Kuna ile sera ya ICT ya 2001 sijui hata inasemaje maana hapa katikati pametokea mageuzi mengi ya kiteknolojia, pia kunakipindi nilisikia jk anafanya mazungumzo na microsoft kututengenezea database na vitu kama hivyo serikalini, sijiu imeishia wapi?
Mimi nadhani kunahaja ya serikali kuwaamini watumishi wake inao waajiri na kuachana kabisa na huu upuuzi wa kutafuta akina gupta kama washauri elekezi kuamua ni mfumo gani unafaa na mashine gani zitumike maana hawa wapo kibiashara zaidi, Mimi naamini hawa ndio wanapotosha kwa kutoa ushauri elekezi unawao wapatia tenda na kuishauri serikali ijitoe katika kumaintain hizo mashine hivyo kulazimu kuwa na watu watakao kuwa wanazishughulikia muda wote na mwisho wa mwezi wanavuta fungu nene.
Kutengeneza website kunahitaji mtaalamu sawa, lakini kunahaja gani ya kutafuta kampuni itakayo kuwa inamaintain website ya idara kwa kufanya updates maintenance nk? huku si kupeana ulaji tu, na je wale walio ajiriwa wanafanya nini sasa ofisini?
Kibaya zaidi wanafunga mitambo na kuitegesha baada ya muda inastop inabidi waitwe kuja kurekebisha hapo tena fungu linazidi kuwa kubwa.
Sasa hii wakati mwingine inawafanya hata ma ict wetu kurelax maana karibu kila kitu wanafanya kutoka nje ya ofisi hivyo wanakosa ubunifu,
iandaliwe sera upya itoe mwongozo baada ya upembuzi yakinifu kuwa kila idara, ofisi nk inahitaji ict ya namna gani kuboresha na kuleta ufanisi wa kazi, waajiriwe vijana waliomaliza vyuo wapo wengi mtaani wafanye kazi, naamini wanaweza kabisa maana hawapo pale kugundua wala kudevelop program just kuafanya kulingana na sera sahihi zitakazo kuwepo.
Kwasasa sifikirii sana kudevelop masoftware nk ingawa sio vibaya, isipokuwa nguvu kubwa iwe ni kingiza mifumo yetu ya kiutendaji pale itapo bidi iweze kwenda na dunia ya leo. ni ngumu kuendelea kama hata mifumo yetu bado ipo kizamani, inamtia mtu uvivu hata kuja kuwekeza nchini