Bajeti ya serikali 2017/2018 kuwa Trillion 31.6

Bajeti ya serikali 2017/2018 kuwa Trillion 31.6

Hii bajeti ni zaidi ya majanga,eti Afya,elimu,maji sio vipaumbele kwa bajeti ya Magufur.Bali vipaumbele ni reli,na ndege,poor mikakati.
 
Kama wabunge wataipitisha hiyo bajeti,basi nitaandelea kupata uhakika kua wabunge wote ni wachumia tumbo ni sawa na walimu ambao hawawezi kugomea kitu chochote hata kama kinawakandamiza
 
Kabla ya kutuambia hii mpya wangeanza kutuambia ilyopita pita imetekelezwa kwa kiwango gani sio kukazana kuongeza tr na nafuu ya maisha hatuioni zaidi ya kuzidi kuumia
 
Kuna baadhi ya mikoa imesahaulika ktk mipango ya kimaendeleo au ni mtizamo wangu tu
 
All I can say: Magufuli ingawa ana nia njema na taifa letu (sijawahi kuwa na wasiwasi na hilo), ajifunze kufanya kazi within budgets. Hili la kwenda na kutoa amri hapa na pale...kwamba mambo yafanyike...kwa kutumia pesa za walipa kodi si njema kwetu wananchi. Kama baba wa familia, he has to have a priorities.

Issue ya Dodoma ni kitu kizuri. Lakini hakikuwa kwenye budget. Kwa hiyo ni kitu ambacho kimetumia resources za vipaumbele vingine. Kwa nini tusingejiwekea timeline kulifanikisha hili? na akalisimamia mwenyewe?

Hili la kununua ndege, ni jambo jema kabisa. Lakini lazima tukubali we need budget for this to happen. By the way tumeshawaanda watu wetu kuhandle biashara kubwa kama hii katika mda mfupi-with success? Maana kama wengi tujuavyo vitu vya bure ni vya bure. this SHOULD BE GRADUAL PROCESS. Otherwise tutarudi kule kule..kuona kwamba ATC ni shamba la bibi. Rwanda air ambaye imetu-inspire..wana zaidi ya miaka kumi na tano..walianza na ndege moja. Progress leo tunaiona.

La kujenga reli na miundombinu ni kitu chema pia, lakini mwisho wa siku tuangalie uwezo wetu unafikia wapi. Magufuli ni baba. Huwezi kununua gari kama watoto hawana uhakika na tiba au chakula. Ingawa kununua gari kunaweza kuisaidia familia kujikwamua..ikasonga mbele zaidi. But lazima watoto waishi. Kwa hiyo lazima tuwaangalie.

Swali la mishahara na maslahi ya wafanyakazi, tutake tusitake ni swala muhimu. Maana these people have families to feed. They have kids in school nk. Serikali inawetegemea hawa hawa kufanikisha haya maendeleo. Kwa hiyo hela wanazolipwa siyo wastage. Ni kuthamini utu wa mtu. Hatuna budi ku-invest katika watu wetu na kuwapa motisha.

Otherwise, yote Magufuli anayopambana nayo ni mema kabisa. Lazima kuumia wengi wetu tuumie. Huyu bwana ana nia ya dhati kabisa kulisogeza mbele taifa.

Chini ya MAGUFULI naamini tutapata maendeleo especially kwenye infrastructure. But at what cost?

Cha mwisho, waTanzania tubadilike. We live in a different world/country now. Lazima tukubali kwamba bila kipato halali mjini maisha yatakuwa ni ya woga na frustrations kila siku. Ukiona tunaongelea inter change Ubungo, Tazara au Reli..lazima tujue these things cost money. na sisi ndo tunaangaliwa tulipe hizo gharama! Lazima tukubali zile zama za kuchukulia pesa za umma kama zisizo na mwenye zimekwisha. Unaanza kazi leo unataka uwe na ghorofa masaki kwisha. I mean we have to start adjusting accordingly to live within our means. Una mashahara wa laki saba..unataka mtoto asome academy! Hizo zama kwisha. The earlier we recognize that, the better.

Uamuzi wa Magufuli kwamba tulipe kodi, Mashirika ya umma yalipe kodi na gharama za kujiendesha ni jambo jema kabisa. Imagine jeshi mnapewa budget halafu mnataka TANESCO iwape umeme bure..kwa sababu nyinyi ni taasisi nyeti. Imagine TRA inatoa misamaha mingi kwa sababu zisizo na mashiko nk. Lazima tukubali. Our government needed radical changes. And Magufuli is a radical leader. Kikubwa tumsaidie. Tuna haki ya kumkosoa Magufuli kama Kiongozi na Mtanzania mwenzetu. Lakini tusiwe negative tuu all the time. Haisaidii. Tanzania itaendelea kuwepo hata baada ya Magufuli na wewe na mimi. So lets be constructive in our criticism. Huwezi jua kuna mawili matatu yatamfikia na akiona ni mazuri akayafanyia kazi. And that will be a plus to our country.

