Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2020/21

Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2020/21

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
710
Reaction score
1,365
‪BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU MWAKA 2020/21

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Aprili Mosi, 2020 amewasilisha bungeni bajeti ya Ofisi yake ambapo amesema hadi kufikia Machi, 2020 Tsh Trilioni 1.28 zimetumika katika ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere na umekamilika kwa asilimia 10.74.

“Nampongeza Rais Magufuli kwani tumeshuhudia maendeleo makubwa nchini ikiwamo miundombinu, huduma za kiuchumi na kijamii, utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na kuhamasisha uwekezaji.

“Tangu kugundulika kwa ugonjwa wa Corona nchini, Serikali inafanya juhudi kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuimarisha ukaguzi, upimaji na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini na kutoa matibabu kwa wanaothibitishwa” Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
_
“Ujenzi wa SGR, ufufuaji ATCL, ufufuaji wa shirika la mali za ushirika, ujenzi bwawa la ufuaji umeme, uboreshaji miundombinu ya maji, elimu na afya ni kati ya hatua za msingi katika kuhakikisha Tanzania inafika uchumi wa kati. ‬
_
Vijiji vilivyounganishwa umeme nchini vimeongezeka kutoka vijiji 2118 mwaka 2015 hadi vijiji 9001 kufikia mwezi Machi, 2020 chini ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA).
_
Kufikia Machi, 2020, Serikali imenunua ndege 8 mpya zenye thamani ya Sh. Trilioni 1.27 na tayari malipo ya awali ya Sh. Bil 85.7 yametengwa kwa ajili ya ununuzi wa ndege zingine 3 mpya.
_
Bajeti ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi imeongezeka kutoka sh. Bil. 31 mwaka 2015 hadi Bil. 269 kwa mwaka 2019 .
_
Serikali imegharamia ujenzi wa Zahanati 1198, ukarabati na ujenzi wa Vituo vya Afya vipya 487, Hospitali za Halmashauri za Wilaya 69, na Hospitali za Mikoa 10.
_
Serikali imeongeza mikopo katika Elimu ya Juu kutoka Sh. Bil 365 mwaka 2015 hadi Sh. Bil 450 mwaka 2019 ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu.
_
Changamoto ya maji imetatuliwa kwa kutekeleza ujenzi na ukarabati wa miradi ya maji 1423, kati ya hiyo 772 imekamilika ambapo miradi 710 vijijini na miradi 82 mijini.
_
Maduhuli ya Serikali yatokanayo na Sekta ya Madini yameongezeka kutoka Sh. Bil 205.2 mwaka 2015/2016 hadi Bil 346.6 mwaka 2018/2019, na mwaka 2019/2020 Serikali inatarajia kukusanya maduhuli Bil. 471.
_
Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa Bil. 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa Trilioni 1.3 mwaka 2019 hii ni kutokana na Serikali kuimarisha matumizi ya mifumo ya mapato kwa njia ya kielektroniki.
_
Tangu mwaka 2015 hadi sasa, Serikali imeokoa Sh. Bil 19.83 ya mishahara kwa kuwaondoa watumishi hewa 19,708 na vyeti vya kughushi 15,411.
_
Jumla ya Watumishi 15,361 wa Wizara na Taasisi za Serikali wamehamia Dodoma, kwa sasa maandalizi ya ujenzi wa majengo ya awamu ya pili na ujenzi wa barabara kiwango cha lami katika mji wa Serikali yanaendelea.
_
“Naielekeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutekeleza ipasavyo Mpango kabambe wa Jiji la Dodoma ili kuhakikisha mji wa Dodoma unapangwa na unaendelezwa bila kurudia makosa yalifanyika kwenye majiji mengine.
_
“Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za jamii nchini kwenye Awamu ya Tano umezalisha jumla ya ajira Mil 12.6.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana kiranja mkuu! Tunakukubari mkuu! Chapa kazi.
 
Sijaelewa hapa kama kuna mtu kaelewa naomba nisaidiwe, Hilo bwawa nilisikia gharama zake zote ni trilioni 6 sasa inakuaje ujenzi wa asilimia kumi yake iwe trilioni 1.28?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafanikio makubwa sana, pongezi kwa serikali.
 
Mambo ya afya,SGR,ukusanyaji mapato,ajira,umeme,maji na umeme havipo chini ya ofisi ya waziri mkuu sasa kwa nini waziri mkuu azisemee???
 
Back
Top Bottom