarifa zote zinazohusu Hijja huwa zinazotolewa rasmi na kitengo cha Bihfa ambacho ni maalumu kwa ajili ya utoaji wa taarifa katika Ofisi ya Mufti ya kule Zanzibar, hivyo kila kitakachotakiwa kufanyika kuelekea katika ibada hiyo mamlaka zetu zitapewa taarifa nazo kuzitolea kwa wananchi,”alisema.

Hata hivyo alisema kutokana na changamoto za ugonjwa wa Covid-19 ulimwenguni kote, mataifa mbalimbali yamekuwa yakichukua hatua dhidi ya janga hilo, hivyo huenda kukawa na utaratibu wa kuingia katika nchi hiyo na hiyo itakuwa pale ambapo taifa hilo litakapowashirikisha wadau wake kwa kuwapa taarifa rasmi kuhusu Hijja.

Aidha kuhusu maandalizi ya ibada ya Hijja kwa ujumla wake, Mruma alisema utaratibu wa ibada hiyo ambayo hufanyika mara baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Idd El Hajj utafanyika mara baada ya utaratibu wa kila mwaka unaohusisha mwongozo wa ibada hiyo kutoka nchini Saudi Arabia mahali inapofanyika ibada hiyo.

Alisema mara taarifa za ubada hiyo zitakopolifikia baraza hilo na taasisi zingine zinazohusika na masuala ya Hijja nchini, baraza litazisambaza kwa waumini wote nchini ili waweze kuanza kufanya maandalizi ya kawaida ya kila mwaka ya kwenda nchini humo.

Aliwataka watanzania kuepukana na taarifa mbalimbali zinazosambazwa katika mitandao, ikibidi kuzifanyia utafiti pale wanapozipata ili kujiridhisha nazo badala ya kuanza kujawa na hofu zisizo na msingi, suala alilodai kuwa halina mantiki ndani ya taifa la sasa linalozidi kukua kimaendeleo.


HabariLeo
 
...Duniani huko hawana mzaha linapokuja suala la Corona; linapokuja suala la kulinda uhai wa wananchi wao kwao ni priority number moja! Nani aliwahi kuwaza ingekuja kutokea Makha ifungwe kwa ajili ya hijja?

Nawashauri hao BAKWATA kama "wamesikia" basi wazitafute wenyewe wasisubiri "kuletewa" ili kuweka mambo sawa kungali mapema! Msije kusema "hatukujua"!
 
Kama kuna watu wameshikiwa akili basi ni BAKWATA ya Mufti Zubeir na Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Dar Sheikh Alhad.
Hivi hawaoni Wakatoliki kupitia TEC na KKKT wanavyoweka misimamo dhidi ya Serikali kwenye ugonjwa wa Corona?

Hiyo misaada ambayo Meko anawapa ya magari ya kutembelea, ukarabati wa nyumba zenu na ulinzi binafsi ndiyo mnashindwa kabisa kuwatetea WAISLAMU??

Jibu gani mnataka mpate kutoka SAUDI kuhusu katazo la kuingia Jeddah na Mecca bila kuwa mmepata chanjo?

Endeleeni na UJINGA wenu halafu zikifika siku za HIJA pandeni ndege nendeni mkawaambie Saudia kuwa Magufuli kasema Tanzania hakuna Corona.
 
Wanadai hawajapokea taarifa yoyote ila wakati huohuo wanasema eti kile kinachoonekana kwenye mitandao ya kijamii hakina ukweli wowote.

Kabla ya kuanza kupayuka ni bora angeenda japo kuuliza tu kwenye balozi za Nchi husika

1614932103149.png
 
Back
Top Bottom