Bajeti zetu ziendane na Hotuba za kwanza za marais wetu kwa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti zetu ziendane na Hotuba za kwanza za marais wetu kwa Bunge

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Danniair, Jun 17, 2012.

 1. D

  Danniair JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila mgombea urais huwa anamalengo ya kuifikisha nchi mahala pa zuri.
  Malengo hayo ndiyo hujinadi kwayo aombapo kura. Akisha kuteuliwa rais huenda ktk bunge (kutakamo
  patikana mawaziri) na kuyaeleza malengo hayo kiufasaha zaidi,ikiwa ni moja ya kazi ambazo wabunge
  watazifanya na kuzitetea. Hotuba hii hufuatiwa na machapisho ambayo husambazwa sehemu mbali mbali.

  Kinachonishangaza, nikuona kuwa inapotengenezwa bajeti, 'Contents' za hotuba hizi huwa
  hazikumbukwi hadi wananchi walalamike/kuzililia. Pia hata bajeti yenyewe naamini huwa haipelekwi Ikulu
  ili mwenye nchi aipambambanishe na ahadi zake kwa taifa. kisingizio kikiwa ni mihimili 3.
  Binafsi, sioni kama ktk swali hili kuna msamiati mihilimili unaohitajika. Kwani kila muhimili upo kwa ajili ya
  muhimili mwingine. Mfano, wizara ya sheria ni kwa ajili ya sheria za nchi na za kumlinda rais.
  Pia, waziri wa sheria shurti ateuliwe na rais. Hata kama si mbunge rais ana haki ya kumpatia ubunge
  na kisha kumteua kuwa waziri.

  Ushauri wangu kwa wahusika:
  1. Bajeti itanguliwe na kutusomea kilicho jili ktk mwaka wa fedha unaoisha.
  2. Bajeti isitupilie mbali ahadi za rais kwa wananchi kwani ndiyo dira yetu ya maendeleo.
  3. Hotuba za kwanza za marais kwa Bunge zichapishwe na kusambazwa hadi ngazi za serikali za mitaa
  kila mmoja ajipatie kopi yake - watakaozifungia maandazi waadhibiwe vikali
  4. Bajeti isisomwe bungeni hadi imepita kwa rais kwanza.
  5. n.k, n.k, n.k, n.k

  Mfano wa hotuba hii ni kilimo cha umwagiliaji alichoahidi rais mwaka 2000. Hadi leo hakuna kitu.
  Juzi tumeshuhudia Mh.Pinda akiwa Amerika ya Kusini akijionea kilimo hicho. Lakini la kushangaza
  kilimo hicho hakimo ktk bajeti. Jambo hili la kuzidharau hotuba za marais linawafanya wapinzani
  kuvuruga wananchi kwa maneno ya chuki kwa faida yao wenyewe.

  Asante
   
Loading...