Bajeti ya Magufuli yamtishia Mkullo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Magufuli yamtishia Mkullo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtoka Mbali, Jun 4, 2011.

 1. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  KIPAUMBELE cha serikali katika Bajeti inayotarajiwa kusomwa wiki ijayo kitakuwa ni miundombinu baada ya kuelezwa kwamba Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk John Magufuli imetengewa kiasi kinachokaribia Sh1.5 trilioni.Kiasi hicho cha fedha ambacho ni kikubwa kupita bajeti ya wizara zote nchini (ukiondoa Ofisi ya Waziri Mkuu), ni sawa na asilimia 11.53 ya bajeti nzima ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 inayokadiriwa kuwa itafikia Sh13 trilioni.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba alisema kutokana na kutengewa kiasi hicho, serikali sasa itakuwa na uwezo wa kujenga madaraja katika maeneo mbalimbali likiwamo lile la Kigamboni, Dar es Salaam; Mto Malagarasi uliopo mkoani Kigoma na Mto Kilombero.

  "Takwimu zinaonyesha tangu tupate Uhuru hadi sasa barabara zetu zipo katika kiwango cha lami kwa kilomita 6,000, lakini mipango ya wizara baada ya miaka miwili ijayo ni iwe imefikia kilomita 11,500," alisema Serukamba na kuongeza:

  "Magufuli amefanya kazi nzuri na bajeti yake imejitahidi kugusa sehemu zote za Tanzania."Alisema kamati yake imemtaka Dk Magufuli kuendela kusimamia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuendelea kubomoa nyumba ambazo zinastahili na kulipa fidia kwa wale wanaostahili.

  Kwa mujibu wa Vitabu vya Makadirio vya Bajeti ya Serikali ambavyo Mwananchi limeviona, Wizara ya Ujenzi imetengewa kiasi cha Sh 1,250,976,939,000 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na kiasi cha Sh245,437,094,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida hivyo kufanya jumla ya fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya wizara hiyo kufikia Sh1,496,414,043,000.

  Fedha hizo ni nyongeza ya asilimia 29 ya kiasi kilichotengwa katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 31, mwaka huu ambacho kilikuwa Sh1.064 trilioni zikiwemo Sh871.553bilioni za maendeleo na Sh293.429 za matumizi ya kawaida.

  Kauli ya Mkulo
  Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alipoulizwa kuhusu bajeti hiyo ya Sh1.5 trilioni kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi alisema:"Kama kamati imepitisha kiasi hicho cha fedha basi waseme na vyanzo vya fedha hizo, si kupitisha tu," alisema Mkulo.

  Alisema ni lazima bajeti iendane na uwezo wa serikali kwa wakati uliopo hivyo wasiwadanganye wananchi… "Mwulize Serukamba anajua atakapopata fedha hizo. Mimi najiandaa kwenda kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha tukienda Dodoma (bungeni) na huu si wakati wa kutafuta 'popularity' (umaarufu)."

  Uchukuzi wako gizani
  Serukamba ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), alisema kamati yake imepitisha bajeti ya wizara mbili na kukwamisha ya Uchukuzi kwa kuwa serikali haijaweka fedha za kuboresha reli na za kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

  "Tunashangaa kwa nini serikali haioni kama suala la Reli ni muhimu. Ni lazima iweke fedha humo. Tumesisitiza kwenye reli lakini fedha hazipo. Inawezekana mpango upo, lakini kama fedha hazipo kwenye vitabu maana yake hakuna kitu," alisema Serukamba.

  Alisema reli inahitaji kiasi cha Sh240 bilioni lakini inashangaza Wizara ya Fedha na Uchumi kuwekewa kiasi cha Sh129 bilioni cha matumizi mengineyo."Bajeti nzima ya mwaka huu ni Sh13.5 trilioni hivyo fedha za matumizi mengine zipo nyingi tu ndani yake ambazo tunaweza kuzipunguza na kuziweka kwenye reli na ATCL," alisema Serukamba.

  Kwa upande wa Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia alisema kamati hiyo imepitisha Sh64 bilioni kwa kuwa imeridhika na maelezo ya wizara hiyo."Mambo watakayofanya ni pamoja na mkongo wa taifa wa mawasiliano, anuani za makazi na fedha za utafiti zipo humo na pia kuhakikisha mitandao ya simu iwepo ili nchini kote kuwe na mawasiliano," alisema Serukamba.

  Waziri Mkuu yatengewa Sh3.2trilioni
  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala imepitisha mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inayofikia Sh3.2 trilioni.

  Kamati hiyo imepitisha mapendekezo hayo huku ikiitaka Tamisemi kuweka kipaumbele katika miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zote nchini.Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika alisema kati ya fedha hizo, Sh2.3 trilioni zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na zilizobaki zitatumika kulipa mishahara watumishi wake.