Masanja
 
Utekelezaji wa ile ya 29Tr ni 33%! Hapo mnaoviziaga ajira serikalini kwa miaka hii 3+ MSAHAU. Kama hakuna pesa ya kumuajiri DAKTARI ambaye mahitaji ya utaalamu wake hayajawahi kupungua na daktari huyu anatolewa SADAKA Kenya akawe cheap labour, ndugu yangu unayesubiri serikali ikuajiri muulize baba yako kama kuna ardhi imebaki kule kijijini ila 2020 wahi sana shahada yako ya kura.
 
bila ai
Pamoja na kutolipa mishahara mipya ya watimishi iliyoidhinishwa katika bajeti hiyo lkn bado kuna upungufu huo. Swali la kujiuliza hiyo ya tr30+ itamudu? Kama siyo tu kuwekeana mitarakimu mingimingi isiyo na kichwa wala miguu.
Tena bila ya aibu mtu na suti yake anasoma mwelekeo wa Trl 32 wakati 29 haikuwezekana!!!
 
Wednesday, March 29, 2017
MPs see business as usual in the 2017/18 Budget


pic+MPs+see+business.jpg

MPs pay attention to Minister for Finance and Planning Philip Mpango when he presented the 2017/18 Budget Framework in Parliament Dodoma yesterday. PHOTO|BUNGE

In Summary
  • Speaking at Bunge grounds after Finance and Planning minister Philip Mpango presented the framework for the next financial year yesterday, some MPs said it was business as usual as much was not attained in development expenditure.

By Alawi Masare @AMasare malawi@tz.nationmedia.com

Dodoma. Some MPs see the next Budget as having nothing new, since 60 per cent of money for development projects for 2016/17 is yet to be released.

Speaking at Bunge grounds after Finance and Planning minister Philip Mpango presented the framework for the next financial year yesterday, some MPs said it was business as usual as much was not attained in development expenditure.

http://www.thecitizen.co.tz/News/MP...-18-Budget/1840340-3868856-9ap2jfz/index.html


BAK hivi ile ya mwaka jana imetekelezekaje au kwa asilimia ngapi vile
 
Ndugu waungwana,
Hivi Serikali na Bunge wanamatatizo gani na namba??

Kiini cha andiko langu,​
Bajeti kwa mwaka 2016/17 ilikuwa Tillioni 29.5, mwaka huu unao anza July 31.7

Nukuu kutoka taarifa ya Waziri wa fedha Bungeni Dodoma
"Taarifa za awali zinaonesha kuwa, Pato la Taifa kwa mwaka 2016 lilikua kwa wastani wa asilimia 7.0, sawa na ilivyokuwa mwaka 2015. Hali hii imechangiwa na kasi kubwa ya ukuaji katika shughuli za: Uchimbaji Madini na Mawe (asilimia 16.5); Usafirishaji na Hifadhi ya Mizigo (asilimia 15.6); Habari na Mawasiliano (asilimia 13.5); na Huduma za Kifedha (asilimia 11.3). Aidha, kwa upande wa utekelezaji wa azma ya Taifa ya kujenga uchumi wa viwanda, shughuli za uzalishaji viwandani zilizidi kuimarika, zikiongezeka kwa asilimia 7.8, ikilinganishwa na asilimia 6.5 mwaka 2015"

"Kwa mwaka 2016/17 Serikali ilitenga shilingi bilioni 11,820.503 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 8,702.697 zilikuwa za ndani na bilioni 3,117.805 fedha za nje. Hadi Februari 2017, fedha zilizokuwa zimetolewa ni shilingi bilioni 3,975.4, ikijumuisha fedha zilizotolewa kwa Halmashauri, sawa na asilimia 34 ya bajeti ya maendeleo. Kati ya kiasi hicho, fedha za ndani zilikuwa shilingi bilioni 3,103.6 na fedha za nje shilingi bilioni 871.8"

