Kwa misingi mibovu ya kiuchumi iliyobomolewa na Kikwete na kuwekwa mipya na mizuri hili la bajeti kujitegemea ndiyo lilikuwa lengo, hata ukitazama Kikwete alipochukuwa tulikuwa wategemezi wa takriban asilimia 50 ya bajeti lakini katuacha tunategemea tunategemea kama asilimia 10 tu.
Uza mashangingi yote,nunua vitara na rav4,asietaka apande basi
Kwa sababu waliandika bajeti yetu ni trilion 23 wakati hatuwezi kukusanya hata trilion 11 kwa mwaka ( wastani kwa mwezi ni mil 900). Uwe unatumia akili na macho ili uweze kung'amua mambo ya kisanii!
Hiyo ni kwa TRA peke yake, kumbuka serikali ina magawio ilikowekeza, mashiraka ya umma, bonds n.k, mikopo etc tutafika tu usihofu
Labda nikusaidie kihesabu hapo..
ikiwa makusanyo yataendelea kuwa angalau 1.3T, then kwa mwaka ni 15.6T pungufu ya 6.4T kufikia 22T. Sasa kama ataendelea kubana matumizi na kuyapunguza yasiyo ya lazima kuna uwezekano mkubwa wa kuokoa hata 2-3T (mfano kukata safari zisizo na umuhimu, mashangingi, maadhimisho yasiyo ya lazima, n.k.)
Aidha, akiongeza ukusanyaji mapato katika sekta nyingine mfano madini, utalii, mauzo ya gas nje, mazao ya misitu, kilimo, ufugaji, n.k. hakika hiyo pungufu kuna uwezekano mkubwa sana wa kuimaliza ama kubakisha pengo dogo sana.
Jambo jema ni pale itakapofikia kukusanya angalau 1.6T kwa mwezi, kweli itakuwa ni neema kubwa kwa nchi hasahasa ikiwa usimamizi utaendelea kufanyika kwa ufanisi.
MKpo from Local banks na mashirika ya umma kama PSPF, NSSF, NHIF nk.
Watu watashangaa, JPM ndio kwanza ameanza kazi baada ya miezi 6 mtaona. Kuna sehemu bado hajazishika vizuri kama vile kwenye utalii, ukifika Serengeti pale uone foleni ya kulipa ya watalii utajiuliza hivi kweli zile pesa zote zinakwenda serikalini au kuna wajanja wachache pale wanafanya mchezo, hii nchi bana tutaelewana tu tuombe uzima wa JPM kuwashughulikia hawa waliofikiri wana hati miliki ya hii nchi. Hiyo bajeti ya T22 ni cha mtoto.
Mkuu bajeti yetu huwa ni tegemezi kwa asilimia 48 (48%). Usishangae, hiyo 22tn 52% tu ndiyo mapato ya ndani.
Bila shaka ulisha wahi kusikia 1. Nakisi ya bajeti ie badjet deficit 2. Bajeti ya Tz hufadhiliwa kwa kiwango cha 30+%
Mimi nasoma bajeti kila mwaka, nilishangaa sana Raisi aliposema mapato ya mwezi yanakaribia 1.3 Trillion.
Nikajiuliza kama matumizi ni 22T kama mwaka jana na tunakusanya 1.3 kwenye mwezi mzuri, inamaana hiyo tofauti ya pesa itatoka wapi? Au bajeti yetu ni maandishi tu?
Kama matumizi ya serikali kwa mwaka ni 22T, na inaendelea kuongezeka kila mwaka by the way, inabidi tukusanye sio chini ya 1.8 trillion kila mwezi.
acha ujinga wako na ujinga wa mpenda chini wako...a.k.a mpenda Kati...si ajabu ashakutafuna weweKwa misingi mibovu ya kiuchumi iliyobomolewa na Kikwete na kuwekwa mipya na mizuri hili la bajeti kujitegemea ndiyo lilikuwa lengo, hata ukitazama Kikwete alipochukuwa tulikuwa wategemezi wa takriban asilimia 50 ya bajeti lakini katuacha tunategemea tunategemea kama asilimia 10 tu.
Trilioni1.3 ilikuwa mpaka tarehe 16 Desemba, bado kuna siku 10 plus mwezi kukamilika bila shaka TRA wataweza kufikia hata zaidi ya trilioni 1.8
Kwa misingi mibovu ya kiuchumi iliyobomolewa na Kikwete na kuwekwa mipya na mizuri hili la bajeti kujitegemea ndiyo lilikuwa lengo, hata ukitazama Kikwete alipochukuwa tulikuwa wategemezi wa takriban asilimia 50 ya bajeti lakini katuacha tunategemea tunategemea kama asilimia 10 tu.