  Alisema hiyo itaziwezesha halmashauri nchini kusimamia miradi yake na kuongeza mapato ambayo yatatumika kwenye zake shughuli mbalimbali za kimaendeleo.“Matumaini yangu ni kuhakikisha kuwa, fedha hizi zinatumika kwa ajili ya kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kulipa mishahara watumishi wake, jambo ambalo tunaamini linawezekana,” alisema Mkuchika.

  Alisema kuwa wizara hiyo imeiomba kamati hiyo kuwaachia fedha zinazotokana na miradi ya maendeleo ili waweze kuboresha miradi hiyo ambayo itachangia kuimarisha shughuli za kimaendeleo.Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana ameitaka Wizara hiyo kuwashughulikia watendaji wasio waadilifu na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

  “Kila mkoa una bajeti yake, lengo ni kuimarisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao, kutokana na hali hiyo watendaji wasio waadilifu wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Chana.

  Kamati ya Makamba yakubali bajeti
  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepitisha mapendekezo ya bajeti ya Wizara hiyo ambayo ni Sh404.4 bilioni lakini ikiitaka kuweka vipaumbele katika miradi mipya ya umeme pamoja na kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo wa majini katika maeneo yanayozunguka migodi.

  Mwenyekiti wa Kamati hiyo January Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa, kati ya fedha hizo, Sh327 bilioni zitatumika kwa ajili ya miradi mipya ya maendeleo na zilizobaki kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

  Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) alisema kamati hiyo imeitaka Wizara ya Nishati na Madini kupeleka umeme vijijini ili wananchi wa aina zote waweze kunufaika na huduma hiyo tofauti na sasa inavyopatikana maeneo mengi ya mjini pekee.“Tumeitaka Wizara kuhakikisha kuwa, bajeti yake inaweka kipaumbele kwenye miradi mipya ya umeme na kusambaza hadi vijijini ili kila mmoja aweze kunufaika na huduma hiyo ambayo imeenea mjini,” alisema Makamba.

  Alisema mbali na fedha hizo, Wizara ilitenga kiasi cha Sh1.3 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo katika vijiji vinavyozunguka migodi ili waweze kufanya kazi zao katika hali nzuri na mazingira ya kisasa, jambo ambalo wanaamini linaweza kupunguza migogoro.

  Imeandaliwa na Boniface Meena, Patricia Kimelemeta na Furaha Maugo kwa kushirikiana na Mtoka Mbali


   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  huyu mtu ana akili timamu kweli? hivi kuna kutafuta umaarufu tena kwenye kutekeleza sera zenu za ccm? au bajeti ya chai imeguswa ndio maana mnan'gaka kama chiligati
   
 3. e

  ejogo JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa kila kitu kizuri mtu anachotaka kukifanya anaambiwa anatafuta umaarufu, tutafika kweli!!!!
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mwenye hazina ni Mkullo ndio anajua serikali inauwezo kiasi gani! ni ajabu mmezoea kudanganywa bajeti bila fedha ya nini? waainishe vyanzo vya kupata hizo fedha ndipo iitwe kazi nzuri! mipango na matumizi ni vitu2 tofauti kabisa.
   
 5. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona ya waziri mkuu kubwa hashangai, kilaza nkulo!
   
 6. I

  Igembe Nsabo Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkulo Mbona hajasemea hii ambayo kiwango kikubwa ni Recurent in nature!! (Matumizi ya kawaida!???), mimi nilitegemea asilimia kubwa ya pesa za Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa (OWM - TAMISEMI) zingekuwa za Development in Nature (Miradi ya Maendeleo na Si kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida).

  Anapo washambulia watu wa Ujenzi kuwa pesa watatoa wapi na wanatafuta umaarufu, sie watanzania hatuwezi kumuelewa, tumeona kazi nzuri aliyofanya Magufuri akiwa kama waziri wa Ujenzi, na tuliona Mapungufu yaliyojitokeza wakati yeye yuko nje ya Wizara hiyo. Watu kama akina Mkulo wako wengi katika Utawala wa Bwana Jakaya Kikwete, na ndio hao ambao ni wanaliletea matatizo taifa hili. This people are les focused, wao kwao kipaumbele ni starehe na unnessary expenditure kwa kujilipa malipo ambayo siyo halali kama zile za PPF (za Group endowments) na ndio maana anazitetea siku zote.
   
 7. i

  iMind JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Kwa hili Mkulo kaongea ukweli, bajeti lazima iendane na mapato. Ukipitisha bajeti ya 1.5 tr na hadi mwisho wa mwaka unapata 10 bil haisaidii. So ni vyema kuweka mipango inayotekelezeka kuliko kuwadanganya wananchi. Binafsi sioni kosa la Mkulo.
   
 8. Balungi

  Balungi Senior Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Si mnamjua mkulo, sasa mnahangaika nae vp?
  Subirini muone
   
 9. M

  Masuke JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Amesema bajeti ni trilion 12.8, kuna ubaya gani kutoa trilion 1.5 kwa ajili ya wizara ya ujenzi, ambayo zaidi ya trilion moja inaenda kuimarisha barabara zetu, wangekuwa wameomba nusu ya bajeti nzima angeweza kung'aka, lakini sasa kile walichoomba hakijafika hata robo.
   
 10. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamaa anavyopenda sifa mbona tutamkoma wanazidi kumjengea mazingira mazuri ya 2015 bila wao kujua
   
 11. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tatizo liko wapi kama pesa zitatumika vizuri kwenye miradi ya maendeleo bila ufisadi?tatizo liko wapi Magufuli akiwa Rais 2015?
   
 12. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Back off..... sio kila kitu ni 2015 hii ni nchi na barabara ni muhimu kwa taifa
  kama wamemtengea pesa nyingi na akazitumia kwa maslahi ya taifa kuna tatizo gani?
  hacha chuki kama kuna mtendaji bora ndani ya ccm mpe sifa,
  hii ni nchi inaitaji watu wenye uzalendo sio lazima wawe chadema na uraisi 2015 ni wananchi wata hamu, nikiwa na maana bila kura kuchakachuliwa
   
 13. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi kila kitu kikipangwa kifanyike kwa ufanisi siku hizi,hoja inakuwa ni popularity na urais 2015?!!hadi waziri Mkulo nae anasema hilo hilo..haa,give us a break!!!yaani kakosa hoja nyingine ya kusema,kama hiyo bajeti haiwezekani!kwani hatuhitaji miundombinu bora?nchi hii bwana!
   
 14. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Mbona baadhi hatulizi za wizara ya fedha - contingency+emergency(?) - about 400 billion mnaona tabu na za barabara? Jamani huko mikoani barabara mbovu sana ukishatoka zile kuu za lami. Hata hapa Dar penyewe mbovu hata hazitamaniki. Kama bajeti ina mwelekeo mzuri kuzimulika, wacha Mapadlock achape kazi. Usumbufu kwenye barabara mbovu ni kero kubwa na inagharimu sana.
   
 15. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Huyo sasa ni waziri wa fedha Bwn Mustpha Mkulo, badala ya kubuni au kutafuta vyanzo vya mapato ili kusaport maendeleo ya nchi, tayari yuko kwenye defensive side!!!!!!!! Kama waziri wa fedha anangaka hivyo tutegemee nini kwenye budget ya safari hii???????????
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nadhani kuna Mambo mengine twaitaji kuyafikia kwa mapana. Wizara ya Dr. Magufuri ni nyeti sana, pasibo bajeti ya kueleweka tusitegemee maendeleo. Hii ni wizara kwa ujenzi pamoja na barabara. Hapa yapaswa tutambue 85% ya watanzania twategemea usafiri kwa njia ya ardhi ktk kusafirisha mazao yetu toka mashambani, mifugo yetu kwenda mnadani, mizigo yetu, usafiri pale tuwapo safirini. Pasipo hii wizira mawasiliano kt ya mkoa kwa mkoa na nchi kwa ujumla yatakua madogo na hafifu, nchi kutawalika itakuwa tatizo pia. Pasipo bajeti kubwa tusafau kuhusu ujenzi wa madaraja bora. TUACHENI SIASA ZA KIPUUZI KTK MAMBO SERIOUS. Dr. Magufuri anapaswa kuungwa mkono. Nadhani utendaji wake twaujua, yeye ni zaidi ya mwanasiasa, ni mtendaji!
   
 17. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kabla hamjafika mbali na kuhoji bajeti ya kusadikika, mnatakiwa mhoji matumizi ya bajeti inayoishia mwezi huu. Kushindwa kuchanganua bajeti ya sasa hivi na kushabikia ya kesho, isiotabirika, inaonesha waTZ walivyo Mufilisi wa kufikiri na wabunge wao wamekaa kimaslahi zaidi. AMKENI WATANZANIA MNADANGANYWA NA WANASIASA.
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi naona wote wako sawa. Mkulo yuko sahihi kwa sababu ndo anaejua kilichopo kwenye chungu na magufuli yupo sahihi pia kwa sababu ndo anachotaka apakuliwe kwenye sahani yake bila kujali sahani zingine. Lamhimu hapa si Mkulo kulalamika bali amuite magufuli na amuoneshe kuwa tulichonacho ni hichi na kwa sababu ni cha wote wewe utapata hiki ili na wengine wapate. KIMYAKIMYA (si kwenye vyombo vya habari. Halafu pia mkulo usipuuzie vyanzo vya mapato cinavyoainishwa na asasi za kirai, vyama vya wafanyakazi na vyama vya upinzani. Ni hayo tu.
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  [video]http://youtu.be/GPMw8r1rFQc[/video]
   
 20. g

  gabagaba Member

  #20
  Jun 4, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tutafika mjomba ila tutachelewa
   
Loading...