"Hadi kufikia Februari 2017, mapato kutoka vyanzo vyote yalifikia sh. bilioni 15,372.4 sawa na asilimia 79 ya lengo la kipindi hicho. Kati ya hizo:
  • (i) Mapato ya kodi yalifikia shilingi bilioni 9,306.0 sawa na asilimia 95 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 9,764.2;
  • (ii) Mapato yasiyo ya kodi yalifikia shilingi bilioni 1,305.7 sawa na asilimia 72.5 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 1,806.2;
  • (iii) Mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa yalikuwa shilingi bilioni 310.6 sawa na asilimia 70 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 443.6;
  • (iv) Mikopo ya ndani ilifikia shilingi bilioni 3,506.7 sawa na asilimia 78 ya makadirio ya shilingi bilioni 4,479.6 katika kipindi hicho; na
  • (v) Misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ilikuwa shilingi bilioni 1,253.6, sawa na asilimia 40 ya lengo la kipindi hicho la shilingi bilioni 3,117.2"

Hapa somo la historia linahusika. Kama katika historia ya mapato yetu hatujawahi kukusanya zaidi ya Tsh 20 Tillioni, iweje tupange bajeti ya Tillioni 32 kasoro???

Kuna miujiza gani tutafanya kufikia mapato hayo ili hali historia ya nyuma na mwelekeo wa hali ya uchumi siku zijazo havitupi matumaini hayo???

Watalaam wetu vipi jamani? Hili nalo linahitaji shule?
Katika familia, kuna watu wanapanga bajeti zao za mwaka kuna mapato na matumizi. Lazima uweke mapato na matumizi yanayo endana na uhalisia wa mambo. Kuna kupata zaidi au kidogo pia kuna kutumia zaidi kuliko au kidogo kuliko makadirio. Ila tofauti hizi siyo kubwa kiasi hicho karibu mara mbili ya uhalisia wa mambo, iweje kwa Serikali hata kama ni Nchi?

Hii ni kuishi kwa matumaini. Tunalisha akiri zetu kuwa hiki nakile kitafanyika ila kila mwaka hatufikii malengo hayo. Kwa nini tusipange kulingana na mapato yetu???

Kama huna uwezo wa kukusanya zaidi ya tillioni 17 kwa mwaka kwa nini usipange bajeti chini ya Tillioni 17?​
 
bajeti ya kwenye makaratasi,utekelezaji hawatekelezi
 
Halafu ndio tunasema tunasomesha wachumi ambao wanashindwa hata kuandika maandiko ama ripoti ya hali ya uchumi wa nchi na kuipublish mtandaoni ili mwananchi at least mwenye elimu ya form six aubform 4 aweze jua tunakwenda wapi.
 
Ila swala la Namba ni ugonjwa wa Taifa hivyo sishangai kupanga kutumia usichoweza kupata.
 
Ila swala la Namba ni ugonjwa wa Taifa hivyo sishangai kupanga kutumia usichoweza kupata.
Umeonaa eeeh!
Namba shidaaah! Watu wanachekelea kwamba miradi yao itafanywa bila kuangalia wala kuchukua juhudi za kujua mapato na matumizi ya serikali kwa miaka iliyopita. Ila kwa nini na wanao itwa wtalaam wa wizara au mamlaka husika wapange kutumia fedha nyingi waiyoweza kupata?

Watalaam mtujibu hapa.
 
kuna instuments zinazotumika katika kuhakikisha serikali haikosi fedha,ikiwa ni pamoja na mauzo ya tressury bills,bonds nk,yenyewe ndio inayopanga ni kiasigani inunue na inunue kwa sh ngapi hao wawekezaji wapo wengi ila huweka nao masharti yao pia,,kwenye soko la kukopa ndani hio ndio istument kubwa,la pia kuna soko la nje na nje kuna namna nyingi mno za kupata fedha kama nchi lakini pia risk huwa ni kubwa. .Miradi mingine inakuwa financed directly kwenye mradi husika kwahio literally hesabu inaweza isiwe 100% balanced in utekelezaji physically ndio jambo la msingi.
Inakuwa ngumu kuague na illiterate wa uchumi na fedha unaague na mtu aliemezeshwa uongo wa mwenyekiti mfalme wake tu.Ukitaka kuelewa fungua akili na usome zaidi usibwabwaje tu.
 
kuporomoka kwa soko la hisa leo inategemea nani ni key players wa soko hilo na kwanini hawaendei kule kupata fedha au kipo chanzo kingine cha kupata fedha.Hii hali ni ya muda mfupi sana ndio maana taarifa za habari kimataifa hutoa taarifa za matokeo ya soko la hisa kila saa,kuna a lot of factoras xinafanya watu wauze au wanunue in agiven time hasa ikiwemo infomations zinazoweza kuongeza uchumi au kuua uchumi wa sehemu husika.Kwa mwandishi huo ni mwisho wa kufikiri na kuona hii ni ishu kubwa.
 
Back
Top Bottom