Bajeti ya leo; Mtizamo wangu......

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Nimesikia kwamba kuna ongezeko la bajeti kufikia zaidi ya Trilioni 15, mtazamo wangu ni kwamba nyongeza hii kimsingi inaenda kwenye matumizi ya kawaida na sio maendeleo so sidhani kama italeta impact yoyote kwa sisi wa huku uswahilini.

Kutakuwa na ongezeko la kodi kwenye vinywaji na sigara kama kawaida maana huko ndiko tumeona kwa kupata mapato huku tukiachia zaidi ya trilioni moja ikipotea kwa misamaha ya kodi isiyo na kichwa wala miguu.

Sidhani kama itaangalia tatizo kubwa ambalo tumekabiliana nalo katika mwaka uliopita wa fedha ambalo ni mfumuko wa bei uliokadiriwa kufikia 30% huku tukisingizia kupanda kwa bei ya mafuta na kadhalika na kadhalika.

Sina uhakika sana lakini tatizo la nishati ya umeme bado naona kama hadithi maana sidhani kama kutakuwa na mipango inayoeleweka sana ya namna sahihi ya kutatua tatizo zaidi ya kutenga fedha kulipa madeni inayodaiwa tanesco na soon kurudi kwenye mgao kama kawaida.

Tatizo la kuporomoka kwa shilingi yetu sijaona kama kuna jitihada za makusudi za kuliangalia hilo maana linachangia kwa kiasi kikubwa sana mfumuko wa bei unaoikabili nchi kwa sasa.

Haya ni baadhi ya yale ninayoona mimi kwamba yanakuja na kupita kila bajeti inaposomwa.....................kila siku ni Blah Blah Blah...........
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom